Jumong S
JF-Expert Member
- Jul 3, 2013
- 7,427
- 10,749
Habari,
Kuna Bwana mmoja anaitwa Sauli, ni mtu wangu wa karibu. Tumeshughurikia pensheni yake as kastaafu shirika la Posta na kalipwa Milioni 70. Sasa game iko hivi, kuna tapeli mmoja dreva (inasemekana kashamliza mfanya biashara mmoja Tsh 80M na mwingine takribani 50M), kashamuweka king huyu mzee wetu. Huyu dreva anachofanya anasema anawatafutia watu fursa za biashara na anawaunganisha na shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNDP kwa kutafuta watu wenye mitaji watakaofanya biashara za misitu. Huyu dreva anakupa mipango kabambe na anakuunganisha na mapadre, maaskofu, mashehe au wachungaji (hawa huwa ni fake) ambao husema nao wanafanya biashara hizi. Sasa siku ya siku utashangaa hao wachungaji fake wanakuja kwako au mnakutana hotelini huku wamevaa mavazi ya kichungaji mainly Roman Color shirts au nguo za kiustaadhi na wanakupa mipango mizuri ya biashara. Wanahakikisha unakuwa interested na watakuomba uchangie mf gharama ya wao kukaa hoteli, mafuta ya gari n.k (kumbe ndo watapeliwa hivyo).
Sasa mtaendelea kuwa na mawasilino huku wakitumia vifungu vya Biblia/Kurani uwachangie karibu kila huduma. Siku nyingine huchagua msitu wa mbali na kwako na kumuagiza huyo dreva muende ukauone then ushughurikie leseni ya umiliki. Sasa hapo penye leseni utaandaliwa watu wa ardhi/misitu fake na utalipia leseni fake let say ya 25M, utalipia usafiri, gharama za upimaji n.k kumbe msitu wenyewe hauuzwi ni mali ya serikari.
Siku nyingine itapangwa trip ya kupeleka hivyo viambatanisho vya Misitu unayomiliki huko Dar, Arusha, Mwanza, Kampala, Nairobi etc kwenye ofisi ya wawakilishi wa UNDP. Kumbuka kila gharama unalipia wewe, huko sasa ndo unaenda kutapeliwa mpaka ndala, unakuja kustuka pensheni yooote uliyoisotea kwa miaka dahari inaliwa na wasio na uchungu nayo.........
Ndugu yangu,
Utapeli ni taaluma, wizi ni ubunifu makini na hawa watu ni wajanja na hubuni mbinu nyingi sana kuibia watu. Wanaofanya haya wakati mwingine ni watu tunaowafahamu, kwa kujua ama kutojua. Wastaafu wengi wamelizwa kwa njia hizi au nyingine. Muonye ndugu yako, muelekeze ajikite ktk biashara halali, asitafute pesa za haraka haraka. Pesa hutafutwa kwa jasho na si kwa njia za mkato. Pensheni imefarakanisha wastaafu wengi na familia zao kwa kuingia ktk biashara za magumashi zisizo na faida na zilizojaa utapeli. Pole kwa waliolizwa. Mzee huyu tunatafuta namna ya kumuokoa ila ndo hivyo keshalizwa, hivi sasa hata pesa za kununulia wanzuki au mbege huku kwetu Katesh hana, anatia huruma na familia yake imesambaratika.
Waweza ongezea utapeli mwingine unaowakumba wastaafu, ili tujiepuke nao.
Wasalaam....