Thread yako nzuri kweli,ila umeuliza maswali ambayo kumbe ulitaka ufundishwe kwanza,ufupi kuna tofauti kubwa sana baina ya mwislamu na uislamu! bakwata ni mwislamu na mahakama ya kadhi ni uislamu,ktk uislamu kila jambo sheria ipo kama benk,afya nk.
Ukitaka kujua zaidi vp mahakama ya kadhi haiathiri uendeshaji na utekelezaji wa sheria za nchi pata taarifa toka Kenya, Uganda, Afrika ya kusini au Zanzibar. Pia hata waulize mawaziri wakongwe kama Wassira na wenzake akina George Kahama waliofanya kazi na nyerere kwani waliikuta ikitumiwa na mkoloni mpaka pale nyerere alipoamua kuifuta kwa sababu anazozijua yeye.
Hivi suala hili linahitaji mjadala bado? Mahakama ya kadhi ruksa.... ila waislamu waanzishe hata kwenye familia zao, sio jambo la serikali. Wawalipe makadhi wao kwa raha zao. Watunge sheria zao kwa raha zao, bila kuingilia sheria za nchi. Wakristo vilevile, mathalan wakatoliki, unadhani hawana sheria? Inaitwa Canon Law. Hii ni sheria mama ya kanisa lao. Waseme pia tuweke kwenye katiba ya nchi? Kwani nchi ni ya ukristo, usabato, uislamu.
Nadhani hapa tutashindwana. Ninahakika kwetu bara waislamu wasahau suala hili kwenye katiba ya Nchi. Labda huko kwao, wakakatane mikono na miguu na pua... si ndo tunayoona wenzao walio na mahakam ya kadhi?