Mwenyekiti wa CCJ, Richard Kiyabo avamiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenyekiti wa CCJ, Richard Kiyabo avamiwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Mar 31, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  MWENYEKITI wa Chama Cha Jamii (CCJ), Richard Kiyabo, amevamiwa na kuporwa mkoba uliokuwa na nyaraka za chama hicho kinachopigania usajili wa kudumu.
  Kiyabo, anadaiwa kuwa alivamiwa na watu wanne wasiofahamika na kumpora mkoba wake uliokuwa na nyaraka mbalimbali za chama hicho kilichojizolea umaarufu katika kipindi kifupi.
  Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa tatu asubuhi jijini Dar es Salaam katika maeneo ya Kariakoo, Mtaa wa Msimbazi, jirani na jengo la klabu ya soka ya Simba, ambapo Kiyabo alikuwa akitembea kwa miguu.
  Baada ya tukio hilo, Kiyabo alitoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Msimbazi na kupatiwa RB yenye namba MS/RB/3606/2010.
  Akizungumza na Tanzania Daima jana, mwenyekiti huyo alisema alishangazwa jinsi tukio hilo lilivyotokea, kwani lilifanywa kwa kushitukiza na watu hao waliokuwa katika gari dogo aina ya Toyota Cresta, ambalo hakuweza kutambua namba zake.
  “Kwa kweli hadi sasa naona maisha yangu yamo hatarini… hii sasa ni mara ya pili kutokewa na tukio la aina hii, leo (juzi) asubuhi nikiwa Kariakoo nikifuatilia masuala ya chama, ghafla nilivamiwa na watu waliovalia makoti meusi na kupora briefcase yenye nyaraka mbalimbali za siri zinazohusu CCJ.
  “Walionipora walisimamisha gari lao mbele yangu kidogo kisha wakatoka na kunishika mikono yangu, halafu wakairudisha nyuma, nilikuwa naongea na simu, mmoja wao akatoa kitambulisho chenye nembo ya serikali akanionyesha.
  “Walipomaliza wakachukua begi langu wakaingia kwenye gari lao ambalo sikutambua namba zake, lakini niliona likiwa na vioo vya giza (tinted) wakaondoka zao… muda wote watu walikuwa wakipita wakiniangalia, lakini hawakunisaidia,” alisema Kiyabo.
  Alibainisha kuwa kutokana na kushtukizwa na tukio hilo, hakuweza kuwatambua kwa sura watu walioshiriki uhalifu huo anaouhusisha na harakati za kisiasa, hasa kipindi hiki ambacho chama chake kimekuwa kikifuatilia usajili wa kudumu.
  Alisema ingawa tukio hilo lilitokea mapema, lakini hakuna mpita njia aliyejitokeza kumsaidia zaidi ya kumuangalia huku wengine wakiendelea na shughuli zao.
  Kwa mara ya kwanza, mwanzoni mwa Februari mwaka huu, Kiyabo alikumbana na vitisho vya kuuawa alivyopokea kwa njia ya simu kutoka kwa watu asiowafahamu, hali iliyomfanya kutoa taarifa polisi.
  Muda mfupi baada ya kuvamiwa kwa mwenyekiti huyo wa muda, aliyekuwa Mbunge wa Kishapu kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Fred Mpendazoe, alikuwa kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) akieleza nia yake ya kukihama chama hicho kikongwe na kujiunga na CCJ. Tangu kuanzishwa kwake, CCJ imekuwa ikihusishwa na vigogo kadhaa wa CCM ambao baadhi yao wamekuwa wakikikana chama hicho ambacho katika kipindi kifupi kimeweza kuwa masikioni na machoni mwa wananchi, kutokana na habari zake kuandikwa na kutangazwa mara kwa mara na vyombo vya habari.
   
 2. G

  Godwine JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  ni kipindi kigumu kwa wanasiasa kwani kadri uchaguzi unapoelekea ndio hatari itazidi , kama wamezuia fedha kwenye kampeni watu watazitumia kukodi majambazi kuteketeza wengine

  poleni wanasiasa
   
 3. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Watu wazima wengine bwana! sasa hiyo picha hapo ni ya nini? Moderators kungekuwaga na kitufe cha opposite ya "thanks" kwa ajili ya vitu kama hivi
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  na wewe acha ujinga mweneykiti wa chama unatembea bila ulinzi na kwa nini utembee na documents za chama kwenye mkoba ??kwani huna ofisi?
   
 5. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mkuu Kigogo kama mtoto ndo kwanza anatambaa.
   
 6. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Unalilia Mods, Bwa! ha! ha! unaleta viroja kwa kutegemea Mods wakusaidie ha! ha! ha! eti Mods ha! ha! ha! ha! ninashkuru sana kwamba ujumbe umefika, saafi sana.

  Es!
   
 7. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Pole pole wananchi wanaanza kuamka, kumpora Documents ni dalili za uoga nani anayeogopa sasa wananchi au viongozi mafisadi? Unaona pole pole the game starts to change!

  Respect.


  FMEs!
   
 8. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #8
  Apr 1, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kila kitu kina muda ama wakati wake. Na wakati ni ukuta. Watanzania wamechoshwa na machafu ya CCM, hivyo hakuna mbinu itakayoweza kuzuia mageuzi ya kweli.
  CCM wameyataka wenyewe haya yanayotokea na yatakayotokea hapo mbeleni. Watanzania wa sasa si mabwege tena, wanaona na wanajua kinachoendelea na sasa wanataka haki na usawa wa kweli kwa kila mtanzania.
   
 9. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #9
  Apr 1, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 231
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  Hivi jamaa hana ofisi mpaka azunguke na mafile ya chama? Nitashangaa kama hawa jamaa watafika mbali. Naona wanalia lia sana ili kutaka kura za huruma.

  CCM wanahitaji ngangari na wala sio kulia lia.
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Apr 1, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Acha pumba wewe! If you dont cry for a Nation you must then be a fisadi.
  BTW inaonekana hii ni kazi ya usalama wa mafisadi....Si bure chama hiki kinawapeleka peleka.
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Apr 1, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huyu mwenyekiti vp tena?
  Anatembea na full doc k/koo! alitaka afoji nn maeneo ya gerezani?
  Dah inasikitisha sana hana hata ulinzi! Watakuwa CCM hao bila shaka.
   
 12. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #12
  Apr 1, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Hiyo ndio CCM maana hawa jamaa wanataka kuimaliza nchi,Wameshaona tayari hawa CCJ wanakuja kivingine kabisa ndio maana wanafanya hivyo...Na mengi sana yatatokea kwa hiki kipindi!!
   
 13. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #13
  Apr 1, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Uhuru wa kusema chochote (U-MC) wakati mwingine ni sehemu ya tatizo, hivi una sababu ya kuwa na nyaraka ofisini ambazo haziruhusiwi kutoka nje ya ofisi? Nadhani hizi zitakuwa ni picha za ukutani kama ile ya muungwana vinginevyo nyaraka za ofisi hulazimika wakati fulani kuwa nje ya ofisi kwa sababu za ki utendaji. Unachonikumbusha: Umependa boga (CCM) hivyo umependa na ua lake pia ndio maana naona upo ku discourage wapenda nchi kwa kuwapenda walanchi.

  Mwe!!
   
 14. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #14
  Apr 1, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  -Sasa je hatuna uhakika kama ni usalama wa taifa wanaolipwa kwa hela za watanzania ndo wanafanya haya?

  Pia siri za chama mbona anaziweka ktk risk kiasi hicho?
   
 15. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #15
  Apr 1, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Inawezekana ni stage show ili ipatikane sympathy from watanzania kuwa wanadhulumiwa. Haingii akilini iweje atembee na siri za chama mkononi?? Jamani watanzania tumekuwa watoto kiasi hicho?
   
 16. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #16
  Apr 1, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,431
  Trophy Points: 280
  Kaporwa na TISS...
   
 17. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #17
  Apr 1, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Hata akiamua kuziacha ofisini hizo documents TISS wakitaka watakuja kuzichukua tu. Ni watemi wale wewe!!!!!

  Tiba
   
 18. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #18
  Apr 1, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Hii habari kanyaboya; leo ni April 1
   
 19. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #19
  Apr 1, 2010
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Unamdanganya nani? Mbona mimi niko nae hapa hata dalili za kuporwa hana??? Thibitisha uwongo wako. 1 Aprili???????????????
   
 20. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #20
  Apr 1, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Swali zuri sana
   
Loading...