Kwani kukaa mikoa tofauti ndio ticket ya kutanga tanga nje ya mahusiano yako na mtu anaekuamini??haaah haah Lizzy bibie imagine dada amesema wanaishi mikoa tofauti so ktk mazingira kama hayo kweli?!
Then kama amekiri why asisamehewe?!
Dada atulie kwanza ampime kama ataelekea asemehe tu huo ndio uhalisia.
Nielewe kwamba sitetei cheating ila nataka dada afanye maamuz sahihi na aangalie mazingira ya kosa na kukiri kwa muhusika. asikurupuke tu
Anahishi Dar, na huyo dada anahishi Dar. Huyo dada hakujui (hajaambiwa kuhusu wewe) na 'mchumba wako' anampenda kiasi kwamba alishindwa kabisa kumwambia asimpigii coz anamkera yeye akiwa na wewe. Milivo amka yeye akarudi dar... Unadhani inakuwaje kule? How do you know hayoko katika harakati za kuomba na yule amsamee? maana kule kasema kuhusu wewe na huku kasema kuhusu yeye, now he is trying to solve huku, maybe he is also trying kule?nipo kwenye uhusiano kwa mwaka wa nne sasa na mchumba wangu.
Mungu kanijalia kazi nzuri tu ambapo napata mahitaji yangu yote bila ya msaada wa mtu yeyote.
Nipo naye mbali (tunafanya kazi mikoa tofauti yeye yupo Dar).
Alikuja kunitembelea, simu yake ikaanza kuita imeita kwa mara ya kwanza Akapokea, akaanza kuongea na huyo mtu (ni dada).
Muda si mrefu (baada ya dakika kama moja) yule dada akapiga tena akamwambia kwanin anamkatia simu?
Alipomaliza nikamuuliza ulikuwa unaongea na nani? Mchumba akanidanganya ya kuwa ni mfanyakazi mwenzie wa kazini,[but] ile idara anayofanyia kazi ni wanaume watupu (ni engineer wa kampuni Fulani Dar).
Mara ya tatu akapiga huyu dada wakaongea tena Mchumba akamkatia tena simu
Haijapita hata dakika dada huyu akapiga, Nikamrudishia simu na akazima kabisa na mchumba hakuwa na amani hata kidogo.
Hapo ndio nikaanza kumhoji huyo ni nani yake akajibu ni rafiki wa dada yake anayeitwa Tuma (hapa nalidanganywa sababu ni tofauti na aliponijibu mwanzoni), nikamuuliza huyu dada umekuwa kwenye mahusiano naye tokea lini akajibu tokea katikati ya mwaka huu.
sina amani nae tena, wala raha nae kama zamani.
Asubuhi yake alipanda basi la kurudi huko Dar.
Kwani kukaa mikoa tofauti ndio ticket ya kutanga tanga nje ya mahusiano yako na mtu anaekuamini??
Kama anajua hawezi kuvumilia si abaki single ili popote anapoenda awe huru kuchukua mtu bila kumuumiza mwingine?Embu watu mjifunze self discpline bana acheni kutafuta visingizio hata visivyo na vichwa...miguu wala mikono.
Heheheh....eti amekiri!!Amekiri au amebambwa???
Nyw,...hata kama angekua amekiri ndo afanye mazoea??Yani kila siku acheat na kukiri??Lini ataacha?Akishamletea mwenzie magonjwa ehhhh!!!?
Ingekua ndio mara ya kwanza nisingeshangaa sana huo utetezi wa ki'mazingira' ila kwa mara zaidi ya ya pili.....mmmh LABDA!!!
NK huwezi kujua, huyu awe mpole tu. Tatizo wanawake mnakimbilia kuachana na wapenz then later inakula kwenu au anapata mpenzi cheater zaidi.
May b jamaa amecheat kutokana na mzingira tu so kama amekiri tena kwa kulia machozi ni wazi hamtaki huyo mpenz wa nje.
So huyu atulie kwa muda apime then atoe uamuzi sahihi na sio kukurupuka tu.
haaah haaah Lizy bana! Ujue hapa uamuzi anao mdada mwenyewe atulie apime na wala sijamaanisha kuishi mikoa tofauti ndio iwe ticket ya kucheat.
Ninachopenda tu huyu afanye maamuzi sahihi asije kujikuta anaruka jivu anakanyaga moto.
Always maamuzi akiwa na hasira hayakuwa sahihi.
Halafu hajasema kosa la kwanza imekuaje je alimkamata vipi mana wadada wengine hata mkiona sms tu ya msichana tayari mnakua na mawazo mnasalitiwa.
Lol. Kama kulia watu tushaliliwa saana; wanaume wengine kulia ni hobby. Unakuta analia kwa wote wawili chezea. Hizo treak ni za kuwadanganya teenagers. Ulie, usilie umechiti; ungejua kuna kilio usingechiti at first place.
I wish ningerudi ujana wangu. Nimemiss adventures. Msichana kuringa bwana. Tuache tulo kwenye ndoa tujiulize mara mbili ila nyie mso na mkataba wala watoto what is that that is making you stick with a person that makes you cry.
Atakuwa anakuchiti analia unamsamehe; miaka inasonga kukuoa hakuoi; ukijashtuka 35 unaanzisha thread ya kuomba ushauri wachumba wamegoma. Kiwingu hicho dada; kiwingu; hakuna atakayekutokea ukiwa kwenye relationship; hata wewe huwezi ona wengine. Zinduka.
Hata akikuoa nina mashaka ndo hao wanaosema (hata humu JF) ooh kuchiti lazima kwani hata wakati naoa nilikuwa na wasichana watatu kwa hiyo siwezi kuwaacha ghafla. Kuna mtu aliandika hivi kwenye thread ya cheating; I felt sick.
Mbona unamtetea sana? Hujasoma hapo anasema sio mara ya kwanza? amesha samehewa na akarudi tena.NK kweli nafahamu kuna uwezekano huyu akawa anabembeleza kote kote.
Najua unaongea kwa hisia zaidi coz umeolewa na una miliki mume.
Nayakubali pia mawazo yako.
Ila hapa tuangalie ile ki uhalisia tu je huyu mchumba wa dada hawezi kubadilika?tukumbuke hakuna binadamu mkamilifu 100% .
Maana naangalia pande zote dada mwenyewe maelezo yake ameonyesha anampenda jamaa. Ndio maana inabidi atulie halafu apime ndio afanye maamuzi.
Mi kinachonichosha ni hivyo visingizio....mara mazingira..mara kakiri...sijui kalia na mengine kama hayo.
The guy is a cheater....a serial one even ...iwe kwasababu au bila sababu.Hata ukipaka rangi gani giza litabaki kua giza tu. Mkubalie kwamba kweli mpenzi wake kakosea (bila visingizio) abaki nae au songe mbele akijua hilo. Sio unajaribu kumpa utakatifu mkosaji na kumtetea wakati kila kitu kiko wazi.
Mbona unamtetea sana? Hujasoma hapo anasema sio mara ya kwanza? amesha samehewa na akarudi tena.
Mbona unamtetea sana? Hujasoma hapo anasema sio mara ya kwanza? amesha samehewa na akarudi tena.
simtetei Lizy mimi najaribu tu kumuonyesha huyu kwamba haya matatizo anaweza kukutana nayo popote pale tena kwa mtu tofauti na huyu wa sasa. Na anaweza akakutana nayo makubwa zaidi ya haya.
Hapa anachopaswa ni kutulia kwanza mzuka wa hasira uishe halafu aamue kwa usahii akipima na akaona hamfai ampige chini na endapo ataona men anarekebishika anaweza kuendelea nae ni poa tu.
ila Men tumeona ana makosa ila hawa wamekaa miaka minne uhusiano wao so full data anazo mdada mwenyewe.
pole sana mpz mana maumivu makali mnooo umepata jaribu kusali kwanza na kutuliza moyo wako kidogo ili usiendelee kuumia ok
then kama alishaucheat hapo mwanzo na ukamsamehe mara nyingi duh! hii si nzuri sana mana yaonesha yy si mwaminifu sana kwako....... asije kukuletea magonjwa kwa house sasa mana dunia imebadilika sana sio kama zamani enzi zetu cc,
pili ww wasema huna amani kukaa naye ila hujasema ka humpendi .............hapa pana utata kidogo mana unaweza kupewa ushauri na usikusaidie mana bado uko inlove mbaya mnoooo na msela
tatu labda upewe ushaur wa ww vp utairudishaje iyo amani yako ili musonge mbele na malavidav yenu mana inaonesha bado mapenz na msela yako
Tena huyu mchumba I can tell kwa uzoefu wangu ni hatari sana. Angekuwa kweli huyu mdada ana status ya "mchumba" kwake (maana nahisi anatumia uchumba kama ticket ya sex) basi the second girl asingethubutu kupiga simu continuously. Basi angeweka wazi kwa the other girl kuwa kuna mwenye mali wewe ni mwizi. Ingawa hiyo haimfutii dhambi ya kuchiti. Nachotaka kusema ni kuwa kuna uwezekano mkubwa sana kuwa the second girl ndiyo chaguo la jamaa maana ameshindwa kumpa masharti; Nasema hivyo nikitumia theory ya last love is the number one love; au anawachezea wote wawili hakuna cha mchumba yeyote kati yao.
Nimeshaona watu wanaochiti wakiwa na wachumba lakini not this way; huwa wana make sure the other girl know that yeye ni mpango wa kando. Sasa huyu jamaa kwa nini amekuwa na kigugumizi mpaka amepigiwa simu akiwa na mamsapu.
Yeahhh...ngoja siku akija hapa kulia mpenzi wake aliemcheat sana akamsamehe amemwambukiza ngoma labda ndo utaona umuhimu wa kukimbia matatizo ikiwa hayatatuliki.
Alafu huyo dada mwingine nae alijitambulisha kama ''mchumba'' according to mtoa mada.
Inawezekana kabisa kwamba yeye ndie mwizi wa penzi japo hajui na mwenzake ndie mmiliki..au yeye ndio anaeibiwa au wote wameingizwa mjini na tapeli wa mapenzi. Hamna namna ya kujua nani ni nani....
Hapo kuna dimention ingine sasa, mwenyewe unasema atakua kaolewa na kuolewa sio jambo la mzaha. The good thing is unaolewa na mtu unae muamini. Kama atakuja kukukosea huko mbele ni tofauti na shahuri zitakua tofauti (ingawa mimi nitamshauri zaidi upande wa kuachana maana swala la ukimwi uko pale pale...)Lizy basi tumshauri amuache bila kupima chochote, then siku akija akisema kaolewa ila mumewe ana nyumba ndogo sijui utamshauri vipi.
Nani kakudanganya? Hapa ndipo unapo kosea. Mbona dada hakucheat? Yeye hakai mbali? Jamani acheni kuuendekeza upuuzi na kuusupport namna hii...Maana kwa maelezo tu amesema wapo mikoa tofauti sasa ile kukaa mbali mbali tu ndio imepelea yote haya.
Hajakurupuka. Kwani ndio kamuacha sasa? kaleta swali hapa: nimwache au nimsamehe? sasa kila mtu anatoa ushahuri alafu ataamua mwenyewe. Kumbuka ana wiki kwa kutoa maamuzi yake kwa 'mchumba' so kula utakacho mwambia tayari kipo katika mpango wa kufikiriwa na hakuna point ya kumshahuri kufikiria tena coz ndio mafikiri yenyewe hapa.Tuache hisia tuangalie uhalisia hata mimi nakataa kwa nguvu zote kucheat ila katka hali kama ya huyu dada kuna mengi ya kutazama sio akurupuke tu na kufanya maamuzi.
I hope mtoa mada kakuskia hapa. With this said, nawatakieni wote (u)siku njema (or mwema?).Unajua kuna kitu kinawachanganya wasichana wengi saana; NDOA.
Yaani yuko tayari awe na player as long as amemvisha pete na kumhakikishia atamuao.
Wanasahau kuwa kuna life after marriage ambayo ni very tough kuliko maisha ya urafiki na uchumba.
Nina best yangu mmoja, dada mzuri hasa wala si wa kudoda ni wa kuchagua tu awe na nani ila alimzimikia pedeshee mmoja (beutiful girl love bad boys) wakati tuko college.
Kashindwa kumuacha [mume wake player] akiwa msichana ataweza kumuacha leo hii wana watoto watatu na makaratasi juu (ndoa)?