Mwenye kufahamu: Jeshi la wokovu

uzeebusara

JF-Expert Member
Apr 15, 2013
657
514
Habari wana JF,

Naomba kujuzwa zaidi juu ya hili jeshi la wokovu 'salvation army' lipo pale JKT Mgulani, Kurasini karibu na taa za kuongoza magari za njia panda ya Uhasibu na kuelekea Bandarini.

Hili jeshi nalo ni kama haya ya JWTZ, JKT, MGAMBO nk au tofauti. Nalo kazi zake zipi au lilianzishwa na serikali kwa malengo gani? Sijawahi kusikia wanatangaza nafasi za kujiunga.

Kwa wenye ufahamu zaidi.Nimevutiwa nalo.

Wasalam
 
Aisee kwani hii nchi watu wa madhehebu ya dini yanaruhusiwa kuwa na vyombo vya usalama kama jeshi, polisi nk?
 
Mwaka 1865 Bibi Catherine na mume wake William Booth waliamua kuokoa masikini kutoka kwenye maradhi na njaa kwa kuwaketea neno la Mungu pamoja na misaada mingine. Walianzisha Jeshi la Wokovu huko London. Jeshi la Wokovu ni jumuia ya misaada ya kimataifa sasa hivi na lina wafuasi takribani million 1.5 duniani kote. Bwana Booth alikuwa Methodist Christians.

Jeshi la Wokovu linasaidia wahanga wasio na makazi baada ya majanga kama tetemeko la ardhi au mafuriko. Kiini hasa cha Jeshi ni kueneza Ukrito kwa njia ya misaada na elimu. Tangia mwanzilishi wake aanzishe dhana ya Jeshi katika mapambano, dhana hiyo inaendelezwa mpaka leo hii.
 
Mada hii ilishajadiliwa hapa sana!!! Lile sio jeshi kama majeshi ya nchi yalivyo ! Ni taasisi flan ndani ya kanisa katoliki inajihusisha na kusaidia makundi maalumu kwa mfano wanayo shule na kituo cha kuwasaidia walemavu na yatima!! Neno jeshi lisilete wasiwasi.

Duc In Altum.
 
Una uhakika ni ndani ya kanisa Katoliki?
 
Mada hii ilishajadiliwa hapa sana!!! Lile sio jeshi kama majeshi ya nchi yalivyo ! Ni taasisi flan ndani ya kanisa katoliki inajihusisha na kusaidia makundi maalumu kwa mfano wanayo shule na kituo cha kuwasaidia walemavu na yatima!! Neno jeshi lisilete wasiwasi.

Duc In Altum.
Kanisa katoliki!!!!! una uhakika unacho KINENA au????????
 
Mchungaji Almarhum Mtikila alikuwa kiongozi wa hili dhehebu kama sikosei. Halina uhusiano na Kanisa Katoliki. Misingi ya kanisa hili imekaa kipentecost sana
 
Jeshi la wokovu ni dhehebu kamili la kikristo linalotitegemea na si kweli kuwa lipo ndani ya RC. Hawa wandugu huvaa kama askari, kutegemea na cheo!
 
Back
Top Bottom