VERITE-NUE
JF-Expert Member
- Jan 28, 2019
- 1,481
- 1,450
Mwanamke aliyekukataa awali ni kwa sababu hakuona thamani yako. Kama ukiona ameamua kurudi kwako sio kwa sababu sasa ameona thamani yako, bali ni kwa sababu chaguo lake la awali lilifeli na sasa anakuona wewe kama plan B yake. Yani wewe ni backup plan yake.
Usikubali kuwa chaguo la pili, usikubali kuwa tairi ya akiba (spare tyre).
Mwanaume anayeijua thamani yake na anayejitambua hawezi kukubali kufanywa kuwa spea tairi. Haruhusu mwanamke aliyemdharau mwanzo na ambaye hakuona thamani yake awali aingie katika maisha yake.
Wewe ni lulu na kama usipoitunza lulu iliyoko ndani yako, wanawake wataendelea kukufanya tairi ya akiba.
Neno la hekima humfaa mwenye hekima.
Kuwa na hekima!
Mwenyekiti wa wanaume nimemaliza!