Atabase Agaya
Senior Member
- Dec 7, 2011
- 120
- 41
Enzi hizo (1982) ndio nilikuwa najifunza kufukuzia visichana kijijini, halafu unatembea kilomita 5 kwenda kijiji cha jirani kufuata walimbwende na tochi yenye mwanga hafifu ukipita katika msitu mnene.............LOL
Atabase Agaya leo hapa nyumbani leo kumezuka KIMBWAIMBWAI, Mama Ngina kacharuka..................
sobhuza Enzi hizo kulikuwa na:
Maalimu Muhidin Gurumo
Shaaban Dede
Hassan rahani Bitchuka
Michael King Enoch (Marehemu)
Cosmas Chidumule
Abel Baltazari (Marehemu)
Senksi mkuu, mimi ni kizazi cha dot.com, unaweza kunipa line-up ya Sikinde wakati huo?
Yaani nimekuja kasi kujua kulikoni kumbe wimbo. Haya huwe unajikaribisha kwenye blog yetu ya Mallechela utakuta hizo nyimbo na za kina Kasongo kyanga na Lesi wa nyika
Huyu mzee naye,kwan ungekubali tu kuwa nilikua chekechea si ingekuwa poa tu!!SALOK enzi hizo Cantalisia alikuwa hajazaliwa bado...
..kuna kigodoro..eeh?@CantalisiaPole baba,njoo huku leo tunakesha!!!
Vocals: Maalim Gurumo, Bichuka Hassan, Khamisi Juma, Cosmas Chidumule
Solo: Abel Baltazar, Joseph Mulenga
Rythim: Abdallah Gama
Bass: Mwanyiro Suleimani
Organ: George Kessy
Sax: Ninja King Enoch, Lendi
TaiJike Wimbo huu bila shaka atakuwa ameimba Juma Nature...........................LOLUzuri wangu wa tausi mama malingo kwetu kawaida,
wenzangu wananisengenya nikipita mara hukonyezana ooo,
wamesahau kazi zao kutwa nzima kunichunguza,
malingo kwetu kawaida hamuwezi kunyamaza ooo.
wasi wasi wako wa nini wacha niseme ukweli,
mwili wangu mzuri kila vazi linakubali,
uzuri wangu wa kuzaliwa malingo kwetu kawaida,
nikigeuka utakubali, nikicheka utakubali nikicheza utazimia wazi wazi... Nimeshindwa kuendeleza, nimesahau.
Mtambuzi huu wimbo uliimbwa na kina nani?