Tuanze kwanza Database relationship ni nini? Database relationship tunaweza kudadavua kama ni uhusiano wa data katika database yako ambazo zipo katika muundo ambao unaitwa ‘tables’(sijui kiswahili chake fasaha may be ‘meza’ …just kidding)
Uhusiano huu huhusisha kuwepo kwa ‘foreign key’ katika kila ‘table’ ambazo zinahusiana, foreign key ndio inabeba dhana nzima ya database relationship.
Unapotengeza tables katika database yako lazima kila table inakua na primary key yake ambayo hua katika mfumo wa integer(namba), primary key hii hua ni utambulisho (identity) ya kila rekodi unayotunza katika database yako ambapo hua ipo unique na inakua generated automatically kwa kutumia auto increment feature kila rekodi mpya inapoingia.
Tukirejea kwenye database relationship, foreign key katika table huwakilisha primary key ya table nyingine katika kuleta ule uhusiano wa table hizo.
Nikianza kujibu swali lako sasa ambapo ni aina za database relationship kama ulivyoziorodhesha
1. One to One
2. One to Many
3. Many to Many
4. Many to One
Nianze kwa kuelezea moja baada ya nyingine
- One to One
Hii ni inahusisha utunzaji wa rekodi moja katika tables mbili tofauti, let say tuna database ya shule, ambapo kuna table ya walimu na table ya masomo, kwa kutumia aina hii ya relationship mwalimu mmoja ana uwezo wa kufundisha somo moja tu vilevile kwa masomo, somo moja litafundishwa na mwalimu mmoja pekee.
- One to Many
Hapa rekodi moja katika table moja inakua na uhusiano na rekodi nyingi katika table nyingine, mfano tukitumia mfano wa database yetu ya shule, mwalimu ana uwezo wa kufundisha masomo mengi huku somo moja linaweza kufundishwa na mwalimu mmoja pekee. Hapa foreign key itakaa kwenye table ya masomo kurefer primary key ya mwalimu husika wa hilo somo katika table ya walimu.
- Many To Many
Aina hii ya uhusiano ni ngumu kidogo ukilinganisha na nyingine, hapa unakuta rekodi nyingi katika table moja inakua na uhusiano na rekodi nyingi katika table nyingine and vice versa, katika kutengeneza relationship kati ya table mbili zenye uhusiano wa namna hii, table ya kati (pivot table) hutumika ambapo inakua na primary keys kutoka table zote mbili.
Nadhani nimetoa mwanga kidogo maana nikieleza kwa mapana zaidi maelezo yatakua mareefuuuu sana, karibuni wadau tujadili zaidi