Mwigamba hatahama CHADEMA kirahisi!

Mwigamba hatahama CHADEMA kirahisi!

Mkuu uchambuzi wako siku zote una bebwa na dhamira ya kweli na uzalendo ndani yake:
Sema chama chako kinapenda sana kuchochea kuni mbichi kwa jirani wakati kwake kuna moto wa gesi na mda wowote unalipuka, Inshaallaaah tukutane hyo 2014/15
 
Unachokisema ni kizuri ils chenye "malice" nyuma yake, hakuna jinsi CHADEMA watadanganywa kumkumbatia mtu ambae tayari ccm wwnamtumia, mchango wake kwa chama unafahamika na utaheshimika, ila hiyo haimpi excuse ya makosa
 
Soma heading then ulichochangia ni vitu tofauti.
Pengine umechanganyikiwa ukiamka ukilala uchaguzi.
Huna mawazo mengine?
Nasema hivi kiongozi aliemaliza muda wa uongozi anahaki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza mashariti katika cheo kimoja hii iko kwenye ibara moja ya toleo la 2004 mwaka 2006 tulifanya renovation mwaka huo huo tulikubaliana kubadilisha baadhi ya vipengele mimi nilikuwa katibu wa wilaya na hiki kipengele hatukiozungumzia juzi wakati napitia katiba nikitaka kujua kwanini mbowe na zitto wanagombana nikaona hiki kipengelee hakipo, nikasema kwanini hatukuambiwa wajumbe wakati kinaondolewa...MBOWE, ARFI - bara, MOHAMEDI ISSA - zanzibar, DR SLAA, Naibu katibu mkuu MOHAMEDI YUSUF- zanzibar, ZITTO –Bar hawa mimi ndiyo nawapinga kuendelea kugombea.....
 
Hata kama cdm wakifanikiwa kum-contain mwigamba, kama hawata zingatia matumizi bora ya ruzuku hasa kupeleka pesa kwenye kanda basi wataibuka akina mwi-GAMBA wengi mara kwa mara. Cdm lazima ijue namna ya kupoza njaa za makamanda wake.
Nakubaliana na wewe, makao makuu wanapaswa kujua namna gani ya kupooza njaa ya wapiganaji wake, hili la mwigamba ni sehemu ya sauti za hao wanaolia kwa njaa, wa kwanza alikuwa Chacha wangwe wasaliti akina shonza wakabeba bango na sasa ni kamanda aliyenishawishi sana kuipigania Chadema Samson Mwigamba, ni wakati wa viongozi wa juu kukaa na kujua ni namna gani wale walioko chini wanaonja ladha ya keki ili wajihisi ni sehemu ya chama vinginevyo mapambano hayataisha
 
Mkuu kuna msemo "Ukiona adui anakusifia, Ujue kuna kasoro ana lake Jambo" Una lako Jambo Kunguru hafugiki atadokoa mboga kikaangoni. Kwa heri Mwigamba tafuta tawi Arusha likustiri, Mzee mshauri bure kuwa Arusha hatuna huruma na wasaliti
 
Mkuu Bramo, amenisihi kutoa maoni yangu juu ya utofauti uliopo kati ya Juliana Shonza, Mtela Mwampamba na Samson Mwigamba (wakiwa CHADEMA). Najaribu tu kusikika hapa:

Juliana Shonza na Mtela Mwampamba(vijana) sasa ni makada wenzetu wa CCM. Mwigamba bado yu CHADEMA. Makada hawa wanaweza kutofautishwa hata wakiwa CHADEMA.

Kwanza, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba walikuwa BAVICHA wakati Mwigamba alikuwa Mwenyekiti wa mkoa Arusha. Hapa pana jambo zito. BAVICHA ni kiwanda cha CHADEMA kutengeneza makamanda imara wa chama na viongozi wanaofuata. Hivyobasi, BAVICHA ni sehemu adimu na adhimu. Si sehemu ya mchezo.

Vijana husika walikuwa humo.Tena mmoja alikuwa Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa (Shonza). Mwigamba yeye ameshaiva na kuivika.Katika hali ya kawaida,hata katika familia zetu,onyo kali mno hupewa kijana mdogo kuliko mtu mzima hata kwa kosa moja. Hii ni kwasababu, kijana bado ana muda mrefu wa kujifunza na kujirekebisha. Akirudia tena,adhabu kali hufuata. Ndivyo ilivyokuwa.

Pili, Juliana Shonza Mtela Mwampamba na Mwigamba wote walikiuka Katiba na Kanuni za chama. Na wote walisimamishwa. Lakini vijana waliendeleza kiburi. Walidai mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuwa wao bado wako BAVICHA na 'hakuna' wa kuwatisha. Shonza alikuwa akisema "Mimi bado Makamu Mwenyekiti BAVICHA Taifa' hata baada ya kusimamishwa.Kiburi kikubwa.Walistahili 'kuletwa' CCM. Mwigamba yeye ameshaongea na waandishi wa habari jana na amemaliza yake ya moyoni.

Tatu, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba walionesha kuwa kufukuzwa kwao ni baraka na nauli tosha kwenda CCM. Wakawahi Dodoma kupokelewa na kupiga picha na Mwenyekiti wetu wa chama-Rais Kikwete. Tena kulikuwa na Kamati Kuu yote pale Dodoma. Makini yeyote ataona haraka kuwa mchezo ulipangwa na kupangika.Hitimisho laweza kuwa vijana hawa walikuwa CHADEMA wakiiwakilisha CCM. Maybe. Mkulima maskini yeye hajahama wala kufukuzwa chama bado.Na hawezi kufanya hivyo kirahisi.

Nne, vijana hawa wakati wanaingia kwenye sintofahamu na CHADEMA walikuwa bado hawana ajira. Lakini Mwigamba alikuwa na ajira yake. Ya uandishi wa habari. Vijana hawa walikuwa wakilelewa na CHADEMA kwa kila kitu. Ingwa wote hawa wana shahada za kwanza za Ualimu na Utawala, Mwigamba yuko katika nafasi nzuri.Yeye angalau alishakuwa Mwalimu na Mhasibu mahali kabla ya kuja CHADEMA. Vijana wote walikuwa bado.

Lakini, wote watatu sasa wanajutia maamuzi yao ya kukimbia vikao rasmi na kukimbilia mitandao. Amini nawaambia, vijana wawili: Juliana Shonza na Mtela Mwampamba hawana maisha ya uhuru na raha kama waliyokuwa nayo CHADEMA. Pale CHADEMA walikuwa wana usemi na nafasi. Hapa CCM hawana. Kuna vijana kama wao hapa waliwakuta na nafasi zao. Wageni hawa lazima wawe wapole. Kimsingi, wako 'limited' sana. Mwigamba bado anadunda ndani ya CHADEMA.Amesimamishwa tu.
Juliana Shonza na Mtela Mwampamba ni vijana wazuri kichama lakini wanaendesheka kirahisi. Yawezekana ni kutokana na kuhitaji makubwa haraka. Lakini, bado wana muda wa kutosha kujirekebisha. Wanaweza kuaminika chama chochote cha siasa nchini na kuendeleza mapambano yao ya kisiasa. Kwanza wakubali kuwa wao wanaongozwa na Katiba na Kanuni za vyama vyao.Viongozi wao wapo tu kuwasimamia na kuzisimamia Katiba na Kanuni husika. Basi.

Kwenye siasa lolote linawezekana. Ipo siku, yaweza kuwepo kweli ndugu zangu, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba wakarejea CHADEMA na Mwigamba akahama CHADEMA. Siasa hazitabiriki!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Mkuu VUTA-NKUVUTE

Nashukuru kwa Maoni yako.
Lakini inasadika kuwa baada ya wataalam wa IT kuikagua Computer ya Mwigamba,inasadika wamekuyata mengi sana.
Ingawa bado hawajaweka wazi ni nini wamekikuta, lakini taarifa za kuaminika yamekutwa mawasiliano (email) yake ya Karibu na Mahasimu wa CHADEMA
Kumbuka kuwa, watu ambao sio weledi wa masuala ya IT mara nyingi kwenye Computer zao, hui ruhusu Browser kukumbuka Nywila (Passwors) zao.
Kwa hiyo mtu anapokuja kuikagua Computer yako anaweza akaenda staright kwenye emails zako na kuona conversation zako zote.
Inasemekana kuwa amakuwa akivujisha mipango mingi sana ya Chama kwa Mahasimu wa CHADEMA, yote yameonekana kwenye mawasiliano yake.
Kumbuka kuwa CHADEMA kina Nguvu kubwa sana Kaskazini, Kumbuka kuwa watu wengi sana wamekufa wakikipigania Chama Kaskazini.
Reffer Marehemu Mbwambo aliyechinjwa USA River, Mbunge Lema ambaye kutwa kuchwa anawindwa na kufunguliwa kesi zisizo na Kichwa wal Miguu.
Hii ndio Sababu iliyopelekea watu kufikia hatua ya Kumpiga Mwigamba.
Based on this, Huoni kuwa Chance ya CHADEMA kum retain Mwigamba ni ndogo sana.
Haya ni Maoni yangu lakini
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: mmh
Ninachojua mwigamba aliachiwa kesi peke yake hadi leo anateseka nayo.

wewe ni mnafiki mpuuz usiyefaa katika jamii yoyote iliyostaarabika.wakati kesi za kijinga wanabambikiwa mwigamba na watanzania wengine maccm ukiwemo na wewe huwa mnafurahia na kushangilia lakn cha ajabu eti leo unamhurumia mwigamba.kweli?
 
Nasema hivi kiongozi aliemaliza muda wa uongozi anahaki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza mashariti katika cheo kimoja hii iko kwenye ibara moja ya toleo la 2004 mwaka 2006 tulifanya renovation mwaka huo huo tulikubaliana kubadilisha baadhi ya vipengele mimi nilikuwa katibu wa wilaya na hiki kipengele hatukiozungumzia juzi wakati napitia katiba nikitaka kujua kwanini mbowe na zitto wanagombana nikaona hiki kipengelee hakipo, nikasema kwanini hatukuambiwa wajumbe wakati kinaondolewa...MBOWE, ARFI - bara, MOHAMEDI ISSA - zanzibar, DR SLAA, Naibu katibu mkuu MOHAMEDI YUSUF- zanzibar, ZITTO –Bar hawa mimi ndiyo nawapinga kuendelea kugombea.....

Mkuu Ritz unaonaje,

Hizi cheche alizorusha Masikini Mkulima zimeweza kuwasha moto ndani ya Chadema ama zimemuunguza mwenyewe Masikini Mkulima? Ama unaonaje?
 
Sababu zipo nyingi.lakini hizi ni chache:

Kwanza,Samson Mwigamba amejijengea jina akiwa CHADEMA. Hata makala zake za 'Kalamu ya Mwigamba' za kwenye Tanzania Daima zinauzika kwakuwa tu yupo CHADEMA na akiwa kiongozi huko. Huo ndio ukweli. Mwigamba wa mwaka 2003 si huyu wa 2013. Kutoka Mwalimu hadi Mwenyekiti wa chama Arusha. Sasa, ni wakati wake kulipa fadhila na kukitumikia chama chake. Aachwe aamue kubaki CHADEMA.

Pili, CHADEMA inampigania. Mara baada ya Mwigamba kukamatwa na kushtakiwa kwa kosa la uchochezi(akiwa pamoja na Absalom Kibanda), CHADEMA ilimwaga Mawakili Wasomi kumlinda kisheria Mwigamba. Tangu siku ya kwanza ya kesi hadi sasa, Mwigamba analindwa,anasaidiwa, anatetewa na kupiganiwa. Naye anaonesha uzalendo kwa chama kiutumishi na kiutawala.Ya Arusha na mitandaoni yanajadilika na kusameheka. Mwigamba hawezi kuhama CHADEMA kirahisi.

Tatu, CHADEMA kimeimarika na kutambulika kama chama kikuu cha upinzani nchini. Ni mpinzani wa kweli wa CCM yetu iliyo madarakani tangu 1977 ilipoanzishwa ikirithi utawala wa TANU ulioanza 1961. CHADEMA kwasasa si chama cha kubeza. Kinasumbua vichwa vya makada na viongozi wa CCM.Si kitu kidogo kuwa ndani ya CHADEMA,tena katika ngazi ya Mwigamba. Mchezaji mzuri hasusi mechi kirahisi.Hununa na kucheka baadaye kidogo. Mwigamba yuko tayari kuingia na kucheza mechi ya 2014 na 2015 akivaa jezi ya CHADEMA. Si rahisi kususa!

Nne, mambo ya Arusha yamekuzwa mno. Hayakutokea kama yarivyoripotiwa. Kwakuwa Mwigamba naye ni mwandishi wa habari, atakuwa ameshang'amua. Amejua jinsi anavyochochewa kuasi na kuhama CHADEMA. Kimsingi, Mwigamba ni mtu makini. Hawezi kuyumbisha chama lakini pia hatathubutu.

Tano, Mwigamba anaijua Katiba na Kanuni za CHADEMA. Atachukua hatua stahiki kikanuni pale ambapo atahitaji kukosoa kwa ajili ya maboresho. Hatarudia kujiita na kufanya alivyofanya. Alitereza. Alikosea. Anajua fika kuwa kwasasa yeye anaihitaji CHADEMA na CHADEMA inamhitaji. Ataiboresha kikanuni. Hawezi kutumika kirahisi kama inavyoripotiwa.

Sita, makada wa vyama vingine tuache kufuatilia na kuchochea yasiyotuhusu. Kwa CHADEMA ya sasa, hategemewi mtu.Hakuna hata mmoja aliye maarufu kuliko chama. Ushushushu na umafia toka nje sasa unakumbana haraka na 'a great wall'. Huu ni ukweli mchungu kuusema.

Hatahivyo, CCM yetu iko imara sana. Haihitaji kuchonganisha na kuvuna wanachama wa CHADEMA. Inajipanga na kujiimarisha zaidi kila kukicha kwa mpambano wa fainali hapo 2014 na 2015. Wachezaji wetu wana morali ya hali ya juu. Wako tayari kupata ushindi. Sasahivi, tumetingwa na kutekeleza Ilani yetu ya 2010-2015. Tukutane uwanjani 2014 na 2015. Kila la kheri wapinzani wetu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Saaam.

Umetumwa umsemee? Mbona kuna uzi hapo juu,unaosema kuhusu ukweli wa katiba yenu na ukweli wa namna kipengele kilivyochakachuliwa, changia hiyo thread kwanza! Sio kumbembeleza Mwigamba!
 
Mkuu 2Pa 2pa Heshima kwako,huwa napenda maandiko yako makini.
 
Mkuu 2Pa 2pa Heshima kwako,huwa napenda maandiko yako makini.

Mwigamba kajimaliza kama Shonza, na atatapatapa sana same kama Shonza, na tutamsahau kama Shonza na Mwampambwa wake
 
hamna kitu Chadema nao wezi tuu,jamaa ni mzalendo hasa lakini godbless lema si mzalendo mwizi
 
Movement for Crazy people wanachama wengi wa CDM hawana uono wa mbali chadema na CCM tofauti ni Mavazi tu l;akini wote ni walewale
\
 
Back
Top Bottom