Mwendokasi katika Mtandao wa Yahoo

kabla ya vita shilingi haikupitwa sana na dola zilikuwa karibu sawa, baada ya vita shilingi ilishuka sana ikawa inflated kwa kiwango cha 5sh kwa dola moja. kitendo hicho ndio moja ya sababu ya kuua uchumi na viwanda kwa kipindi hicho.
Huo ni mwaka gani? Ninavyokumbuka mimi dollar ilikuwa shillingi tano kabla ya vita na sio baada ya vita.
 
Huo ni mwaka gani? Ninavyokumbuka mimi dollar ilikuwa shillingi tano kabla ya vita na sio baada ya vita.
mkuu watanzania tunaongea siasa muda wote usichukulie vinavyoandikwa humu kwa umakini wengi waliomo wamezaliwa 2000+,
1976 dola moja ilishavuka tsh 8 ya bongo.
 
mkuu watanzania tunaongea siasa muda wote usichukulie vinavyoandikwa humu kwa umakini wengi waliomo wamezaliwa 2000+,
1976 dola moja ilishavuka tsh 8 ya bongo.
Naelewa kuna watoto wengi sana humu (watoto wetu). Lakini ndio hivyo wanatuchangamsha akili na sio vibaya kulumbana. Mwaka 1974 tayari nilikuwa mfanyakazi pale kitega uchumi gorofa ya nne (National Insurance, Motor Underwriting Dept. chini ya bosi Mwabulambo). Kwa hiyo niongeacho sio cha kusimuliwa na mjomba bali nimekiishi nikiwa na akili timamu.
 
Wow So nice, Tanzania hiyo ya mabadiliko safi sana Magufuli Go. Ndio Daladala inatokana na Dollar- Wakati huo Nauli ilikuwa Ths 5. Ambayo ilikuwa equivalent to 1USD.
 
Yaani waliozaliwa 1980s onwards huwa wabishi mnooooo! Ukweli ni kuwa TSH 5 ilikuwa sawasawa na 1 USD ndio maana ya kuita Daladala. Yaani Vijana ukiwaambia Zamzni magari yalikuwa yanarudi nyuma bila kupiga honi watakubishia mpaka kukesha!
 
kabla ya vita shilingi haikupitwa sana na dola zilikuwa karibu sawa, baada ya vita shilingi ilishuka sana ikawa inflated kwa kiwango cha 5sh kwa dola moja. kitendo hicho ndio moja ya sababu ya kuua uchumi na viwanda kwa kipindi hicho.
Hebu acha ubishi usio na tija. Hao wanaosema walikuwepo wakati huo sasa ubishi ni wa nini?!?!?!?
 
....sawa,lakini tuambie kwanini shiling tano iliitwa dala, w ndo umemuelewa vibaya,
 
Dollar kipindi hicho thamani yake ni shillings tano yaani dola thamani yake ikaitwa dala dala kwa mnasaba Wa shilingi tano kwa roti moja
 
Yaani waliozaliwa 1980s onwards huwa wabishi mnooooo! Ukweli ni kuwa TSH 5 ilikuwa sawasawa na 1 USD ndio maana ya kuita Daladala. Yaani Vijana ukiwaambia Zamzni magari yalikuwa yanarudi nyuma bila kupiga honi watakubishia mpaka kukesha!

Nadhani ndiyo maana hata walimu wanapata taabu sana mashuleni,
 
Haya maisha sijui tulikosea wapi sisi.. Dollar 1 sawa na sh 5 ya kibongo.. Sasa imepanda maradafu.. Sio maradufu tena.

Ni kweli kabisa ukizingatia ni nchi yenye kila kitu - Ee Mungu tunusuru, wahenga walisema kosa mali pata akili😀
 
Hakuna kitu kinachozuka tu, bila kuwa na chanzo au sababu. Jambo la msingi ni kukubali kukosolewa unapokuwa umekosea. Hutapungukiwa na kitu, badala yake utaonekana muungwana. Wakati mwingine tunajifunza kutokana na makosa.

Umenena!! barikiwa
 
Najaribu kuunganisha dots kwa uelewa wangu dala lala ilimaanisha hiyo shilingi tano ambacho ndicho kiwango cha nauli kipindi hicho kama ilivyokuwa nchini kenya wakilipa shilingi tatu nauli wakaita matatuu ila hili la shilingi tano kuwa ilioriginate kutoka neno dollar hakuna ukweli watu tusipotoshane bure!! kama kitu hujui bora uulize upate ufafanuzi.
 
Safi, ndo kuumitangaza bongo huko, TTB waongee na hao jamaa vzr wawe wanarusha news za serengeti/zanzibar pia ili tuvute mkwanja
 
Nijuavyo ni jina tu limezuka kama mia tano kuitwa jero au mia kuitwa jiti elfu kuitwa buku,hivyo sina haja ya kumtafuta huyo jimmy chika wala jimmy choka
Hata nayo yana chimbuko. Jero ilitokana na Pajero.
 
kabla ya vita shilingi haikupitwa sana na dola zilikuwa karibu sawa, baada ya vita shilingi ilishuka sana ikawa inflated kwa kiwango cha 5sh kwa dola moja. kitendo hicho ndio moja ya sababu ya kuua uchumi na viwanda kwa kipindi hicho.
Haijawahi kuwa hivyo. Kabla ya matatizo ya kiuchumi kwenye.miaka ya 1980 kulikuwa na sera ya fixed exchange rate. Dollar Karibu Sawa na Sh. 5 na Pound Sawa na Shillingi 20. Ikiwa na maana kuwa viwango vya kubadilisha fedha za kigeni vilibaki vile vile bila kujali hali ya uchumi/soko. Baada ya kuingia IMF na nduguye World Bank sera ikabadilishwa na kuwa floating exchange rate pamoja na Shillingi kushushwa thamani (devaluation). Huo ukawa mwanzo wa Shilingi kuporomoka Kila kukicha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…