Mwenzenu nimetekwa nyara na shangingi

aise

JF-Expert Member
May 16, 2018
4,107
11,822
Yalinifika ya mwaka, kule mbali kiungani, gari liliharibika, nikitokea kazini,
usiku ulipofika, nikapata mhisani, kumbe ninatekwa nyara, na shangingi mswahili..
Kwake nikapumzika, kajua na msalani, kinywaji niliposhika, kumbe kina kungu ndani,
pindi nikazuzulika, nikajilaza kitini, kumbe nimetekwa nyara, na shangingi mswahili..
Chakula alichopika, kikawa ni biriani, nyute zikanidondoka, kingali huko jikoni,
mezani akikiweka, hana nguo maungoni, kumbe nimetekwa nyara, na shangingi mswahili..
Chakula hakikulika, nikauliza kunani akasema anitaka, hajui ninangojani,
Huku akichekacheka, kanisukuma kochini, kumbe ninatekwa nyara, na shangingi mswahili..
Ndipo aliponishika, na kunibusu shavuni, akanipiga mweleka, na kuniangusha chini,
nikawa nababaika, nalazimishwa kuzini, kumbe nimetekwa nyara, na shangingi mswahili..
 
Akili akaniteka, kanifanya hayawani, japo nilishawishika, sikuipata makini,
majuto yalinifika, na wasiwasi moyoni, kumbe nimetekwa nyara, na shangingi mswahili..
Ukimwi ukinishika, atakuwa lawamani, atajibu mashtaka, kunitia taabani,
kwa kweli alinibaka, elewa wangu mwandani, kwamba nilitekwa nyara, na shangingi mswahili..
Usinione kuchoka, sinazo nguvu mwilini, nililala na wahaka, nililala ugenini,
nilipata hekaheka, lisilo kamwe kanuni, kumbe nimetekwa nyara, na shangingi mswahili..
Najua umeshtuka, na wala huniamini, lakini yakimwagika, ayazoaye ni nani ?
japo unipe talaka, ukweli nimebaini, kwamba nilitekwa nyara, na shangingi mswahili..
Nilifanya kutoroka, kupitia dirishani, akashindwa kunishika, niliporuka uwani,
ndio sasa nimefika, nimerejea nyumbani, jana nilitekwa nyara, na shangingi mswahili…
 
Ile chai uliyotupikia na kutunywesha ya safari ya Kigoma ilikubeba sana, kila nnapoona nyuzi zako naona chai tena ya moto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yalinifika ya mwaka, kule mbali kiungani, gari liliharibika, nikitokea kazini,
usiku ulipofika, nikapata mhisani, kumbe ninatekwa nyara, na shangingi mswahili..
Kwake nikapumzika, kajua na msalani, kinywaji niliposhika, kumbe kina kungu ndani,
pindi nikazuzulika, nikajilaza kitini, kumbe nimetekwa nyara, na shangingi mswahili..
Chakula alichopika, kikawa ni biriani, nyute zikanidondoka, kingali huko jikoni,
mezani akikiweka, hana nguo maungoni, kumbe nimetekwa nyara, na shangingi mswahili..
Chakula hakikulika, nikauliza kunani akasema anitaka, hajui ninangojani,
Huku akichekacheka, kanisukuma kochini, kumbe ninatekwa nyara, na shangingi mswahili..
Ndipo aliponishika, na kunibusu shavuni, akanipiga mweleka, na kuniangusha chini,
nikawa nababaika, nalazimishwa kuzini, kumbe nimetekwa nyara, na shangingi mswahili..
Ungeza Stanza naona Kama limeishia Njiani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akili akaniteka, kanifanya hayawani, japo nilishawishika, sikuipata makini,
majuto yalinifika, na wasiwasi moyoni, kumbe nimetekwa nyara, na shangingi mswahili..
Ukimwi ukinishika, atakuwa lawamani, atajibu mashtaka, kunitia taabani,
kwa kweli alinibaka, elewa wangu mwandani, kwamba nilitekwa nyara, na shangingi mswahili..
Usinione kuchoka, sinazo nguvu mwilini, nililala na wahaka, nililala ugenini,
nilipata hekaheka, lisilo kamwe kanuni, kumbe nimetekwa nyara, na shangingi mswahili..
Najua umeshtuka, na wala huniamini, lakini yakimwagika, ayazoaye ni nani ?
japo unipe talaka, ukweli nimebaini, kwamba nilitekwa nyara, na shangingi mswahili..
Nilifanya kutoroka, kupitia dirishani, akashindwa kunishika, niliporuka uwani,
ndio sasa nimefika, nimerejea nyumbani, jana nilitekwa nyara, na shangingi mswahili…
Lovely
 
Bora ukarudisha tu zile pesa za watu ulizochangiwa wakati ule uliposingizia uko njiani kutokea Kigoma.
 
Yalinifika ya mwaka, kule mbali kiungani, gari liliharibika, nikitokea kazini,
usiku ulipofika, nikapata mhisani, kumbe ninatekwa nyara, na shangingi mswahili..
Kwake nikapumzika, kajua na msalani, kinywaji niliposhika, kumbe kina kungu ndani,
pindi nikazuzulika, nikajilaza kitini, kumbe nimetekwa nyara, na shangingi mswahili..
Chakula alichopika, kikawa ni biriani, nyute zikanidondoka, kingali huko jikoni,
mezani akikiweka, hana nguo maungoni, kumbe nimetekwa nyara, na shangingi mswahili..
Chakula hakikulika, nikauliza kunani akasema anitaka, hajui ninangojani,
Huku akichekacheka, kanisukuma kochini, kumbe ninatekwa nyara, na shangingi mswahili..
Ndipo aliponishika, na kunibusu shavuni, akanipiga mweleka, na kuniangusha chini,
nikawa nababaika, nalazimishwa kuzini, kumbe nimetekwa nyara, na shangingi mswahili..
Wakuja tu uswahilini lakini si mswahili, waswahili hatuna mila hizo za kishenzi, tukipenda twapumbaza, kwa wenye uhalali. Usituone wapumbavu chuo tumepewa ukibisha muulize Isaya wa ishirini na tisa kumi na mbili. Ni nani mwenye chuo?

Huyo wakuja, uswahili kajipachika, uswahili kiukweli ni desturi nzuri nzuri. Waswahili hatuteki twakutia kibindoni. Uidhinishwe kihali kimasomaso mwandani, twakuweka mgongoni na khanga twakutanda twakupeleka bafuni kwa mbeleko na kisosi.

Mfate MO akujuze watekaji kina nani. Waswahili abadan.
 
Hua namuhurumia sana huyu kijana, basi kwasababu aliomba msaada akasaidiwa basi anatakiwa aishi maisha ya kinyonge kuliko unyonge wenyewe.... na hii ndio tafsiri nzima ya Muafrica, chuki, roho mbaya, unyonyaji, unyongeshaji, utwana, n.k.

Go Aisee Goooooo, shairi zuri ila ungejaribu kuacha nafasi baina ya beti na beti.
 
Bahati mbaya ruge ametutoka,na hakuna wa kuvaa viatu vyake angeshaona kipaji ungeshatoboa
 
Back
Top Bottom