ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 643
- 1,603
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman anazungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari muda huu katika Hoteli ya Serena.
Mazungumzo ya Mgombea Urais wa Zanzibar Kupitia ACT Wazalendo na Wahariri wa Vyombo vya Habari, Serena Hotel, Dar es Salaam tarehe 23 August 2025:
Ndugu zangu Wahariri na Waandishi wa habari,
Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana leo kwa ajili ya kupata kifunguwa kinywa pamoja asubuhi ya leo. Nawashukuru nyinyi kwa kukubali mualiko wetu na kuhudhuria mazungumzo haya asubuhi kwa lengo la kujuwana na kubadilishana mawazo.
Kwa hakika, huku ni kuendeleza utamaduni wetu wa miaka mingi wa kukutana ana kwa ana, kupata riziki pamoja, kutangamana na kuzungumza mambo yetu hapa na pale.
Lengo hasa ni huku kukutana na kuwa pamoja - nje ya vikao vya kikazi, nje ya vikao vya kisiasa. Tuwe na wasaa baina yetu kama wananchi wa nchi hii, kama ndugu na kama marafiki. Tuambizane moja kwa moja yale tunayotaka kuambizana. Tushauriane. Tuongozane. Tukosoane. Tuelekezane.
Ndugu zangu Wahariri na Waandishi wa Habari,
Huu ni mwaka wa uchaguzi nchini Tanzania katika pande zake zote mbili za Jamuhuri ya Muungano. Harakati za uchaguzi zilizoanza tangu kwenye uandikishaji wa wapiga kura zinaendelea na zitakamilika kwa upigaji kura na utangazaji matokeo mwishoni mwa mwezi Oktoba. Sisi ACT Wazalendo ni miongoni mwa wale walioamua kushiriki kila hatua ya uchaguzi huu.
Tunafahamu kuna changamoto kubwa kwenye mfumo mzima wa uchaguzi na utendaji wa taasisi na watu wanaohusika na uchaguzi wenyewe - kuanzia Tume za Uchaguzi, Polisi, Mahakama hadi maafisa wa Serikali katika ngazi mbalimbali. Changamoto sio tu za kitaasisi na kiutendaji, lakini ni za mfumo mzima wa uendeshaji wa shughuli za umma kwa misingi ya uwazi, haki, uwajibikaji na ustaarabu unaokubalika duniani.
Kwa hakika mazingira ni magumu sana. Katika hali hiyo, ni wazi kuwa hata mawazo ya kutafuta suluhu lazima yatatafautiana sana miongoni mwa wadau wote. Lakini chini ya kaulimbiu yetu ya “Piga Kura Linda Kura, Muhuni Hasusiwi!” tumeamua kuchaguwa kibaya kutoka kibaya zaidi. Kushiriki kwetu uchaguzi ni kuendeleza mapambano ambayo tumeyaanza miaka mingi. Ni kukabiliana na uhuni wa waliouteka nyara uhuru na demokrasia yetu. Ni kuwathibitishia kuwa uhuni wao hautaachwa ututawale milele na kwamba sisi wananchi wenye dhamira ya kweli tutakabiliana nao.
Ndugu Wahariri na Waandishi wa Habari,
Katika kuitimiza ndoto ya kila Mtanzania na kila Mzanzibari ya uhuru, usawa, maendeleo na umoja wa kweli, kila mmoja wetu hapa ana jukumu la kutekeleza kwa nafasi yake. Sisi tulioamua kutumia jukwaa la siasa na nyinyi munaotumia jukwaa la habari, tuna nchi moja ya kuijenga, taifa moja la kulirejeshea heshima yake, watu wa kuwasaidia kutunziwa utu na ubinaadamu wao.
Hivyo, pamoja na kwamba kukutana hapa ni kwa ajili ya kuendeleza utamaduni wa kuja pamoja baina ya wadau wa masuala ya umma, tunaomba pia iwe fursa ya kubadilishana mawazo ya jinsi ya kuutimiza wajibu wetu huu kwa taifa na watu wetu.
Upande wetu - kama ACT Wazalendo - daima tumekuwa tayari kwa mazungumzo na mijadala ya kina kwa ajili ya taifa letu. Tunajiita Chama cha Masuala kwa maana ya taasisi inayoshughulika na mambo makuu yanayoigusa jamii moja kwa moja. Ndio maana mara kwa mara tumekuwa tukifanya tafiti kwenye masuala mbalimbali na kuja na majibu yanayotekelezeka kwa vitendo.
Kuingia kwetu kwenye uchaguzi ni matokeo ya utaratibu wetu huo huo wa utafiti na utekelezaji. Ni kwa sababu hiyo, ndio mana nimeambatana na viongozi waandamizi wa Chama ili nao washiriki katika hafla hii.
Kwa hivyo, tunaendelea kuwakaribisha muchangiane nasi mawazo, fikra na hata ukosoaji kwenye jinsi ya kuutekeleza vyema zaidi wajibu wetu. Tasnia yetu ya vyombo vya habari ni daraja muhimu sana baina ya sisi tulio kwenye siasa za wazi na wananchi wa kawaida. Ukiacha macho na masikio ya kawaida, wananchi wanatuona na kutusikia sisi kupitia kwenu.
Kwa hakika, hata wenyewe kwa wenyewe tunaonana na kusikiana kupitia nyinyi watu wa habari. Ndio maana wito wetu kwenu ni kwamba kuweni macho maangavu na masikio masikivu ili hatimaye jamii nayo iwe elevu na erevu panapohusika masuala muhimu ya taifa leo - likiwemo hili la uchaguzi.
Ndugu Wahariri na Waandishi wa Habari,
Uchaguzi wa mwaka huu tumeuita uchaguzi wa maamuzi, na kwa Zanzibar tunasema ni mwaka wa kuinusuru Zanzibar. Wakati taratibu zitakapomalizika na kampeni kuanza, tutawajia Watanzania na Wazanzibari kuwaelezea jinsi ya kuyasimamia maamuzi yao na jinsi ya kuinusuru nchi yao. Chama chetu kilianza msimu huu wa Siasa kwa kuandaa AHADI YA CHAMA KWA WATANZANIA [Brand Promise] kwa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
AHADI YA CHAMA pamoja na tafiti zilizofanyika katika masuala mbali mbali yalitupelekea kuandaa ILANI za pande zote mbili za Muungano. Tutainadi ilani yetu na tutajenga hoja yetu. Tunawatarajia nyinyi wenzetu wa tasnia ya habari kuwa daraja la kuyavuusha hayo kwa uadilifu na ufanisi wa hali ya juu. Bila ya nyinyi, kila jambo linakwama.
Ndugu Wahariri na Waandishi wa Habari,
Mimi nimeamua kugombea nafasi ya Rais wa Zanzibar na nashkuru sana Chama changu na wanachama kwa kunipa imani na kunichagua kwa kura nyingi. Miongoni mwa mambo yaliyonisukuma ni kuamini kwangu kwamba yapo mambo ya msingi ambayo yanahitaji kurekebishwa kwa haraka Zanzibar.
Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na Katiba ya Zanzibar ya 1984 na Mfumo wa Muungano, Uchumi wa Zanzibar, Mfumo wa Uwajibikaji, Utendaji wa Vyombo vya Utoaji Haki, Utumishi wa Umma, Utawala Mwema, Mfumo mzima wa usimamizi wa ardhi Uwezeshaji Kiuchumi, Uwezeshaji Wananchi katika Maisha, Mustakbali wa Urithi wa Zanzibar, Huduma za Kijamii na Matumizi ya Teknolojia.
Ninaamini taaluma, uzoefu, imani na dhamira yangu ya dhati kwamba Zanzibar inahitaji mageuzi makubwa sana ili ipate maendeleo endelevu, ustawi wa kijamii na amani na utulivu wa kudumu.
Huu ni uwanja mpana ambao tunaweza leo hii kuutendea haki kwa kubadilishana mawazo, kupeana ufafanuzi wa mambo kadhaa ambayo mtakuwa na haja ya kupata ufafanuzi na kupeana rai na mawazo juu ya namna ya kukabiliana na changamoto ziliopo katika maeneo hayo.
Ndugu Wahariri na Waandishi wa Habari
Baada ya kuyasema hayo, nirejee kuwashukuru kwa kuja kwenye mualiko wetu huu. Kama nilivyosema, hiki si kikao rasmi bali ni muda wa kutangamana, kujadili, kupeana mawazo na kuulizana pia.
Kwa sababu hiyo, mukinipa zawadi ya masuali, mawazo, michango na chochote kile cha kunielekeza, nitaipokea kwa mikono miwili mimi na wenzangu niliojumuika nao hapa. Nasi tupo tayari kushirika mjadala, kutoa ufafanuzi na kujibu maswali yoyote yanayoakisi hafla hii.