Ipo hivi mkuu..!
Naomba nikujibu kwa kutumia mfano wa Chakula kilicho fungwa kwenye package.
Expire date ni tarehe ya mwisho ambayo hicho chakula kitakuwa ni salama kwa kukitumia.
Best-Before date ni tarehe ambayo ubora wa hicho chakula utaanza kupungua ( na sio usalama wa chakula )
Kwa maana hiyo basi chakula ambacho utakitumia after Expire date sio salama,
na kile ambacho utakitumia after Best-Before date, hicho kimepungua ubora (ingawa kinaweza kikawa ni salama kwa kula )