Mwenzako wa ndoa anapo-chakua/chakachuliwa

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
Nimesoma mahali fulani mwanamume anatafuta ushauri baada ya kugundua kuwa mke wake amemsaliti, lakini linaweza kumfika mwanamke pia, iwe kwenye ndoa au katika mahusiano tu. Mkasa ulikuwa hivi:

Mwanamume mmoja wa Argentina aliondoka kwenda kupiga box Marekani kwa lengo la kutafuta maisha mazuri kwa familia yake. Safari iliyotarajiwa kuwa ya mwaka mmoja ikageuka kuwa ya miaka mitatu. Wakati wote alikuwa anawasiliana na mke wake. Aliporejea, rafiki yake akamweleza kuwa aliwahi kumuona shemeji disko na dume fulani. Mume alipomwuliza mke wake, mwanzo alisema kuwa alikuwa rafiki tu, lakini baada ya mume kumbana sana mkewake, alikiri kuwa alikuwa na uhusiano na baadhi ya wanaume (10 kwa idadi) kutokana na upweke, lakini anajuta na bado anampenda zana.

ANGALIZO: Mwanamume alihakikisha kuwa katika kipindi hicho cha miaka mitatu kamwe hakuwahi kuwa na uhusiano na mwengine kwa sababu kazi zake zilimkosesha muda kabisa, hata hivyo alikiri kuwa kama angelipata nafasi angeliitumia.

Wana JF, unaweza kujibu moja au yote kati ya maswali haya pamoja na maoni mengine uliyonayo. Ikiwa ni wewe, mwanamume au mwanamke, ukikumbana na kadhia kama hii, ungefanya nini?
1. Ungelimsamehe mwenzako na kukubali sababu za mwenzako?
2. Ungelimwacha kwa kuwa amekusaliti?
3. Kweli masafa na kutengana kwa muda mrefu ni kikwazo kwa ndoa/mahusiano?
4. Muda gani mwanamme/mwanamke anaweza kustahamili upweke?

Nawakilisha.
 
wanaume 10 wote hao tena ndani ya miaka mitatu tu. huyo dada lazima ni changu. ampige chini tu hamna cha kusamehe wala nini!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom