Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Kusini wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mjumbe wa Kamati Kuu, Aden Mayala amekihama chama hicho na kutimkia Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Oktoba 22, 2025 wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika viwanja vya Kecha Ilala Jijini Dar es Salaam