Brigedia Chan-ocha
JF-Expert Member
- Mar 7, 2014
- 1,353
- 2,851
Bila kumung'unya maneno vifungu hivi vya katiba ya Zanzibar vimekiuka katiba ya muungano na ni vya kihaini! Hivyo kwa mamlaka ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anatakiwa kuifuta katiba hii na kuwafungulia mashtaka ya kihaini wote waliohusika katika kuiandaa katiba ya Zanzibar!Wabadili katiba yao hasa hasa vifungu hivi....
1. Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la
Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka
na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
2A. Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali, Rais
aweza kuigawa Zanzibar katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo
kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la
Wawakilishi.
6.(1) Kutakuwa na Mzanzibari ambaye upatikanaji wake, upoteaji
wake na urudishwaji wake atakuwa kama alivyoainishwa katika Sheria
iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.
26.(1) Kutakuwa na Rais wa Zanzibar ambaye atakuwa Mkuu
wa Nchi ya Zanzibar, Kiongozi Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Walivyo wajanja wakaweka kikwazo katika hii ibara ya 80A.
80A.(1) Bila ya kuathiri masharti ya kifungu cha 80 cha Katiba,
Baraza la Wawakilishi halitaweza kufanya mabadiliko ya Katiba
kuhusiana na sharti lolote liliomo katika kifungu chochote kilichoainishwa
katika kijifungu cha (2) cha kifungu hiki, mpaka kwanza mabadiliko
hayo yakubaliwe na wananchi kwa Kura ya Maoni.
(2) Kwa kuzingatia masharti ya kijifungu cha (1) cha kifungu
hiki, vifungu vinavyohitaji Kura ya Maoni ni:
(a) vifungu vyote vya Sehemu ya Kwanza ya Sura ya
Kwanza;
99. Mahkama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
itakuwa na uwezo wa kusikiliza rufaa kutoka Mahkama Kuu ya
Zanzibar isipokuwa kesi zozote zinazohusika na:
(a) tafsiri ya Katiba hii;
(b) mambo ya Kiislamu ambayo yameanzia katika
Mahkama za Kadhi;
(c) mambo mengine yoyote yaliyoainishwa katika Katiba
hii na Sheria nyengine yoyote iliyotungwa na Baraza la
Wawakilishi.
Bila kumung'unya maneno vifungu hivi vya katiba ya Zanzibar vimekiuka katiba ya muungano na ni vya kihaini! Hivyo kwa mamlaka ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anatakiwa kuifuta katiba hii na kuwafungulia mashtaka ya kihaini wote waliohusika katika kuiandaa katiba ya Zanzibar!
Unamawazo za kikoloni kweli eti halafu munajitia kuuita muungano.
huu ni ukoloni wa tanganyka kw znz na tutaupinga kw nguvu zetu zote.
Ni vema mkapinga kwa hoja za kisheria na si kwa kubwabwaja na kufanya fujo!Unamawazo za kikoloni kweli eti halafu munajitia kuuita muungano.
huu ni ukoloni wa tanganyka kw znz na tutaupinga kw nguvu zetu zote.
Hapo tutakushangaa. Hivi hujuwi kuwa wazanzibari wanaongozwa kwa katiba mbili . ya muungano ( jamhuri) na ile ya Zanzibar.Wazanzibari hawatokubali kesi hio ya uhaini kwa sababu katiba yao imewapa mamlaka ya baraza la wawakilishi kwa wakati huo kufanya MAREKEBISHO YALIYOFANYWA MWAKA 2010. Kumbuka Zanzibar sasa ni Nchi kamili na kabla ya hapo ilikuwa na maamuzi yake kupitia BLW. Kulilia huko ni masikitiko ya Tanganyika kukosa zile nguvu ilizozowea kuikaba na kuikandamiza Zanzibar kwa jina la Tanzania. Sisi tumeshatia mavumba na Ubani Lazima jinni aje juu. SAMAHANI LAZIMA JINI TANGANYIKA AJE JUU ILI TUONGEE NAE. MAANA WENYE MGONJWA HAWAKUBALI TENA.Bila kumung'unya maneno vifungu hivi vya katiba ya Zanzibar vimekiuka katiba ya muungano na ni vya kihaini! Hivyo kwa mamlaka ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anatakiwa kuifuta katiba hii na kuwafungulia mashtaka ya kihaini wote waliohusika katika kuiandaa katiba ya Zanzibar!
Hata sisi tushakuchokeni kupe nyie. Muungano ni serikali moja, hamtaki ondokeni.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010 ni batili kwa mujibu wa katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania! Nadhani JK aliwaachia muendelee na mchezo huo mchafu ili kuepusha mauaji mliyokuwa mnakabiliana nayo!!Hapo tutakushangaa. Hivi hujuwi kuwa wazanzibari wanaongozwa kwa katiba mbili . ya muungano ( jamhuri) na ile ya Zanzibar.Wazanzibari hawatokubali kesi hio ya uhaini kwa sababu katiba yao imewapa mamlaka ya baraza la wawakilishi kwa wakati huo kufanya MAREKEBISHO YALIYOFANYWA MWAKA 2010. Kumbuka Zanzibar sasa ni Nchi kamili na kabla ya hapo ilikuwa na maamuzi yake kupitia BLW. Kulilia huko ni masikitiko ya Tanganyika kukosa zile nguvu ilizozowea kuikaba na kuikandamiza Zanzibar kwa jina la Tanzania. Sisi tumeshatia mavumba na Ubani Lazima jinni aje juu. SAMAHANI LAZIMA JINI TANGANYIKA AJE JUU ILI TUONGEE NAE. MAANA WENYE MGONJWA HAWAKUBALI TENA.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010 ni batili kwa mujibu wa katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania! Nadhani JK aliwaachia muendelee na mchezo huo mchafu ili kuepusha mauaji mliyokuwa mnakabiliana nayo!!
Sasa hatuwezi kuendelea kuvumilia makosa hayo ya JK!
Prof. Issa Shivji anaweza.....
Ni vema mkapinga kwa hoja za kisheria na si kwa kubwabwaja na kufanya fujo!
Hatuwezi tukakubali katiba ya nchi kuvunjwa mchana kweupeee!! Hakika udhaifu wa JK kuwachekea chekea ndiyo umetufikisha hapa!
Hivyo nawashauri mjiandae kisaikolojia kupokea matokeo!
Kumbuka kwa mujibu wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Zanzibar ni sehemu ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na SIYO NCHI!Katiba ya nchi gani umevunjwa Mkuu,walichokifanya zanzibar ni kuzawazisha au kurekebisha katiba yao tu, ambayo ilikuwepo muda wote,,,kama zanzibar wangelilazamisha katiba ya Tanzania irekebishwe hapo ndio ingelikuwa uhaini...
Zanzibar ina Katiba yake kabla na baada ya mungano,Karume na nyerere walipounganisha nchi walichokifanya ni kuiacha katiba ya zanzibar kama ilivyo,wakachagua mambo 11 ambayo ndio yakawa ya mungano.
Nyerere akangojea mpaka 1977 akatengeneza katiba ya mungano ambayo vile vile ni katiba ya Tanganyika,,, na ndio maana wasomi kama akina Shvji na wengine pamoja na serikali ya Tanzania hawakuwea kufanya chochote wakati Karume anarekebisha Katiba ya Zanzibar.
Sasa wasomi serikali ya Mungano amabyo ndio serikali ya Tanganyika wamepagawa hawajui wafanye nini makosa sio yetu mimi na wewe makosa yako waasisi wa huu mungano feki Kaarume na Nyerere
Kumbuka kwa mujibu wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Zanzibar ni sehemu ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na SIYO NCHI!
Hata kwa katiba ya Zanzibar ya kabla ya 2010 ilisema Zanzibar ni sehemu ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania! Na hivi ndivyo Karume na Nyerere walivyoitunga na kuiacha!
Kusema Zanzibar ni nchi ni kuvunja katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na ni UHAINI!
Mpaka karume anauwawa mwaka 1972 Zanzibar haikuwa na Katiba. Karume alikuwa natawala kwa amri 'presidential decrees'. Katiba ya Uhuru ya 1963 ilfutwa baada ya Mapinduzi. Katiba ya kwanza rasmi ya Zanzibar ilitungwa mwaka 1984. Kwa hiyo Karume hakurekebisha Katiba ya Zanzibar. Tusipotoshane.Katiba ya nchi gani umevunjwa Mkuu,walichokifanya zanzibar ni kuzawazisha au kurekebisha katiba yao tu, ambayo ilikuwepo muda wote,,,kama zanzibar wangelilazamisha katiba ya Tanzania irekebishwe hapo ndio ingelikuwa uhaini...
Zanzibar ina Katiba yake kabla na baada ya mungano,Karume na nyerere walipounganisha nchi walichokifanya ni kuiacha katiba ya zanzibar kama ilivyo,wakachagua mambo 11 ambayo ndio yakawa ya mungano.
Nyerere akangojea mpaka 1977 akatengeneza katiba ya mungano ambayo vile vile ni katiba ya Tanganyika,,, na ndio maana wasomi kama akina Shvji na wengine pamoja na serikali ya Tanzania hawakuwea kufanya chochote wakati Karume anarekebisha Katiba ya Zanzibar.
Sasa wasomi serikali ya Mungano amabyo ndio serikali ya Tanganyika wamepagawa hawajui wafanye nini makosa sio yetu mimi na wewe makosa yako waasisi wa huu mungano feki Kaarume na Nyerere
Hapo Brigedia ndipo shida ilipo, akina Shivji waliohamasisha wazanzibari watunge hiyo katiba na kujiwekea hivyo vifungu... leo Wanakuja kumshutumu warioba kwa nini hajatoa pendekezo wazanzibari warekebishe katiba yao
Sitta anashindwa kuwa mkweli aeleze namna alivyochaniwa na kutupiwa rasimu ya kwanza Unguja, kunawatu wana macho ila hawaoni, wacha tuvute muda
Kwa mujibu wa Hati ya Muungano Katiba ni kati ya mambo 11 ya awali yaliyokubaliwa kuwa ya Muungano. Kwa hiyo Zanzibar haina mamlaka kikatiba ya kufanya lolote kuhusu hayo mambo 11. Ni Bunge la Jamhuri ya Muungano linaloweza kubadili katiba kuyaongeza au kuyapunguza.Kama Zanzibar sio nchi sasa Tanganyika imeungana na nini,,,,
Mkuu napenda Kurudia,,,Zanzibar wamerekebisha katiba yao,kila siku tunasikia malalamiko ya mungano pande zote mbili kwanini hizi kero hazikurekebishwa na chama na serikali inayotawala....mpaka imefikia hapa.
Katiba sio msahafu wala Biblia,Kutokana na mungano tuliokuwa nao Zanzibar ina uwezo wa kurekebisha katika yake kwani mambo ya ndani ya zanzibar sio ya muungano