Mwenzenu niko kalenge dhahabu imefumuka

OMEGA

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
693
300
Wakuu,kwa wale wenye interest ya mambo ya madini njooni kalenge,sio mbali sana ni njia ya kwanda Kibondo KM kama 25 toka njia panda ya Nyakanazi,mimi nipo hapo tangu juzi,zimefumuka dhahabu haijawahi kutokea,wasukuma wanasema kuyila.Ninavyoongea kila baada ya dakika mbili inafika misafara ya magari yenye maelfu ya watu toka sehemu mbalimbali kujaribu bahati zao,mimi nimekuja juzi lakini angalau hata nikiondoka kesho niko safi.Nachoofia ni out break ya magonjwa kama kipindupidu etc kwani watu wamefurika utadhani Loliondo enzi hizo.Pia RPC Kigoma sijui kama anazo taarifa kwani ni hatari tupu,watu wapo na mamilions kwa ajili ya kununua dhahabu papo kwa papo,Burundi ipo jirani na nimeona raia wa nchi izo wengi tu.Mwenye interest na dhahabu karibu Kalenge,uliza mjaluo utanipata.
 
Dhahabu yenyewe ni ya vikole au kwenye mwamba? Nataka kuja na metal detector fasta!
 
gramu moja ni bei gani bwana:
ni nyunga sana! au ni mabonge tu??? kuna haja ya kubeba krona na mercury au?????
 
Tz is full of riches!
Unajua ata pale bwawa la mindu kuna dhahabu watu walikunywa kwa gear ya kutengeneza bwawa!
Ndo maana kuna kipindi watu walikuwa wanachimba wajeda wakawapiga stop!
 
Hiyo sehemu ya kalenge hadi vijiji vya mubanga ishapewa muwekezaji kwa ajili ya kilomo cha mawese. mda si mrefu mtafukuzwa. ndo maana hiyo barabara kuanzia njia panda ya nyakanazi kwenda kibondo inatengenezwa kwa kiwango cha lami ili kuwalahisishia usafiri. kama vipi kaeni kwa machale coz hawa polisi hawakawii kuja kuwamiminia risasi.
 
Du! ila wakuu hayo maeneo nimewahi kupita, mkuu hebu tupe hali ya kiusalama huko. chakushangaza ni mahali ambapo Mabasi lazima yawe na escott ya police wenye magazine mbili mbili full of bullets. Kwa mtazamo wangu nilihisi maeneo ya hapo nyakanazi usalama si wakujiaminisha sana. Sijui mtoa mada hilo suala hususani watu kuja na maburungutu ya fedha maeneo ambayo ujambazi ni tishio wewe unalionaje.

Hebu nipe updated kwa miaka ya hivi karibuni. Maana ni mahali pekee ambapi tanzania hii niliwahi kuona defender ya polisi ikiwa inabunduki yenye mkanda mrefu wa risasi kwa ajili ya kusaka majambazi.
 
Wakuu,kwa wale wenye interest ya mambo ya madini njooni kalenge,sio mbali sana ni njia ya kwanda Kibondo KM kama 25 toka njia panda ya Nyakanazi,mimi nipo hapo tangu juzi,zimefumuka dhahabu haijawahi kutokea,wasukuma wanasema kuyila.Ninavyoongea kila baada ya dakika mbili inafika misafara ya magari yenye maelfu ya watu toka sehemu mbalimbali kujaribu bahati zao,mimi nimekuja juzi lakini angalau hata nikiondoka kesho niko safi.Nachoofia ni out break ya magonjwa kama kipindupidu etc kwani watu wamefurika utadhani Loliondo enzi hizo.Pia RPC Kigoma sijui kama anazo taarifa kwani ni hatari tupu,watu wapo na mamilions kwa ajili ya kununua dhahabu papo kwa papo,Burundi ipo jirani na nimeona raia wa nchi izo wengi tu.Mwenye interest na dhahabu karibu Kalenge,uliza mjaluo utanipata.
kuna ulinzi wa kutosha?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom