Bakwata na katiba inayopendekezwa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,263
MAPENDEKEZO YA BAKWATA KUHUSU MAHAKAMA YA KADHI



DSCN1106.JPG
Sheikh Hamid Jongo

1. Leo kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 11 jioni tulikuwa ktk ukumbi Wa Julius Nyerere Conference katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala tukiwawasilisha mapendekezo ya Muswada wa Mahakama ya Kadhi. Tulikuwa taasisi 11: Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Tanzania, Annahar, Basuta, Tampro, Dumt, Shura ya Maimamu, jumuiya na taasisi mbalimbali kwa upande mmoja na Bakwata upande wa pili, Tanganyika Legal Society (TLS) nk nk. Pia alialikwa Jaji Robert Makaramba na Arcado Ntagazwa.

2. Maoni ya Jaji Robert Makaramba ni kuwa Mahakama ya Kadhi ni chombo halali na hakipaswi kuitwa cha kidini bali ni chombo cha dola, kigharamiwe na dola, Wakristo wasilalamike sababu hata mahakama za kawaida zinatumia sheria za Kikristo ambazo zinatokana na Common Law.

3. Bakwata wao wameiambia Kamati ya Bunge kuwa Mahakama ya Kadhi ni mahakama ya kidini hivyo isigharamiwe na dola bali zijigharamie zenyewe kama tunavyogharamia ''maji ya udhu,'' ''mikeka'' na ''umeme,'' misikitini, pia Mahakama ya Kadhi hiyo ndiyo hii Mufti aliyoiunda, na kwamba Mufti anayetajwa na muswada awe ni Mufti wa Bakwata hiyo iwe rasmi ndani ya sheria. Maoni ya Bakwata yamewasilishwa na Katibu wa Bakwata Mzee Lolila na Sheikh Hamid Jongo.

4. TLS wao wanapendekeza muswada huu uondolewe haufai.

5. Maoni yetu ya taasisi 11 kama yalivyoandaliwa na wanasheria kwa ushirikiano na masheikh yamewasilishwa na Wakili Njama. Kimsingi tumesema huu muswada haufai uondolewe na badala yake kamati tumeiomba ipokee muswada mbadala tuliouandaa ambao unaunda Mahakama ya Kadhi, unaunda Bodi ya Sheria za Kiislam ambayo ndiyo itakayoteua makadhi na kudhibiti nidhamu za makadhi, pia Waziri wa Sheria asipewe mamlaka ya kutunga sheria au kanuni zinazohusu Waislamu bila ya kushauriana na wanazuoni. Mahakama ya Kadhi tumetaka iwe sehemu ya "Judiciary," igharamiwe na dola. Bakwata na Mufti wa Bakwata wasiwe ndiyo wateuzi wa makadhi. Tumeitaka Kamati ya Bunge iishauri serikali iuondoe muswada wake haufai na wala haukidhi vigezo vya kuunda chombo chenye hadhi ya mahakama.

6. Ntagazwa ameeleza historia ya Mahakama ya Kadhi na ameeleza kuwa muswada huu hauna nia ya dhati kuanzisha Mahakama ya Kadhi ya ukweli bali nia ni kupata kura za Waislamu tu. Ntagazwa aliungana nasi kuwa muswada uondolewe.

7. TLS nao waliunga mkono hoja zetu kwa kiasi kikubwa. Katika kikao hicho kwa upande wetu tulikuwa mimi, Wakili Njama, Dr. Benhajj, Wakili Hamza Jabir, Masheikh: Kundecha, Kilemile, Sheikh Bawazir, Sheikh Mbalamwezi Mwanahistoria Mohamed Said na wengi wengine. Alhamdulillah tuliwakilisha vyema na wrote walituelewa tunaamini kazi tuliitimiza yaliyobaki Allah anajua zaidi. Mjadala ulikuwa mkali kutwa nzima lakini tuliwatuliza.
 
Huyu jaji Robert Makaranga anasema eti mahakama zinatumia sheria za Kikristo? Huyu ni janga kubwa. Ana jina la Kikristo lakini hajawahi hata kusoma Biblia. Watu wa namna hii wanakuwa chanzo cha mitafaruku kwenye jamii.
 
Huyu jaji Robert Makaranga anasema eti mahakama zinatumia sheria za Kikristo? Huyu ni janga kubwa. Ana jina la Kikristo lakini hajawahi hata kusoma Biblia. Watu wa namna hii wanakuwa chanzo cha mitafaruku kwenye jamii.

Mkuu jaribu kufahamu kwanza maana ya Sheria Kikristo.
Km tunavyofahamu ktk Historia kuwa Sheria nyingi za nchi yetu tumezirithi kutoka kwa Waingereza.

Na mpaka leo Uingereza inatawaliwa na Wawakilishi wa Church of England ambalo Custodian wake ni Queen akifuatiwa na Prince Charles.

Kwa maana hii Mr Makaranga Hakukosea kuyasema aliyo yasema.
Na wewe kumuita yeye Mkristo jina hakutobadili Ukweli wake.

Ahsante sana.
 
Back
Top Bottom