Nimekuwa nikitafakari juu ya utendaji wa tume ya taifa ya uchaguzi toka tuingie mfumo wa vyama vingi kwa kweli hauridhishi na unatia shaka impartiality yake. Kwa utaratibu tulio nao sasa rais ndo anateua mwenyekiti na anaweza kumfukuza kazi muda wowote. Jambo hili siyo tu linamfanya mkuu wa tume kuwa na uwoga wa kukosa kazi bali pia unamfanya asiwe mtu wa kuamaminika pamoja na timu yake na vyama shindani.
Nilikuwa napendekeza rais abaki na haki ya kumteua lakini lazima kwanza ajadiliwe na bunge ahojiwe bunge likimpitisha ndo apewe kazi. Akishapewa kazi baada ya kumwapisha rais asiwe na nguvu ya kumwondoa isipokuwa bunge pekee au kamati maalum ya majaji wa mahakama ya rufaa baada ya kujiridhisha kwamba amekiuka maadili ya utendaji kazi wake.
Nawasilisha wana JF