Mwenendo wa Wenye Ulemavu Nchini Tanzania

Admin1988

JF-Expert Member
Mar 30, 2017
1,603
1,835
Habari zenu wakuu, Niswachoshe naandika kwa kifupi Saana, Wahusi wafaniye Kazi, au Mood wakiona Uzi haufai waufute.
""Binafsi sina Ulemavu wala ndugu Mlemavu wala KUHITAJI NAFASI huko nitako pasema""

Elimu Maalum Nchini ilianzishwa miaka ya 1960's na Watu wa Nje ya Tanzania hasa Kanisa Katoliki na Anglicana na Baadae FPCT (Rejea Shule ya Tabora Viziwi, Shule ya Wasioona Furaha Tabora na Shule ya Buigiri Blind)

Baada ya Hapo Serikali ika jitutumia kuwa kuendesha shule kadhaa na kuanzisha Chuo cha Ualimu Patandi Arusha Ambayo awali ilikiwa MIDDLE SCHOOL kwa kuhamisha kitengo cha Elimu Maalum kilicho kuwa Tabora Teachers' College mwanzoni mwa miaka ya 1990's

Ndipo wataalamu wakaanzishwa kuzalishwa (Waalimu wa Elimu Maalumu), na Serikali kuendelea na Harakati Japo kwa kusua sua miaka ya 2004 Waka Tengeneza SERA YA WENYE ULEMAVU NCHINI TANZANIA,
Ambayo Utekelezaji wake Bado ni kizungumkuti,

Ndipo vika anzihwa vyuo/Department za Elimu Maluum kama vile UDOM, UDSM, OUT, SEKOMU na AMUCTA ambavyo kimsingi ndivyo vilivyo zalisha Wataalmu wa Elimu Maalumu Nchini Kuanzia miaka hii hii ya 2010's SEKOMU kulingana na Vurugu zake na Figisu Figisu KIKAFUNGWA HADI HIVI LEO, but kina.Mchango Mkubwa Vijan wengi wamo Wizarani, T.I.E na Hata Baraza la Mitihani (Nawafahamu kwa Majina) ilihali chuo chao kime kufa kifo kitakatifu....

Baadae kidogo zikaanzishwa Idara na za Wenye Ulemavu Ambazo hazina Watendaji na wenye Psycho-social wa Ulemavu, mfano; KWA WAZIRI MKUU KUNA kurugenzi ya Wenye Ulemavu inayo simamiwa na JACOB huyu ni Albino na Naibu waziri na Joyce Ndalichako nk,
But watendaji wa Wenye Ulemavu ni Watu wa Sosialojia na Medical Attendant (Kwa.mujibu wa Mkurugenzi MWAIJANDE) Ambao Kimsingi hawana Taaluma ya Wenye Ulemavu, na Saikolojia ya Uhitaji kwa Wenye Ulemavu, nk

Baadae kidogo Miaka hii ya 2010's Wizara ya Elimu Tanzania ikaanzisha Unit ya Wenye Ulemavu chini ya Mtaluma Mkuu nchini (Kamishina wa Elimu)

Unit Hii, ina Madudu ya kutosha na Vichekesho kila Leo kuanzia kwa Mkurugenzi wake Dr. MATONYA, Huyu ni Empty Box, haelewi chochote kuhusiana na Ulemavu, japo ana mtoto wake wa Kuzaa mwenye Ulemavu wa Akili na Usonji, Yeye na Staff yake hawezi kabisa kutetea HALI YA ULEMAVU NCHINI, Vijana alio nao wakina Henerico, Chamshama (hawa ni zao la SEKOMU), Dr Wakulu (huyu ni zao la PATANDI hana kitu na Certificate ya Elimu maalum ya Patandi Na digrii za Udsm zisizo za Elimu Maalum) nk
Hawawezi chochote na HAWAJIAMNI.

Kwa sasa TAASISI YA ELIMU TANZANIA (T.I.E) chini la Agizo na Rais na harakati za wadau wengine wako kwenye mchakato wa Kuandaa mitaala ya Elimu japo Ime gubikwa na Wahuni ambao hawataki Iendelee,
T.I.E chini ya Dr. Aneth Komba, imekuwa ikiita wadau watengeneze Adapted Curriculum ya wenye Ulemavu yaa MTAALA REKEBIFU KWA WENYE ULEMAVU lakin vikao hivyo haviishi kwa Amani, huko Morogoro, hata jana tu 11/3/2023 Wako Ukumbi Flani, Hawa Taki Wana wapinga Wataalamu wakina Dr. Mnyanyi, Dr. Mkama, Kabora DC nk,
Kwani wao ndio wataalamu lakn HAWAWAZIKILIZI.

Wakampgia Dr. Matonya Nae HAJUI wakampigia Mkuu wa Patandi LUCIAN ERNEO SEGESELA naye hana uelewa, Hivyo wakashindwa kufikia UELEWA WA PAMOJA ili vijana wetu wapate Elimu Maalumu na Kuzalisha Wataalamu wengi, Kupinga huku hii ni Mara ya Pili Serikali ina poteza gharama za Fedha watu wana ishia KUBISHANA na kulipwa posho na wanaondoka bila kutimiza kusudi lilo wapeleka,

Ninayo Mengi ila sihitaji kuwachosha, naomba yafuatayo yatekelezwe, SERIKALI NA WATU WA USALAMA CHUKUENI HAYA
1. Hiyo Adapted Curriculum wanayo Andaa morogoro IKAMILIKE,

2. Unit ya Elimu Maalumu Wizara ya Elimu WAWEPO WATAALUMU na sio Hao wakina Matonya nk waliopo kwa Sasa HWAWEZI,

3. Tekelezeni Muongozo wa Elimu kwa Wenye Ulemavu Nchini wa Mwaka 2019 kwa kumuweka Mkuu Patandi, Kabanga na Mpwapwa mwenye TAALUMA YA WENYE ULEMAVU,

4. Kurugenzi ya Ofisi ya Waziri Mkuu Wenye Ulemavu, WEKENI WATAALAMU WA WENYE ULEMAVU na sio hao waliopo kwa sasa wekeni wapya washirikiane,

5. Patandi chuo cha Ualimu Kipewe wakufunzi wataalamu wa Wenye Ulemavu kwa Kuondoa hao waliopo sasa WENYE CERTIFICATE ZA ULEMAVU na Digrii zingine kama vile Maendeleo ya Jamii nk HALAFU ANAFUNDISHA WAALIMU Ambao serikali inaajiri,

6. Vyuo vya Mpwapwa TC na Kabanga TC vipekewe waalimu wa Elimu Maalumu kwani Mpaka sasa Mfano mpwapwa TC kuna wanachuo zaidi ya 220 na mwalimu mmoja mwenye TAALUMA YA WLIMU MAALU afundishw Course zaidi ya 8 huo ni Ubabaishaji, na Kambanga pia kuna aanachuo zaidi ya 150 na Mwalimu Mmoja haiwezekani, (NA WANACHUO WOTE HAO MWEZI WA TANO MWAKANI WANAMALIZA ELIMU YA UALIMU PASIPO KUWA NA.MAARIFA YA KUTOSHA)

7. VETA nchini Waanzishe Unit au Kurugenzi ya Wenye Ulemavu kwani hawana Morogoro MVTC ambako ndiko wanako zalisha waalimu wa VETA Nchini na Makao Makuu wawe na Wataalamu kwani, WENYE ULEMAVU WENGI WANASHINDWA KUENDELEA NA TAALUMA ila wana weza elimunya UFUNDI sasa wawapo huko wanakosa Msaada VETA

Na kama ikiwezekana Serikali Ijenge Chuo kimoja cha Mfano cha VETA kwa wenye Ulemavu au kuhuisha chuo chochote kitekeleze Kozi za Wenye Ulemavu.

Ninayo Mengi, lakina hayo Mambo Saba, naomba Serikali, Watu wa Usalama na Wadau mbali mbali yafanyieni kazi, haraka iwezekanavyo ili KUSAIDIA WENYE ULEMAVU.

ANAYEHITAJI USHAHIDI AJE PM
Asanteni
 
Back
Top Bottom