WA-UKENYENGE
JF-Expert Member
- Oct 1, 2011
- 2,918
- 1,233
Duh, pole sana wana Ipuli na Tabora! RIP Mwenyekiti!
WanaJF,
Usiku wa kuamkia leo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Uyui mkoani Tabora (Mh. Mashaka) ameuawa kikatili kwa risasi akiwa nyumbani kwake eneo la Ipuli nje kidogo ya mji. Ameuwawa akiwa na familia yake ambapo inasemekana ni wezi, iko hivi...
Hili ni tukio baya kabisa likiwa ni la pili ndani ya miaka 5 kuhusisha madiwani/wenyeviti wa Uyui Districts na huwa hakuna taarifa kubaini wauaji zaidi ya kuzungushwa.
- Nyumba yake imepigwa jiwe kubwa mlangoni maarufu kama 'fatuma' na kuweza kuingia ndani.
- Amemiminiwa risasi 7 mkono wa kulia.
- Risasi 8 upande wa mkono wa kushoto.
- Amekatwa panga utosini na fuvu kuchanika.
- Alikuwa na familia yake nyumbani.
- Mazishi yatafanyika siku ya jumapili katika kijiji cha Utyatya-Sikonge.
- Alikuwa ni diwani wa kata ya Iyenze.
- Ameuwawa kati ya saa saba usiku na saa nane usiku.
- Ameuwawa akiwa ndie mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Uyui.
- Taarifa za kiintelijensia bado hazijatolewa na chombo kinachohusika.
- Wauaji nao bado hawajapatikana.
Mwaka 2008 tarehe 19 saa tatu usiku aliuawa diwani ambaye alikuwa ni babu yangu aitwae Salum Said Mgeleka wa kata ya Ibiri ambapo hadi tuongeavyo hakuna taarifa zozote za kiintelijensia zilizobaini wauaji zaidi ya porojo. Mzee Mgeleka aliuawa kwa kupigwa risasi tatu pajani na kutelekezwa jirani ya mtaro ambapo bleeding ilisababisha kifo chake. Huyu pia alikuwa jirani kabisa na nyumbani kwake. Inaogofya.
MY TAKE: Tabora inatisha sana kwa mauaji ya aina hii, serikali zote kuu zipo lakini sijui tatizo ni nini. Kuna harufu mbaya sana. Wale wanaowania nafasi fulani za Tabora wawe chonjo na aina hii ya mauaji.
Source: Madiwani 2 wa Uyui, kunijuza kwa kunipigia simu.
Je Polisi wametoa kauli gani?

Hata aliyefariki? Tabora hakuna upinzani. Majimbo na Halmashauri zote ni za CCM. Poleni wafiwa.
nakumbuka kuna diwani wa tabora,kanyenye alivyolambwa risasi kwake,siku moja kabla ya kutoa ushahidi mahakamani dhidi ya mkurungenzi (mama khalfan na genge lake wakina munde tambwe)walivyokuwa wakitafuna pesa za halmashauri.isije ikawa ndio yaliomkuta huyo diwani.tabora huwa ni shamba la bibi.ni sehemu pa kuchumia mihela.
Nio maana hawaendelei.
Mimi siku hizi huwa siwalaumu viongozi lahasha ila nawalaumu wananchi. Kwanini tusiwatupe nje hawa magamba? Tabora hakuna upinzani kwa nini? Tunalalamika halafu uchaguzi ukifika mtu anaridhika na pipi! Maamuzi ya kuondoa upuuzi wote huu na uushenzi huo wa kuuana yako mikononi mwa mwanachi. Sio kweli kwamba hawajulikani wauaji ila mijitu mingine inaficha tu uharamia kama huu. Serikali yetu imisha kuwa ya kishenzi sana, tunahitaji uongozi wenye dira na dhamira ya kumlinda mwanachi. Je tutafika kweli? Labda miaka 100 ijayo maana kwa akili hizi tulizonazo sasa hivi haitawezekana. Unamuua mwenzio kisa uongozi? Hao wanajulikana sana wanajf