Mwenge uzimwe Butiama

Mwenge uzimwe Butiama

Congo

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2008
Posts
2,079
Reaction score
2,334
Kama serikali imeamua tarehe 14.10 kila mwaka ndio sio ya kuzima mwenge ambayo pia ni siku ya Nyerere. Basi mwenge huo uwe unazimwa Butiama kila mwaka.

Unaweza kuwashwa popote lakini uzimwe Butiama. Sii vema sii vema kufanya shughuli ya kumbukumbu ya Nyerere mbali kabisa na kaburi lake. Si busara familia yake kusafiri kuufuata mwenge ulipo ili kufanya kumbukumbu.

Butiama ipo, kaburi lake lipo. Poa ni kuienzi shughuli hiyo alipozaliwa kila mwaka.
 
Dj mbowe alisema siku chadema ikishika madaraka mwenge utakimbizwa mbio moja tu,kutoka ikulu kwenda makumbusho ya taifa ukahifadhiwe.
Yupo sahihi, mwenge kukimbizwa una madhara hasi kuliko chanya, kwenye mbio za mwenge wanazaliwa watoto useless kama akina Napengwa.
 
Mwenge is an old school politics, ni aibu kwa taifa kuendelea kukimbizwa in the modern globalized world!
 
Dj mbowe alisema siku chadema ikishika madaraka mwenge utakimbizwa mbio moja tu, kutoka ikulu kwenda makumbusho ya taifa ukahifadhiwe.
Ht mimi ntashiriki mbio hizo na bila shaka zitakuwa ni za kihistoria
 
Kama serikali imeamua tarehe 14.10 kila mwaka ndio sio ya kuzima mwenge ambayo pia ni siku ya Nyerere. Basi mwenge huo uwe unazimwa Butiama kila mwaka.

Unaweza kuwashwa popote lakini uzimwe Butiama. Sii vema sii vema kufanya shughuli ya kumbukumbu ya Nyerere mbali kabisa na kaburi lake. Si busara familia yake kusafiri kuufuata mwenge ulipo ili kufanya kumbukumbu.

Butiama ipo, kaburi lake lipo. Poa ni kuienzi shughuli hiyo alipozaliwa kila mwaka.
Ngoja kwanza tukauzime Pemba na baada ya hapo kwa Steve Nyerere(sic) kisha iwe Butiama Mwitongo.
 
Julius Nyerere ni mtoto wa Chief Burito wa Wazanaki kijana huyu alizaliwa 13 mwezi wa 4 mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama. Mimi nafikiri ni vyema siku ya kumbukumbu ya maisha ya Mwl. Nyerere ingalikuwa ni siku aliyozaliwa badala ya ile aliyokufa.

Kama tarehe aliyozaliwa inafahamika kuwa ni 13 Aprili, basi adhmisho la kumbukumbu yake ingalikuwa ni siku hii ya furaha ya kuja kwa hapa duniani.

Pengine nakosa mantiki ya kulchagua siku ya tarehe 14 Octoba. Pengine wajuvi wa mambo ili kunipa elimu zaidi. Ndani ya chama alichokiasisi tunaona wakisherekea siku ya tarehe 5 Februari kila mwaka, kwa kuwa katika siku kama hii mwaka 1977 ndipo kilipozaliwa.

Mimi sijui ni hesabu gani zimetumika kwenda kinyume na kanuni hii ya ujio wa CCM.
 
Kama serikali imeamua tarehe 14.10 kila mwaka ndio sio ya kuzima mwenge ambayo pia ni siku ya Nyerere. Basi mwenge huo uwe unazimwa Butiama kila mwaka.

Unaweza kuwashwa popote lakini uzimwe Butiama. Sii vema sii vema kufanya shughuli ya kumbukumbu ya Nyerere mbali kabisa na kaburi lake. Si busara familia yake kusafiri kuufuata mwenge ulipo ili kufanya kumbukumbu.

Butiama ipo, kaburi lake lipo. Poa ni kuienzi shughuli hiyo alipozaliwa kila mwaka.
Ningekuwa mimi ningejiuliza huu mwenge unaendena na mazingira yaliyopo hivi sasa? Je Malengo ya kuanzishwa kwake ( tutawasha Mwenge na kuuweka mlima Kilimanjaro ili umulike hata nje ya mipaka yetu, kuleta tumaini pasipokuwa na tumaini, Upendo Penye chuki na hshima ambapo pamejaa dharau) ikiwa kama kweli tunayaishi na kuyaenzi haya, sina shida na siku hiii kufanyika sio Butiama tu bali kokote ambako mwenge umefanikiiwa.

Malengo ya mwenge kama nilivyoyaeleza hapo juu, bado yako yanaishi na kustahili zaidi leo kuliko ilivyokuwa hapo jana na ikiwezekana tuanzishe "mienge" zaidi na ambayo itawalenga zaidi watawala wetu, badala ya kuuuimbiza nchi nzima na kuzinduia inayoitwa Miradi( sijui hili lilitoka wapi).

Kuhusu kusafiri kwenda kushiriki siku hii kusikokuwa na kaburi, hili ni janga ambalo tunalo, alisema mwanafalsafa mmoja "Nikifariki usije kaburini kwangu kunikumbuka, ninatakiwa kuacha alama ambazo popote zitaonekana".

Nikuache na swali hili, hawa watalawa waliokusanyika huko Manyara leo wanamuenzi nyerere au wanaishi malengo ya Mwenge?
 
Back
Top Bottom