VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Sababu zipo nyingi.lakini hizi ni chache:
Kwanza,Samson Mwigamba amejijengea jina akiwa CHADEMA. Hata makala zake za 'Kalamu ya Mwigamba' za kwenye Tanzania Daima zinauzika kwakuwa tu yupo CHADEMA na akiwa kiongozi huko. Huo ndio ukweli. Mwigamba wa mwaka 2003 si huyu wa 2013. Kutoka Mwalimu hadi Mwenyekiti wa chama Arusha. Sasa, ni wakati wake kulipa fadhila na kukitumikia chama chake. Aachwe aamue kubaki CHADEMA.
Pili, CHADEMA inampigania. Mara baada ya Mwigamba kukamatwa na kushtakiwa kwa kosa la uchochezi(akiwa pamoja na Absalom Kibanda), CHADEMA ilimwaga Mawakili Wasomi kumlinda kisheria Mwigamba. Tangu siku ya kwanza ya kesi hadi sasa, Mwigamba analindwa,anasaidiwa, anatetewa na kupiganiwa. Naye anaonesha uzalendo kwa chama kiutumishi na kiutawala.Ya Arusha na mitandaoni yanajadilika na kusameheka. Mwigamba hawezi kuhama CHADEMA kirahisi.
Tatu, CHADEMA kimeimarika na kutambulika kama chama kikuu cha upinzani nchini. Ni mpinzani wa kweli wa CCM yetu iliyo madarakani tangu 1977 ilipoanzishwa ikirithi utawala wa TANU ulioanza 1961. CHADEMA kwasasa si chama cha kubeza. Kinasumbua vichwa vya makada na viongozi wa CCM.Si kitu kidogo kuwa ndani ya CHADEMA,tena katika ngazi ya Mwigamba. Mchezaji mzuri hasusi mechi kirahisi.Hununa na kucheka baadaye kidogo. Mwigamba yuko tayari kuingia na kucheza mechi ya 2014 na 2015 akivaa jezi ya CHADEMA. Si rahisi kususa!
Nne, mambo ya Arusha yamekuzwa mno. Hayakutokea kama yarivyoripotiwa. Kwakuwa Mwigamba naye ni mwandishi wa habari, atakuwa ameshang'amua. Amejua jinsi anavyochochewa kuasi na kuhama CHADEMA. Kimsingi, Mwigamba ni mtu makini. Hawezi kuyumbisha chama lakini pia hatathubutu.
Tano, Mwigamba anaijua Katiba na Kanuni za CHADEMA. Atachukua hatua stahiki kikanuni pale ambapo atahitaji kukosoa kwa ajili ya maboresho. Hatarudia kujiita na kufanya alivyofanya. Alitereza. Alikosea. Anajua fika kuwa kwasasa yeye anaihitaji CHADEMA na CHADEMA inamhitaji. Ataiboresha kikanuni. Hawezi kutumika kirahisi kama inavyoripotiwa.
Sita, makada wa vyama vingine tuache kufuatilia na kuchochea yasiyotuhusu. Kwa CHADEMA ya sasa, hategemewi mtu.Hakuna hata mmoja aliye maarufu kuliko chama. Ushushushu na umafia toka nje sasa unakumbana haraka na 'a great wall'. Huu ni ukweli mchungu kuusema.
Hatahivyo, CCM yetu iko imara sana. Haihitaji kuchonganisha na kuvuna wanachama wa CHADEMA. Inajipanga na kujiimarisha zaidi kila kukicha kwa mpambano wa fainali hapo 2014 na 2015. Wachezaji wetu wana morali ya hali ya juu. Wako tayari kupata ushindi. Sasahivi, tumetingwa na kutekeleza Ilani yetu ya 2010-2015. Tukutane uwanjani 2014 na 2015. Kila la kheri wapinzani wetu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Saaam.