TANZIA Mwenyekiti Umoja Wa Wanawake CCM Mkoa Wa SIMIYU Afariki Dunia

TANZIA Mwenyekiti Umoja Wa Wanawake CCM Mkoa Wa SIMIYU Afariki Dunia

Inside10

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Posts
33,615
Reaction score
40,162
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu kimepata pigo kufuatia kifo cha Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoani humo, Mariam Manyangu, aliyefariki dunia leo Jumamosi Machi 21, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Simiyu, Lumen Ngunda, marehemu amefariki dunia akiwa jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa chama kimepokea kwa masikitiko makubwa kifo hicho, kikimtaja Manyangu kuwa kiongozi aliyetoa mchango mkubwa katika kuimarisha umoja wa wanawake ndani ya chama na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya jamii mkoani humo.

Screenshot 2026-03-21 190903.png
 
Back
Top Bottom