Mwigulu amshukia Mnyika, amuuliza ana uhusiano na wauaji wa Kibiti?

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Mnyika alisema serikali kama imeshindwa kuwadhibiti wauaji wa Kibiti basi hawataweza kuwadhibiti watanzania wakiamua kutumia silaha yao ya kura.

Mwigulu amesema ni vema akawa makini akiwa anaongea, na kusema angeweza kumuuliza maswalia ambayo angeshindwa kuyajibu, moja ni kama ana uhusiano na hao wahalifu mpaka akadhani wameshinda walikuwa wangapi na wamebaki wangapi?

Mwigulu amesema kama anajua hayo mauaji yataendelea maeneo mengine itabidi watafute connection kwa nini anajua yataendelea maeneo mengine kwa kuwa wanauawa wa CCM tu.

 
Hayo majibu ya kitoto sana...
Hoja siyo kuwa yataendelea sehemu nyingine, hizo hatua zilizochukuliwa kizuia hayo mauaji imekuaje ziendelee kuacha mianya ya mauaji kuendelea kutokea...
Kuna kitu nlitaka kukiandika lakini naona ntaitwa mchochezi!
 
Hao wangapi ambao wamebaki, kwa nini waendelee kubaki? Kama kuna waliokamatwa au kupotezwa mbona bado hatuoni unafuu huko kibiti? Na kama ni political motivated kwa nini intelejensia iliyogundua hivyo haijaweza kuwamaliza na kuwaanika hao wanasiasa walioingiza Taifa katika huu umwagaji wa damu. What's really going on Mr Waziri?
 
Analeta usiasa kwenye mambo serious????

Wanaokufa ni watanzania na wala sio ccm. Anajua kauri hiyo ina impact gani au karopoka tu??

Anahamasisha wasio wanachama wa ccm wafurahi badala ya kuhuzunika mauwaji wa watanzania wenzao!!!

Bure kabisa. Hawa viongozi wajifunze kauri
 
Wanauwawa hao aliowataja Mwigulu,sbb ndio wamedhulumu watu kwa muda mrefu
Huyu Waziri alizoea kuleta siasa za ugaidi wa Chadema na kina Lwakatale,akasema ana ushahidi wa duniani na mbinguni...Sasa hao wahuni na magaidi wa Kibiti wanamshindaje?

Huyu bwana mdogo Analeta siasa,alikuwa anajidai kujiita "Field Marshal",alifikiri ni cheo kinapatikana baada ya kutesa wapinzani na kubambikia kesi...Unajiita Field Marshall kwa kwenda JKT wiki tatu tena ukitokea Bungeni?Na picha unapiga kabisa ili urushe insta??Huna adabu kabisa we dogo

Watu wanakufa bado unaleta siasa?Kaa pembeni achia wizara wanaume wafanye kazi
 
Back
Top Bottom