PreGE2025 Mwenyekiti wa UVCCM Ali Kawaida: Nilishawahi kusema Mtandao wa X ufungwe ila watu walinibeza

PreGE2025 Mwenyekiti wa UVCCM Ali Kawaida: Nilishawahi kusema Mtandao wa X ufungwe ila watu walinibeza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Blessed Tajiri

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2023
Posts
221
Reaction score
659
Mwenyekiti wa UVCCM Ali Kawaida akiongea hivi karibuni kwenye mkutano mkuu wa CCM jijini Dodoma ameendelea kushikilia msimamo wake wa kufungia mtandao wa X ambao aliutoa miezi kadhaa iliyopita

"Nilishawahi kusema Mtandao wa X ufungwe ila watu walinibeza bila kujua nini nilichokuwa namaanisha katika maoni na maoni yangu niliyatoa. Hatukatazi watu kutoa maoni, mawazo yao, changamoto zao na kama tunaruhusu hayo mambo kuendelea. Mimi kama Mtanzania ambaye ni kijana siwezi kuruhusu Rais wangu kukejeriwa, kubagazwa"

"Tunapomzungumzia Rais Samia Suluhu Hassan ni Kiongozi Mkuu wa nchi na kwa nyumbani tunazungumzia mama au baba ni nani ambaye yupo tayari kumuona baba yake na mama yake akitukanwa na mtu mwingine? Ni sawasawa na Rais wangu yupo katika kuwawakilisha Watanzania. Nakereka sana"-
Mohammed Kawaida, Mwenyekiti UVCCM Taifa kwenye mkutano wa Kijani Power CCM Dodoma.


 

Attachments

  • Screenshot_20250530_101627_Instagram.jpg
    Screenshot_20250530_101627_Instagram.jpg
    406.6 KB · Views: 20
Imagine una vijana wajinga kama hawa na ndio wanaopata vipaza sauti kusambaza sauti zao! Hii ni hatari kwa usalama wa nchi

====


Nilishawahi kusema Mtandao wa X ufungwe ila watu walinibeza bila kujua nini nilichokuwa namaanisha katika maoni na maoni yangu niliyatoa. Hatukatazi watu kutoa maoni, mawazo yao, changamoto zao na kama tunaruhusu hayo mambo kuendelea. Mimi kama Mtanzania ambaye ni kijana siwezi kuruhusu Rais wangu kukejeriwa, kubagazwa.

"Tunapomzungumzia Rais Samia Suluhu Hassan ni Kiongozi Mkuu wa nchi na kwa nyumbani tunazungumzia mama au baba ni nani ambaye yupo tayari kumuona baba yake na mama yake akitukanwa na mtu mwingine? Ni sawasawa na Rais wangu yupo katika kuwawakilisha Watanzania. Nakereka sana"- Mohammed Kawaida, Mwenyekiti UVCCM Taifa kwenye mkutano wa Kijani Power CCM Dodoma.
Hamna kitu kichwani hapa
 
Back
Top Bottom