Mwenyekiti wa UVCCM Arusha lawamani

buswelu moja

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
226
147
Jamani kuna taarifa leo kwenye gazeti la MAGAZETI leo kwamba Mwenyekiti wa Uvccm wilaya ya Arusha,SAITOTI ZELOTHE ambaye pia ni mtoto wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Rukwa,ZELOTHE STEPHEN amelalamikiwa na wanachama wa umoja wa vijana Arusha kwa kuanza kampeni mapema kabla ya muda.

Taarifa zinaeleza kwamba kijana huyu amekuwa akitumia jina la katibu wa Uvccm TAIFA,SHAKA HAMDU SHAKA kwamba hana wasiwasi jina lake litarudi baada ya mchujo maana ana wakubwa kule juu na kwa sasa anazunguka katika wilaya za KARATU NA MERU akiomba wapitishe jina lake kwa kuwa ana uhakika litarudi.

Sote tunajuliza pesa za kuzunguka kila kona ya wilaya anazipata wapi?pili tunajiuliza kwann ameanza kuzunguka mapema kabla majina hayarudi kutoka makao makuu baada ya mchujo je ana uhakika gani jina lake litarudi? tatu nani yuko nyuma yake huu ubavu wa kuzunguka anaupata wapi kipndi hiki cha RAIS MAGUFULI?

Mkurugenzi wa uchaguzi wa tuhuma hizi ni vyema mmngechunguza kwa umakini na kutupa majibu ya uhakika kama tunataka kutengeneza UVCCM yenye nguvu na sio yenye ushawishi wa watu fulani fulani najiuliza hivi hawa watu wanapataje ujasiri wa kufanya haya chini ya utawala wa RAIS MAGUFULI?
 

Attachments

  • IMG_20171029_135204.jpg
    IMG_20171029_135204.jpg
    320.6 KB · Views: 29
Back
Top Bottom