''Mwendo Kasi wa Maigizo''

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Ni aibu ni aibu sana sisi kama taifa kuwa na aina ya viongoz ambao badala ya kukaa na kuumiza kichwa ili kutatua matatizo ya wananch ikiwemo na kutembelea maeneo mbalimbali zenye changamoto kwa wananchi lkn wao badala ya kufanya haya wamelazmika kufanya maigizo ili sisi tuwaone kuwa wana huruma na sisi wananchi.

KWANINI MA DC,RC WENGI WANAFANYA MAIGIZO KATIKA AWAMU HII?

Tumeshuhudia wateule wengi wa mh mtukufu wakifanya maigizo ili mh mtukufu awaone kuwa ni aina ya viongoz ambao ni wachapakaz wanaoendana na kasi yake na falsafa yake ya HAPA KAZI TU.

Matukio kama haya tumeyashuhudia yakiongezeka kila siku kwa hawa wateule na kuna wengne tumeshuhudia wakiangukia kwenye mitalu ya maji na lengo na madhumuni yao ni kulinda vibarua vyao na hili linaweza kuleta athari kubwa kwa sababu wengi wao watajikuta wakishindwa kufanya kaz ipasavyo ikiwa ni pamoja na kushindwa kuumiza kichwa kwa kubuni project mbalimbali ya kimaendeleo kwa maslah ya mlalahoi aliyeko huko vijijin kwa sababu wao muda mwingi wanautumia kufanya kazi ya KUIGIZA na kupost kwenye mitandao ili waonekane eti kisa MTUKUFU huwa anafuatilia kwa karibu matukio mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii.

Na kwa mfumo huu wa uongoz wa hawa wateuliwa wa mtukufu basi zitakuwa ni ndoto za KUSADIKIKA KWA NCHI HII YA MAZIWA NA ASALI KUWEZA KUPATA MAENDELEO NA KUONDOKA HAPA TULIPOKWAMA

Na viongoz wa aina hii wengi wao hawajiamn kama wanatosha kwenye hzo nafasi kwa kuwa hawana taaluma ya uongoz kwa sababu uteuz wao ulikuwa wa KISIASA TU na hawa mwisho wa siku uteuz wao ukitenguliwa wengne wanakufa kwa presha na wengne kulialia kwenye media na kulalama eti waonewe huruma eti kisa WAMETOKA FAMILIA duni.BADILIKENI

Ni mimi mlalahoi Mwanakijiji lugusi
mwanakijiji@gmail.com
 
Attachments

  • FB_IMG_1468545806955.jpg
    FB_IMG_1468545806955.jpg
    24.4 KB · Views: 30
Maigizo ni mengi tu, kama yule DC mmoja wa kule nyanda za juu kusini ambaye alikuwa akiwabeba mgongoni wananchi wa wilaya yake anaowangoza akiwavusha kwenye mto uliofurika maji kipindi kile cha mafuriko!!
 
Na yule wa kutokea Mkoa wa Kilimanjaro aliyejidondosha kwenye maji... maigizo ya Mwendokasi
 
Maigizo ni mengi tu, kama yule DC mmoja wa kule nyanda za juu kusini ambaye alikuwa akiwabeba mgongoni wananchi wa wilaya yake anaowangoza akiwavusha kwenye mto uliofurika maji kipindi kile cha mafuriko!!

Huyu ni wa ITV vile?
 
Back
Top Bottom