Mwezi mkubwa zaidi kuonekana duniani

amygdala

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
1,082
997
_92426725_supermoon.jpg

Mwezi mkubwa zaidi kuonekana

Watazamaji wa anga wanajiandaa kuuona mwezi mkubwa zaidi wakati ambapo utakaribia dunia tangu 1948.

Uingereza itakuwa na fursa nzuri kuuona mwezi huo siku ya Jumatatu jioni,licha ya kuwa utakaribia dunia mwendo wa saa tano na dakika 21 muda wa GMT ambapo utakuwa umbali wa kilomita 356,509.

Wachunguzi watauona mwezi huo kuwa mkubwa zaidi kwa asilimia 7 ukilinganishwa na mwezi wa kawaida na kung'aa zaidi ya asilimia 15, licha ya kwamba macho ya binaadamu yanaweza kupambanua tofauti hiyo.

Huku mwezi huo ukitarajiwa kutokaribia dunia hadi tarehe 25 mwezi Novemva 2034, idara ya maswala ya hewa nchini Uingereza imesema kuwa kutakuwa na mawingu mazito wakati mwezi huo utakapokaribia.

Huku mwezi ukizunguka dunia,kuna tofauti ya mwangaza unaotolewa na jua.Ni wakati huo ambapo mwezi wote humulikwa na mwangaza huo na kutoa mwezi mkubwa zaidi.

Chanzo: BBC Swahili
 
Sijui kwa Tanzania utapitia pande zipi? Tumwombe mwenye universe yake apishe mbali haya mabalaa maana sio mazuri kabisa. Jua limepatwa juzi hapa mara likafuata tetemeko; hili la Mwezi kuning'inia karibu zaidi na dunia linaweza kuleta maafa kuliko neema au ugunduzi wa kisayansi. No wonder mwaka huu unaelekea kuwa wa ukame mkali.
 
Back
Top Bottom