Mwenyekiti CHADEMA mkoa wa Njombe ahamia CCM

Jamjicho

Member
Jan 25, 2016
15
45
Aliyekua MWENYEKITI wa CHADEMA MKOA WA NJOMBE WAKILI EDWIN ENOSY SWALE AMEHAMIA CMM
Edwin Enosy Swale mwaka 2015 aligombea ubunge kuptia tiketi ya Chadema kwenye Jimbo la lupembe, hata hivyo leo tar 06/10/2019 ametangaza rasmi kujiunga na chama cha mapinduzi katika ofisi za CMM mkoa wa Njombe
IMG-20191006-WA0034.jpeg
IMG-20191006-WA0025.jpeg
IMG-20191006-WA0032.jpeg
 

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
31,404
2,000

Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
4,099
2,000
Boss sijui ni kuwahi kuwa wa kwanza au vipi ila umefoa ile mbaya aisee. Mara chadema kwenda chadema mara cmm!

Anyway tumeelewa mkuu. Mwenyekiti wa chadema mkoa wa Njombe kahamia CCM, hichi ndio ulimaanisha?
 

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
20,560
2,000

mikedean

JF-Expert Member
Mar 15, 2018
2,867
2,000
Sawa hiyo kawaida ila punguza kuchapia una undugu na Musiba? Una undigu na JPM una undugu na........maaaa hao ndo mabingwa wa kuchapia+uongouongo
 

Admin1988

JF-Expert Member
Mar 30, 2017
1,175
2,000

LIMBOMAMBOMA

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
9,062
2,000
Vipi yeye kahaidiwa kupewa mkoa UPI? Maana nasikia hata mbunge mmoja Kule Moro Wa upinzani kahaidiwa kupewa mkoa akiunga juhudi
 

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
15,454
2,000
Aliyekua MWENYEKITI wa CHADEMA MKOA WA NJOMBE WAKILI EDWIN ENOSY SWALE AMEHAMIA CMM
Edwin Enosy Swale mwaka 2015 aligombea ubunge kuptia tiketi ya Chadema kwenye Jimbo la lupembe, hata hivyo leo tar 06/10/2019 ametangaza rasmi kujiunga na chama cha mapinduzi katika ofisi za CMM mkoa wa Njombe View attachment 1224895 View attachment 1224896 View attachment 1224898
Kijana wa Malangali high school, classmate wa DC wa Dodoma mjini huyu........Siasa buana kazi kweli
 

Alex Mbwilo

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
346
500
Aliyekua MWENYEKITI wa CHADEMA MKOA WA NJOMBE WAKILI EDWIN ENOSY SWALE AMEHAMIA CMM
Edwin Enosy Swale mwaka 2015 aligombea ubunge kuptia tiketi ya Chadema kwenye Jimbo la lupembe, hata hivyo leo tar 06/10/2019 ametangaza rasmi kujiunga na chama cha mapinduzi katika ofisi za CMM mkoa wa Njombe View attachment 1224895 View attachment 1224896 View attachment 1224898
Joto na fukuto kali lisilowahi kutokea hapa nyumbani tutalishuhudia mwakani, na baada ya hapo inawezekana ndio tutakuwa na wanasiasa kweli, maana kwa sasa matumbo yanawaendesha watu wanaojifanya ni wanasiasa. Ni dalili nzuri kwa mstakabali wa siasa za nchi siku za mbele.CCM isimkatae mtu chukua wote kabisa, kwa kuwa huu ni mwelekeo wa kuja kuwa na wanasiasa hasa katika taifa letu.
 

Jamjicho

Member
Jan 25, 2016
15
45
*MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA NJOMBE AJIUNGA NA CCM ASEMA RAIS MAGUFULI ANASTAHILI KULINDWA*

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Njombe Ndg, Edwin Swalle na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Jimbo la Lupembe Mkoani Njombe Ndg, Msafiri Mpolo wametangaza kukihama Chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.

Ndg, Edwin Swalle na Ndg, Msafiri wametangaza uamuzi huo katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Njombe, na kupokelewa na Viongozi wa CCM wakiwemo Madiwani kutoka Kata mbalimbali Wilayani Njombe waliokuwa wakiendelea na Kikao chao na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi, Ruth Msafiri.

Licha ya kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Njombe Edwin Swalle ni Wakili Msomi na alikuwa Mwanasheria wa Chama hicho pia ni Miongoni mwa Wagombea nafasi ya Ubunge Mwaka 2015 katika Jimbo la Lupembe kupitia CHADEMA akishindana na Mbunge wa Jimbo hilo aliyeibuka Mshindi kupitia CCM Mhe, Joramu Hongoli.

Akitangaza Kuihama CHADEMA na Kujiunga na CCM Wakili Swalle amesema hana Chuki na Mbunge wa Jimbo la Lupembe Mhe, Joramu hongoli badala yake atatumia Taaluma aliyonayo kuhakikisha anamsaidia Mbunge huyo na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli katika Kutekeleza Majukumu yao.

“Bahati Pekee ambayo Tanzania tumeipata ni hii ya kumpata Rais Magufuli, hatakiwi kutukanwa bali anahitaji kuungwa Mkono, haitaji Kukosolewa ila anahitaji kulindwa na kushauriwa ili azidi kututumikia Watanzania, tumeona Soko la Kisasa, Stendi kubwa na Hospitali kubwa Imejengwa Njombe ” Bw, Swalle.

Hatahivyo amesema Ameamua Kujiunga na CCM bila kushauriwa na Mtu yeyote ni Baada ya kuridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho unaofanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli ambae ameamua kuirudisha Heshima ya Chama Cha Mapinduzi Nchini.

“Nilikuwa Nchini Afrika Kusini ilipotua Ndege ya Tanzania Wenzetu kule wanasema Magufuli anaingia Nchini nikatafakari sana na kuona kweli Rais Wang ni mtu wa kuungwa Mkono na kila Raia mwema wa Tanzania mwenye nia ya kutaka Taifa hili lizidi kupaa kiuchumi” Ameeleza Wakili Msomi Edwin Swalle.

Msafiri Mpolo alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Jimbo la Lupembe amesema kwasasa vyama vya Upinzani ikiwemo CHADEMA havina tena Ajenda zitakazo wasaidia kuikosoa CCM kwakuwa chama hicho kupitia Serikali yake iliyoko Madarakani kimemaliza hoja zote za Upinzani.

“Nataka niwaeleze Vijana wenzangu wa Njombe sasa Vyama hivi vya Upinzani havina tena Hoja ya kuikosoa CCM, nyakati zimebadilika Chama hiki tulichokuwa tunakikosoa kimeamua kubadilika kimemaliza hoja zote za Upinzani hivyo haina haja ya kuendelea kushangaa naomba katika kipindi hiki kifupi tutumie nafasi hii kubadilika” Msafiri Mpolo.

Mbunge wa Jimbo la Lupembe kupitia Chama Cha Mapinduzi Mhe, Joramu Hongoli amempongeza Wakili Swalle kwa kuamua kujiunga na CCM na kusema, anaamini watashirikiana katika kuwatumikia Wananchi wa Lupembe na Mkoa wa Njombe kwa ujumla.

Baada ya kujiunga na CCM Wanachama hao kutoka CHADEMA Wamekabidhiwa Kadi za Chama Cha Mapinduzi na kula Kiapo cha Uadilifu ndani ya Chama mbele ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Njombe Ndg, Edward Mgaya, ambae amewakaribisha ndani ya Chama hicho na kuahidi kuwa CCM itawapa ushirikiano wa karibu.

Awali Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Njombe Ndg, Hanafi Msabaha alisema, Wakili Swalle aliandika Barua na kuikabidhi Ofisini kwake akiomba kujiunga na Chama Cha Mapinduzi Ombi ambalo CCM kupitia Vikao vyake iliona ni vyema kumpokea kwakuwa ni Kijana Msomi ambae atakuwa Msaada ndani ya Chama na Serikali.

*KAZI NI KIPIMO CHA UTU, CHAPA KAZI TULINDE UHURU NA UTAIFA WETU, Imetolewa na Ofisi ya Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Njombe.*
 

Drift

Member
Jul 27, 2019
73
125
Aliyekua MWENYEKITI wa CHADEMA MKOA WA NJOMBE WAKILI EDWIN ENOSY SWALE AMEHAMIA CMM
Edwin Enosy Swale mwaka 2015 aligombea ubunge kuptia tiketi ya Chadema kwenye Jimbo la lupembe, hata hivyo leo tar 06/10/2019 ametangaza rasmi kujiunga na chama cha mapinduzi katika ofisi za CMM mkoa wa Njombe View attachment 1224895 View attachment 1224896 View attachment 1224898
Hongera kwa kuchagua njia sahihi
Hivi hata angebaki huko kwenye chake angeongelea kitu gani ambacho hakijatekelezwa..?
Macho yake yanaona vizuri yanayoendelea..!
Hongera sana Mkuu Edwin Ennosy..
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,054
2,000
Hongera kwa kuchagua njia sahihi
Hivi hata angebaki huko kwenye chake angeongelea kitu gani ambacho hakijatekelezwa..?
Macho yake yanaona vizuri yanayoendelea..!
Hongera sana Mkuu Edwin Ennosy..

Kama angebaki angeweza kuzungumza mengi ikiwepo ajira, kilimo, deni la taifa, demokrasia nk. Mtu asiyejua siasa tu ndio atakosa cha kuongea.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom