upupu255
JF-Expert Member
- Sep 4, 2024
- 341
- 476
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera Cde. Faris Buruhani amewakumbusha vijana wa mkoa huo kuzikimbilia fursa kubwa na za muda mrefu zinazopatikana kwenye miradi mbalimbali ya serikali inayotekelezwa kwenye maeneo yao badala ya kuhangaika na fursa za siku moja ambazo hutokea mara moja tu kila baada ya miaka mitano.
Wito huo umetolewa na Cde. Faris wilayani Muleba alipokuwa akizungumza na wajumbe wa baraza la vijana wilaya wakati wa kikao cha baraza maalum kilichoketi kwenye kata ya Izigo wilayani humo.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Cde. Faris amewakumbusha wajumbe hao umuhimu wa kutafuta fursa za ajira katika miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ili waweze kunufaika na miradi hiyo na kuwasaidia kujiinua kiuchumi.
Kadhalika Cde. Faris amewahimiza kutimiza wajibu wao kila mtu kwa nafasi yake kwa kuwa waliomba nafasi ya kuwatumika vijana katika kata zao.
Katika hatua nyingine amewataka wajumbe hao kujifunza kuvumiliana, kustahimiliana, kwa kuwa hakuna anayejua kesho ya mwenzake.