Mwenye makosa ni nani? Mke au mume?

mwanamke asiache kazi kamwe.......
ninachoona hapo huyo mwanamke anaangalia wanaomtazama......hivi akipata chongo au ulemavu kwa kipigo atamlaumu nani ( kuachwa ni aibu) unaachwa mnaachana???ushawekewa kika bibi huna kwenu....gari hakuna kuuza wala kuacha kazi....waambie wakurudishe kwenu......wanao kila siku wanaona unapigwa....mmeo sidhani kama alienda jandoni huyoo.....maisha hayasimami bibie.......songa mbele.....acha kazi then uje na story ya ukewenza.....
 
Straight the point bila kupepesa kushoto au kulia...

Mume ndiyo mwenyewe makosa tena makubwa sana...

Inakuaje mtu unayechunguliana nae viungo vya uzazi umtenge namna hiyo mpaka afikie hatua ya kujichukulia maamuzi yake...

Alafu ati bila aibu unataka ache kazi na kuuza vitu vyake... kama umeshindwa kumpa nafasi mke wako muache ajipe nafasi mwenyewe...

Na huyo mwanamke ana moyo sana kuvumilia familia yakijinga kama hiyo...


Cc: mahondaw
 
Straight the point bila kupepesa kushoto au kulia...

Mume ndiyo mwenyewe makosa tena makubwa sana...

Inakuaje mtu unayechunguliana nae viungo vya uzazi umtenge namna hiyo mpaka afikie hatua ya kujichukulia maamuzi yake...

Alafu ati bila aibu unataka ache kazi na kuuza vitu vyake... kama umeshindwa kumpa nafasi mke wako muache ajipe nafasi mwenyewe...

Na huyo mwanamke ana moyo sana kuvumilia familia yakijinga kama hiyo...


Cc: mahondaw


Uko vizuri
 
Wanaume wengine ndio mana wanagongewa wake zao... Sasa huyodada hayo anayopitia akipata wakumliwaza nje si ndoa itakuwa kama sehemu yakutunzia watoto tu....
Kwa hiyo akigongwa atakuwa amemkomoa nani ndugu?
 
Asee inakera mno lkn kaz usiache kabsa ukiacha utateseka mno vta picha Leo kaz unayo unafanyiwa hvo je ukikosa kaz Kansas!!!?? ,yaana inakera mpaka mtu unataman wanaume wte wa aina hii M. MUNGU awe anatchukua mapeeema hata Kabla ya kuoa kulko kuwa af rmot inakuwa kwenu mwanaume badala ya kuish Vyema na familia uloamua kuijenga, af alvyompuuz mpka watoto anawatenga shenz kabisa
 
kusema ukweli communication hapa ndio tatizo, pili wanawake wengi hufikiri hazii atabadilika with time, naamini alikuwa hivyo tangia wakichumbiana ila bibie hakuona tatizo. Ushauri wangu ni kwamba watu tuangalie mapungufu na kuyarekebisha kabla hatujaingia ndoani; na incase mapungufu yamejificha yakija onekana tuulizane kulikoni na kupata suluhu.
Wakati mwingine ukisoma story kama hizi ndo unajikuta kusema bora uwe tu single maza uishi maisha ya raha mustarehe katika dunia hii Mungu alotupatia.
Mmmh Shem na Usingo maza wapi tena
 
Kuna wanaume vichefuchefu..sasa aliolea nini..haya mambo unanioa alafu nakua kama invisible hapana..siwezi hata..na gari siuzi.
 
PART 2

Ni mume wangu kabisa. Niliyempenda .
Kikao kilimalizika hivyo. Kwamba Niuze gari.
Nikirudi nyumbani na mawazo kede kede
Alitumia uanaume wake pia.
Na cha kwanza alichoniambia ni hataki kuona gari inapaki nyumbani kwake.
Pili watoto wake wasipakie hiyo gari.
Nikiumia sana.
Hata kama ningeiuza bado singefaidi. Deni nakatwa mimi. Na sikujua hiyo pesa ingefanyia maendeleo gani.
Lakini kufanyia maendeleo haingekuwa na shida. Shida ni maendeleo ambayo hutakuwa na uhuru nayo .
Ungeweza kuniona na kiburi sana.
Lakini ni kwa sababu nilifika mwisho wa mawazo.
Nikichoamua ni kusaka mahali pa kuipaki hiyo gari. Nikapata hotel fulani. Na nikawa nampa mlinzi pesa ya chai asbh. Kila siku nalipa elfu 2000 kwa mlinzi.
NIkaona walau inanipa kupumua.
Maisha yakawa ni hayo tuu. Hakuna amani. Hakuna raha. Hakuna kuelewana .
Kila nikiraka kitu naamviwa..
KAMA UMEWEZA KUNUNUA GARI FANYA.
Nakumbuka siku moja mama yangu mzazi alivunjika mguu. Kijijini hakuna huduma nzuri.
Sikuwa na pesa. Nikamshirikisha mr. Mr akaniambia ulinunua gari nini kinakushinda?
Dah.
Na kweli hakutoa pesa gari ikazaa balaa.
Nikiwaza sana . Mwisho mama yake akaniambia hivi kiburi hadi lini?kama hiyo gari hutauza hapo sikanyagi. Maana huna adabu na umekuwa na majivuno.
Dah. Ni mama huyu. Wa miaka 57. Mtu mzima sana. Anaongea ujinga kama huu. Sikumjibu. Nikinyamaza. Lakini msg za kila siku. Mpaka nikaamua kuwablock.
Siku moja mama akawa anataka dawa za kuku. Akampigia mr akamkosa.
Kisha akaniandikia na mimi msg.
Kwa vile nilimblock msg haikuingia. Na sikuiona.
Mama akamuonyesha mwanawe msg ya kuhusu dawa kumbe kwangu haikufika.
Mr akachukia sana.
Akaniambia kama unaweza kum block mama yangu mzazi huna maana. Ondoka.
Nilikuwa na hasira sana. Nikaona sass hawa issue sio gari. Issue ni hawanitaki. Yani gari tu ndo inazua balaa nyingi hivi?
Nikamwambia Mr. NITAONDOKA ILA NA WANANGU.
Kama ni kuondoka nifungashie wanangu. Then niondoke nao.
Mr akaniambia sawa. Akapigia ndugu zake simu waje Kwa kikao.
Nikawaambia na mimi lazima wazazi wangu wawepo. Mr akasema haoni haja ya ndugu zangu. Kikao kkaandaliwa. Kikao kikakaa. Ndoa inavunjwa. Yani wala hawaoni aibu. Nikkawaza nikapata jibu kwamba hawa hawakuwa wananihitaji. Na wamepata sababu.
Tulikaa kikao. Kisha nikaambiwa nifungashe nguo zangu. Nikafungasha. Na nikaambiwa watoto nitapewa ila ni marufuku kutoka nao out bila idhini ya mr. Na kila ijumaa waende kwa mama. Yani kwa mama mkwe wangu. Na niwachukue jumapili jioni.
Nikakubali tu.
Nikafungasha nguo zangu. Na za wanangu.
Siku ya kwanza ikapita. Ya pili na ya tatu. Nafungasha tuu.
************
Nimeshafungasha . Nikakumbuka ahaaa .Irene Mbowe yupo Dar.
Ndo sasa ananiambia juu ya Nauli nk.
Ninashida na pesa napaswa kuhama nk. Lakini nikaona well. Nimpe tu hiyo.
Sasa nafika. Nakaa naye na ananiambia kwamba kashapata ticket. Na tuongeee.
Namuelezea mpaka swala la mimi Kufungasha.
Da Irene akaniambia kitu.
Akaniambia ,
Katika nyakati ngumu na za taabu ndoani ni kwa wale ambao wameolewa na wanaume ambao hawahitaji WASAIDIZI.
Mume hakuwa anataka msaidizi.Ila mke tu wa Kumdinya. Na ndio maana unaona haya yanatokea.
Na sio yeye peke yake tuu. Wako wanaume wa aina hii wengi mnoo. Na si mmoja. Wako wengi. Ambao
1. Hawataki wake zao wawe na pesa.
2. Hawataki wake zao wafanye vitu kwenye familia nk.
3. Hawataki wake zao wasome nk.
Na ndio maana unaona issue ya gari imemshtua.
Japo umekosea sana kutomshirikisha. Lakini kama angekuwa ni mume aliyeoa msaidizi angekuonya. Na yangeisha. Ila kwa vile sio wa hivyo ndo maana unaona gari imekuwa tatizo mpaka anataka uache kazi. Uuze gari na sasa uondoke.

Sasa nataka kukushauri.... Da Irene aliongezea
Alikuwa anaandika kwenye Diary. Sikuwa naelewa anaandika nini. Lakini ni kama alikuwa anachora.
Kisha akaniambia...
NINAKUSHAURI JAMBO AMBALO LITAKUSAIDIA.
1. Kuamua kuolewa maana yake ni kukomaa. Yani ndoa ni safari. Ni kama dereva anayesafiri njia ambayo haifahamu. Na hujipanga kwa vitu muhimu kuhakiki gari yake inajitosheleza.

2. Lakini pia hata kama dereva anaijua njia vyema lazima ajipange tu pia.
Hali kadhalika kwa mke. Iwe ndoa ni nzuri ama la lazima mke awe amejipanga. Na ndio maana unaona unapata shida sasa hivi. Ni kwa vile hukujipanga. Tatizo sio kupata pancha. Tatizo una spare tairi?
Anayepata pancha kama ana spare tairi wala haimsumbui. Ila kama hana tairi halooo...
Sasa huyu ndo wewe na ndio maana umefungasha.
Labda nikuulize... UNAENDA WAPI KWA MFUNGASHO HUO?
Da Irene aliniuliza tena kwa kubetua midomo. Na namna alivyoniuliza ni kama mwanamke wa kiswahili anayepashana....
Nikimtazama na akanitazama..
Akaongeza.
Bibie... mfungasho huo wenda wapi?

Niliguna. Mh.. nikamwambia kupangisha.
Da Irene nitapangisha. Maisha yaende. Yani...
Napangisha.
Akaniambia... Sawa utapangisha.
Ila nakuhakikishia... utapata hasara kibao.
Na hasara ya kwanza itakayo kuuma maishani mwako ni WANAO.
Hao ambao ijumaa mpaka jumapili watakuwa kwa Bibi. Bibi ambaye hajui kuonya. Kufundisha. Kusaidia.. nina mashaka.
Hao wanao wataoandikiziwa mambo ambayo haloo kuyatoa itakugharimu zaidi ya MFUNGASHO.
Unajua ijumaa mpaka jumapili wataambiwa nini?watafundishwa nini?
Umeliwaza hilo?

Mh...Akili yangu ikafunguka vaaap.... nikawa kama nimezibuliwa.
Nikakumbuka mtoto wa shemeji yangu mmoja alivyoharibika. Yani shemeji aliacha mke. Akaoa mwanamke mwingine. Akaacha mtoto wa darasa la saba na darasa la nne.
Wa darasa la sava akakaa na bibi. Lakini huyo mtoto akawa hamsalimii mama yake. Mtoto wa miaka 15 akiwa form 2 anamuita mama yake Malaya na mchawi.
Siku ya graduation yake ya std seven mtoto hataki keki kutoka kwa mama yake. Anamwamvia mama yake i dont trust you.
Mama alilia sana. Mpaka kesho anaumia.
Nilikumbuka tu haraka.
Nikanza kulia sana.
Nikawaza nirakaaje na mume kwa mateso hayo. Nilia sana.

Da Irene akanikumbatia. Akaniambia...Be strong. Wewe ni wa Thamani sana. Dawa ya Mwanaume ambaye hajaoa Msaidizi anatakiwa azione Thamani zako.
Na ataonaje Thamani zako lazima ufanye haya.


ITAENDELEA....
 
hii ndoa kiukweli haina tena furaha bali ni karaha mwanaume huyu tuseme bado ana akili za kitoto kweli mke wako mwenyew unashindwa kumnunulia usafiri unaenda mnunulia mdogo wako tena wa kike upendo wa kindugu upo but kwa hayo mkaka anayomfanyia mkewe puuu huo ni unafki mtupu mm binafsi mtu kama huyo ata kuishi nae ni shida sana huyo dada akae pembeni kwa mda ila aweze kumpa huyo kaka ajitambue na ajue amekosea wapi bila hivyo hakuna kitakachobadilika sana sana ni kutesena tu moyo
 
Back
Top Bottom