Mwenyekiti wa kijiji chetu bado hajatambua kuwa amepanda cheo anadhani yeye bado ni mjumbe tu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Mwenyekiti wetu hapa kijijini(jina la kijiji nalihifadhi kwa sasa) tangu achaguliwe kuwa mwenyekiti wetu inaonekana bado hajatambua wadhifa mpya alionao na zaidi majukumu mapya aliyonayo na badala yake bado anadhani yeye ni mjumbe tu wa serikali ya kijiji kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Huyu mwenyekiti wetu kabla hajachaguliwa kuwa mwenyekiti hivi karibuni, alikuwa ni mjumbe katika serikali iliyopita ya kijiji na alikuwa amepewa jukumu la kusimamia kitengo cha miundombinu ya kijiji. Mwenyekiti huyu pamoja na kupanda cheo, bado anaonekana ku-deal zaidi na kitengo kile kile cha awali ambacho sasa amekipanua zaidi na kusahau vitengo vingine vyote hapa kijijini.

Ushauri wangu kwake ni kuwa hivi sasa anapaswa kutambua kijiji kizima kinamuangalie yeye hivyo asijisahau akumbuke na vitengo vingine maana wanakijiji hivi sasa wanaumia kwasababu vitengo vingi hapa kijijini havina kitu na ni kama vimesahaulika kabisa.

Mh.Mwenyekiti unaua kabisa morali ya wanakiji waliko mtaani hapa kijijini kwetu na hata wale wanaofanya kazi katika vitengo hivi maana kwa sasa umewasahau.

Mwenyekiti acha kabisa kuelekeza fedha nyingi kwenye kitengo kimoja kisa kitengo hiki kina vitu vingi vya kuonekana machoni pa watu ukidhani vitu hivi ndio vitawashawishi wanakijiji kukuchagua safari iyajo wakati wao maisha yao yakiendelea kuwa magumu.

Katika kijiji chetu kwa sasa ni kila siku afadhali ya jana na mwenyekiti katia pamba masikioni na miwani ya mbao juu sasa sijui tutakimbilia wapi na nani tumlilie!
 
Huyo atakuwa Jamali Mahindi...yule aliekuwa mwenyekiti wa kamati ya kuzibua mitaro na vichochoro:
 
Back
Top Bottom