Mwenye kuelewa juu ya AIM GLOBAL

Mwenye kuelewa juu ya AIM GLOBAL

Hamis Zmc

Member
Joined
Aug 25, 2016
Posts
48
Reaction score
27
Hello, napenda kuuliza kwa mtu mwenye kuelewa juu ya AIM GLOBAL Hawa watu ni kweli wanaweza kukusaidia kupata kipato cha ziada kupitia biashara za bidhaa zao au ni janja janja?
 
Hello, napenda kuuliza kwq mtu mwenye kuelewa juu ya AIM GLOBAL Hawa watu ni kweli wanaweza kukusaidia kupata kipato cha ziada kupitia biashara za bidhaa zao au ni janja janja?
Kimbiaaaaaaaaaaaaaaaaaa

Utalia sasa hivi
 
upumbavu wenu sijuu utaishw lini. haya Aim global ni sawa na Qnet
Acha upuuzi kalime
 
Ase yani umenikubusha Bali nishawahi kuhudhuria semina yao nikatoka nduki kifupi skuwa na imani nao
 
Hello, napenda kuuliza kwa mtu mwenye kuelewa juu ya AIM GLOBAL Hawa watu ni kweli wanaweza kukusaidia kupata kipato cha ziada kupitia biashara za bidhaa zao au ni janja janja?
Ujinga wa watanzania bado ni mkubwa sana.

Elimu elimu elimu.
 
Itakulipa ukiuza zile products zao. Kipengele kitakuja nani atanunua? Package unauziwa laki 5 madawa yenyewe + coffee zile ni ngumu kutuuzia watz sie.

Nahisi kutakuwa na hizo bonuse za ukimleta A nae akawaleta B na C wewe Z utapata kamisheni ya laki 3. Upuuzi mtupu tu
 
Wakuu hivi huu uzezeta mnautoaga wapi ? daah AIM GLOBAL NI kama QNET Mtaumia sasa ivi
 
Si tulishawahi kualikwa kwenye semina yao pale mwenge. Tulipofika pale tukashangaa namna watu walivyokua wanafake maisha, kila mtu amevaa suti wengine na glass amchoni

Speech imeanza, tunategemea watu waanze kujadili namna global yao inavyofanya kazi wao wanajikita kuelezea magari na pesa wanazomiliki

Kuna kapambe kamoja walikapa u-mc sijui walikaahidi watakalipa shingapi maana kalikua kanawapaisha kinoma.

Jamaa akatuambia kua anamiaka 27 kaacha chuo kwa kazi hiyo now anamiliki utajiri wa milion 175 na ana gari ya kifahari ambayo inaogopwa na watu kwa ulaji wake wa mafuta

Akasema lengo la hii biashara ni kuwainua vijana wasiojiweza waweze nufaika

Akatupa mchanganuo wa upataji pesa nikaona haimake sense, mara sijui utoe laki 5 uwape wao watakupa package yenye dawa kisha watakufungulia account yenye kianzio cha 30,000 halafu sijui uanze kutengeneza pair kwa ku-invite wenzako. The more you invite tho more you earn

Nikawauliza mnauhakika hii ishu ina hela kama ambavyo nyinyi mnaipigia promo hapa? Wakasema ndiyo

Nikawauliza kwa msisitizo tena mlimaanisha mliposema lengo kuu la hii biahara ni kusapoti vijana? Wakasema ndiyo

Nikasema sawa, kutokana na wewe hapo mdau ulivyotuelezea kua umefanikiwa na una miliki utajiri mkubwa basi laki 5 kwako sio ishu hivyo tunatumaini wewe ndiye utakua nuru ya sisi kwa kuanza kutupa sapoti ya kutukopesha hiyo laki 5 ya kuanzia.

Jamaa alikua anatabasamu tabasamu na ucheshi wa hapa na pale lakini baada ya hilo swali nikaanza kuona mabadiliko taratibu huku jamaa akionekana kutofurahishwa na swali langu

Nikaendelea kukazia, nikamuambia kwenye hiyo laki tano utayotukopesha tutaanza kutengeneza pair ambayo iko chini ya management yako na account zetu zitakua chini yako ili pesa ikiingia tu utakua unaikata huko huko juu kulipa deni lako

Hamuwezi mkawa mnasema mnalengo la kuwasaidia vijana kwa kuwatoza 500,000 ya kujiendeleza wakati uhalisia mnaujua kwa mtaani mtu ambaye anaweza ku afford laki 5 huwezi kumuongelea kama ni mtu asiyejiweza wakati mtaani humo humo kuna watu wapo hawana hata senti

Nikaskia brother tunashukuru kwa swali lako ila swali lako utajibiwa privately baada ya kikao kuisha na aliye kualika
 
Boss ungejibu swali ungeonekana muungwana
 
mkuu unahaki yakuniambia hivyo , kusema kweli reaction nlokuja nayo ni kutokana na namna watu walivyoumia QNET na pia inatokana na namna tulivyokuwa tunawaambia kistaarabu na hawakutaka kusikiliza, nisamehe boss , ila naomba nikwambie kitu Achana na Aim global fanya kazi zingine mkuu utakuja kunikbuka siku moja... Namna biashara ya aim global wanavyoiendesha haina tofauti na Qnet...Watakuliza mkuu.
 
Hello, napenda kuuliza kwa mtu mwenye kuelewa juu ya AIM GLOBAL Hawa watu ni kweli wanaweza kukusaidia kupata kipato cha ziada kupitia biashara za bidhaa zao au ni janja janja?

Naona wamewaanza first year ili wawakamue boom! Utalia, Uta Sup, mwisho usipokaa sawa uta disco sababu ya stress za Pyramid Scheme zisizo na tija. Kimbia mbali sana na hao watu.
 
Heshima yako Boss
mkuu unahaki yakuniambia hivyo , kusema kweli reaction nlokuja nayo ni kutokana na namna watu walivyoumia QNET na pia inatokana na namna tulivyokuwa tunawaambia kistaarabu na hawakutaka kusikiliza, nisamehe boss , ila naomba nikwambie kitu Achana na Aim global fanya kazi zingine mkuu utakuja kunikbuka siku moja... Namna biashara ya aim global wanavyoiendesha haina tofauti na Qnet...Watakuliza mkuu.
 
Itakulipa ukiuza zile products zao. Kipengele kitakuja nani atanunua? Package unauziwa laki 5 madawa yenyewe + coffee zile ni ngumu kutuuzia watz sie.

Nahisi kutakuwa na hizo bonuse za ukimleta A nae akawaleta B na C wewe Z utapata kamisheni ya laki 3. Upuuzi mtupu tu
Heshima yako🙏
 
Back
Top Bottom