Mkuu
Bramo, amenisihi kutoa maoni yangu juu ya utofauti uliopo kati ya Juliana Shonza, Mtela Mwampamba na Samson Mwigamba (wakiwa CHADEMA). Najaribu tu kusikika hapa:
Juliana Shonza na
Mtela Mwampamba(vijana) sasa ni makada wenzetu wa CCM. Mwigamba bado yu CHADEMA. Makada hawa wanaweza kutofautishwa hata wakiwa CHADEMA.
Kwanza,
Juliana Shonza na
Mtela Mwampamba walikuwa BAVICHA wakati Mwigamba alikuwa Mwenyekiti wa mkoa Arusha. Hapa pana jambo zito. BAVICHA ni kiwanda cha CHADEMA kutengeneza makamanda imara wa chama na viongozi wanaofuata. Hivyobasi, BAVICHA ni sehemu adimu na adhimu. Si sehemu ya mchezo.
Vijana husika walikuwa humo.Tena mmoja alikuwa Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa (Shonza). Mwigamba yeye ameshaiva na kuivika.Katika hali ya kawaida,hata katika familia zetu,onyo kali mno hupewa kijana mdogo kuliko mtu mzima hata kwa kosa moja. Hii ni kwasababu, kijana bado ana muda mrefu wa kujifunza na kujirekebisha. Akirudia tena,adhabu kali hufuata. Ndivyo ilivyokuwa.
Pili,
Juliana Shonza Mtela Mwampamba na Mwigamba wote walikiuka Katiba na Kanuni za chama. Na wote walisimamishwa. Lakini vijana waliendeleza kiburi. Walidai mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuwa wao bado wako BAVICHA na 'hakuna' wa kuwatisha. Shonza alikuwa akisema "Mimi bado Makamu Mwenyekiti BAVICHA Taifa' hata baada ya kusimamishwa.Kiburi kikubwa.Walistahili 'kuletwa' CCM. Mwigamba yeye ameshaongea na waandishi wa habari jana na amemaliza yake ya moyoni.
Tatu,
Juliana Shonza na
Mtela Mwampamba walionesha kuwa kufukuzwa kwao ni baraka na nauli tosha kwenda CCM. Wakawahi Dodoma kupokelewa na kupiga picha na Mwenyekiti wetu wa chama-Rais Kikwete. Tena kulikuwa na Kamati Kuu yote pale Dodoma. Makini yeyote ataona haraka kuwa mchezo ulipangwa na kupangika.Hitimisho laweza kuwa vijana hawa walikuwa CHADEMA wakiiwakilisha CCM. Maybe.
Mkulima maskini yeye hajahama wala kufukuzwa chama bado.Na hawezi kufanya hivyo kirahisi.
Nne, vijana hawa wakati wanaingia kwenye sintofahamu na CHADEMA walikuwa bado hawana ajira. Lakini Mwigamba alikuwa na ajira yake. Ya uandishi wa habari. Vijana hawa walikuwa wakilelewa na CHADEMA kwa kila kitu. Ingwa wote hawa wana shahada za kwanza za Ualimu na Utawala, Mwigamba yuko katika nafasi nzuri.Yeye angalau alishakuwa Mwalimu na Mhasibu mahali kabla ya kuja CHADEMA. Vijana wote walikuwa bado.
Lakini, wote watatu sasa wanajutia maamuzi yao ya kukimbia vikao rasmi na kukimbilia mitandao. Amini nawaambia, vijana wawili:
Juliana Shonza na
Mtela Mwampamba hawana maisha ya uhuru na raha kama waliyokuwa nayo CHADEMA. Pale CHADEMA walikuwa wana usemi na nafasi. Hapa CCM hawana. Kuna vijana kama wao hapa waliwakuta na nafasi zao. Wageni hawa lazima wawe wapole. Kimsingi, wako 'limited' sana. Mwigamba bado anadunda ndani ya CHADEMA.Amesimamishwa tu.
Juliana Shonza na
Mtela Mwampamba ni vijana wazuri kichama lakini wanaendesheka kirahisi. Yawezekana ni kutokana na kuhitaji makubwa haraka. Lakini, bado wana muda wa kutosha kujirekebisha. Wanaweza kuaminika chama chochote cha siasa nchini na kuendeleza mapambano yao ya kisiasa. Kwanza wakubali kuwa wao wanaongozwa na Katiba na Kanuni za vyama vyao.Viongozi wao wapo tu kuwasimamia na kuzisimamia Katiba na Kanuni husika. Basi.
Kwenye siasa lolote linawezekana. Ipo siku, yaweza kuwepo kweli ndugu zangu,
Juliana Shonza na
Mtela Mwampamba wakarejea CHADEMA na Mwigamba akahama CHADEMA. Siasa hazitabiriki!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam