gogo la shamba
JF-Expert Member
- Mar 1, 2013
- 6,669
- 2,165
Katika kipindi cha BBC Asubuhi, nimemsikia aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha ACT, pamoja na yote aliyoyasema eti kwamba anashangaa CUF na CCM wameanzisha mgogoro.
Kwa maoni yake anasema uchaguzi ulikuwa wa haki na amani na kura zilikuwa zinatangazwa kwa haki na amani, waangalizi wa nje na ndani wamesema hivyo, sasa hapo CUF wamesababishaje mgogoro hapo, wanaosababisha mgogoro ni CCM kwa kukataa kutangaza matokeo.
Ukweli ndio utakaomaliza matatizo ya Zanzibar, lakini tukiweka unafki na kujipendekeza kama baadhi ya viongozi wanavyofanya Zanzibar haitopata salama na hata huku bara hatutokuwa salama maana hata bara CUF wapo.
Kwa maoni yake anasema uchaguzi ulikuwa wa haki na amani na kura zilikuwa zinatangazwa kwa haki na amani, waangalizi wa nje na ndani wamesema hivyo, sasa hapo CUF wamesababishaje mgogoro hapo, wanaosababisha mgogoro ni CCM kwa kukataa kutangaza matokeo.
Ukweli ndio utakaomaliza matatizo ya Zanzibar, lakini tukiweka unafki na kujipendekeza kama baadhi ya viongozi wanavyofanya Zanzibar haitopata salama na hata huku bara hatutokuwa salama maana hata bara CUF wapo.
Akihojiwa katika kituo cha Radio cha Capital amesema na ameomba CCM NA CUF Zanzibar kamwe zisiwachanganye wananchi wala kuwavuruga wananchi
Akizungumzia suala hilo amesema Tokea mwaka 2000 visiwani Zanzibar kumekuwa na Mgogoro wa kisiasa na kusema kuwa huenda Zanzibar kuna kitu nyuma ya Pazia na Uchaguzi unatumika tuu kama kigezo lakini kuna kitu zaidi ya Uchaguzi katika siasa za Zanzibar Sababu mgogoro wa kisiasa Hauishi na kuwataka viongozi wa vyama hivyo viwili kukaa meza moja na Kuyamaliza!
Amesema kuwa Dr.Shein na Maalim Seif wasisahau kuwa wapo katika serikali ya kitaifa ambapo wao walikubaliana kuunda Serikali ya Mseto! Hivyo Kama Dr.Shein anaendelea kuitwa Rais inamaana serikali ya Mseto Zanzibar bado ipo
Akizungumza kwa umakini kabisa na kusema kuwa yeye hayuko katika upande wowote ule katika Mgogoro wa Zanzibar amesema Kuwa waangalizi na wasimamizi wauchaguzi walisema uchaguzi ulikuwa ni huru na wahaki na hivyo Maalim Seif kujitangazia kuwa Ameshinda Urais Zanzibar ni kitu cha kawaida tu kama watu walivyo nyumbani na kusema kuwa fulani kashinda lakini ushindi haupo kisheria kama tume haikumtangaza kuwa ni Mshindi
Ameshangwaza na CCM NA CUF Zanzibar kwa mda wa miaka 5 walio kaa madarakani pamoja kama walishindwa kujuana kisiasa na kushindwa kuongelea Ukomo wa mgogoro wa kisiasa Zanzibar ni kitu cha ajabu
Katika kutatua mgogoro huo amemuomba Rais wa JMT Dr.JPM kuingilia kati na kutatua mgogoro Huo! Na kusema kuwa alitegemea kuwa Siku ya Mapinduzi Zanzibar alitegemea Dr.JPM angepewa nafasi ya kuongea ili kujua mtazamo wake na utatuzi juu ya mgogoro huo lakini haikuwa hivyo
Alipo ulizwa suala la kurudiwa uchaguzi alisema haoni sababu wanaweza kurudia kuhesabu kura zilizo kwisha pigwa na Mshindi kupatikana na kutangazwa kisheria tofauti na Maalim Kujitangaza kinyume na Sheria Maana Wasimamiz wa Uchaguzi walikwisha sema ulikuwa Uchaguzi Huru na Wa haki!
Pia Mh Anna Mwigero Amempongeza Rais Dr.JPM kwa utendaji wake wa kazi na kumuomba kutokata Tamaa katika kupambana na Ufisadi!