Mwendelezo wa Elimu za siri, Namba maumbo na ishara sehemu ya 1

Mwendelezo wa Elimu za siri, Namba maumbo na ishara sehemu ya 1

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
2,144
Reaction score
3,459
📚 MWENDELEZO WA ELIMU ZA SIRI 📚
NAMBA, MAUMBO NA ISHARA
sehemu ya 1️⃣


Kwa wiki tatu mfululizo tumekuwa tukijifunza Elimu ya Namba, tukiona jinsi namba zinavyobeba mitetemo, siri za maisha, na nguvu za roho. Lakini safari hii hatuaishii pale: namba peke yake hazitoshi.

Ili kuelewa lugha ya ulimwengu kwa kina, tunapaswa kuunganisha:

▪️Namba .....vibration na mtiririko wa maisha.

▪️Maumbo .... muundo wa nishati na nguvu zinavyopangwa.

▪️Ishara ..... alama na ujumbe wa roho kutoka ndoto, maono, na historia.

👉Kauli kuu ... Namba + Maumbo + Ishara = Lugha kamili ya Ulimwengu/universla language

Hii ndiyo sababu ndoto, maono, na ramani za kale zimetengenezwa kwa alama na mifano. Ukiunganisha hizi tatu, unapata ufahamu wa ndani wa roho, siri za maisha, na mwelekeo wa kweli wa ulimwengu.

Kwa maneno mengine, sasa tunaanza kuona chini ya uso wa mambo, kugundua mchoro wa kweli wa maisha na roho, si tu idadi au matukio. Huu ni mwanzo wa safari ya ndani ya roho kupitia elimu ya siri.

⚫ ELIMU YA ISHARA NA NGUVU ZAKE 📖

Nakupa Dondoo Kuu

▪️1. Kila ishara ni lugha ya ulimwengu wa roho
Kabla ya maneno na maandiko, ulimwengu uliwasiliana kwa alama na vibration.
Ndiyo maana mtu akiona ndoto mara nyingi huona alama (mfano nyoka, maji, mlango) kuliko kusikia sentensi ndefu. Ishara ndiyo lugha ya asili ya roho.

▪️2. Ishara ni daraja kati ya roho na mwili
Akili ya kibinadamu ina mipaka; haiwezi kushusha moja kwa moja taarifa za kiroho.
Roho inashusha ujumbe kupitia alama ambazo ubongo unaweza kuzitafsiri.
Mfano: ukiona namba fulani ikijirudia mara kwa mara (11:11, 7:7:7), hiyo si ajali ...ni roho inakutumia daraja la ishara.

▪️3. Nguvu ya ishara iko kwenye mtetemo wake
Kila umbo lina frequency yake.
mfano 👇

✝️ Msalaba = Namba 4 ikimaanisha uimara, misingi, dunia yenye pande nne.

⭕ Duara = umilele, cycle isiyo na mwanzo wala mwisho ...ishara ya Mungu wa milele.

🔺 Pembetatu = nguvu tatu kuu (mwili, nafsi, roho / Baba, Mwana, Rohomtakatifu) Trinity

Kadri unavyotumia ishara fulani, unajiunganisha na mtetemo wake.

▪️4. Ishara hufungua milango ya fahamu ya ndani
Kila mtu ana akili ya ndani (subconscious mind). Ishara zikiliwa na kuonekana mara kwa mara, zinaingia huko na kufungua nguvu zilizolala.

Mfano: ✡ Nyota ya pembe sita = mbingu ↔ dunia. Ukitazama mara nyingi hujifungulia daraja la ndani la kuunganisha vitu vya rohoni na vya kimwili.

▪️5. Kila dini na tamaduni hutumia ishara
Hakuna dini wala tamaduni isiyo na ishara — zote zinatambua kuwa ishara ni lugha ya ulimwengu wa roho.

Ukristo .... ✝️ Msalaba = daraja la kifo na uzima, ulimwengu wa chini na wa juu.

Uislamu ....🌙 Mwezi na ⭐ Nyota = mwongozo wa mwanga gizani, cycle ya roho.

Uhindu .... ॐ (Om) = sauti ya uumbaji, vibration ya mwanzo wa ulimwengu.

Misri ya kale .... 👁 Jicho la Horus = kinga, kuona yasiyoonekana, ulinzi wa kiroho.

👆Hizi zote si mapambo tu, bali codes za siri ambazo zimebeba frequency na ujumbe wa rohoni.

✍️ukweli ni kwamba,Ishara si mapambo bali ni lugha ya Mungu, lugha ya roho, na njia ya kuwasiliana na nafsi ya ndani.
Utakapozielewa na kuzitumia, utajua mambo makubwa kabla hayajatokea na utajifunza kuishi kwa mwongozo wa juu zaidi.

🟢 ISHARA KUU NA TAFASIRI ZAKE 📖

👉1. Duara ⭕

Umilele, ukamilifu, cycle isiyo na mwanzo wala mwisho.
Umoja wa roho, nafsi, na mwili.
Pia huwakilisha mzunguko wa maisha (kuzaliwa, kukua, kufa, kuzaliwa upya).
Ndio maana pete ya ndoa ni duara ... ishara ya ahadi isiyo na kikomo.

👉2. Mstari/ ─

Ni njia, mwendo na uelekeo.
Huwakilisha nidhamu, sheria na kusogea kutoka hatua moja kwenda nyingine.
Mstari ulionyooka = uthabiti na ukweli.
Mstari ulioinama au kuvunjika = changamoto, dhiki, au safari yenye mizunguko.

👉3. Msalaba ✝️ / +

Muunganiko wa juu...chini (mbingu na dunia) na kulia....kushoto (mambo ya wakati huu).
Namba 4, misingi ya dunia, pande nne, upepo wa dunia.
Ni ishara ya transition.... kupita hatua moja kwenda nyingine.

Ndiyo maana msalaba hutumika kwenye kaburi (kupita maisha ya kimwili ... ya kiroho).

👉4. Pembetatu 🔺 🔻

Ni ishara ya nguvu tatu (Trinity).

🔺 Pembetatu juu = mwanaume, chanya, moto, jua, kupanda.kwenye freemasonry huwakilishwa na bikali

🔻 Pembetatu chini = mwanamke, hasi, maji, mwezi, kupokea, tumbo la uzazi.katika masonic huwakilishwa na kipima pembe

Zikikutana 🔺+🔻= ✡ Nyota ya Daudi (umoja wa mbingu na dunia, chanya na hasi).

katika Alama kuu ya Masonic

bikali + kipima pembe vikeshikana, kisha katikati kuna herufi "G" kuwakilisha kizazi(Generation) kwani ulimwengu huundwa na Nguvu mbili,uwepo wa hizi nguvu ndio hufanya maisha kuwepo...umeelewa hapo❓

👉5. Spiral 🌀

Ukuaji, mageuzi, nguvu ya kuzunguka ya uhai.
Huwakilisha safari ya nafsi inayopanda ngazi kwa ngazi (ascension).
Ni ishara ya DNA ya mwanadamu na pia ya galaksi zinazozunguka.

Inatufundisha kuwa maisha si mstari wa moja kwa moja bali ni mizunguko inayopanda juu zaidi.

👉6. Jicho 👁

Ufahamu (consciousness), kuona yasiyoonekana.
Kinga ya kiroho, uwezo wa kutambua hatari kabla haijatokea.
Jicho la tatu (third eye) = kuona ukweli wa kiroho bila pazia.

🗣️Fumbo la Adamu na Hawa/Eva: walipokula tunda, walijua wako uchi .... walifunguliwa jicho la ndani, yaani waliona ukweli wa hali yao. hilo ni fumbo kuhusu kufungua jicho lako la 3 kupitia meditation,mfungo ,nguvu zako za mdani pale zinapopanda juu kuzunguka mti wa katikati/utiwa mgongo kwa mfano wa umbile la nyoka( nyoka wa bustani ni hizi nguvu ,mti ni uti wako wa mgongo,shamba ni mwili wako,kula tunda ni kufanya ibada ya meditation,kufunga,maombi n.k, hii mzungu hataki ufanye a.k.a bwana Mungu...umeelewa?

zamani liliitwa Jicho la Horus (Misri ya kale) = ulinzi, hekima na kuona ndani zaidi.

👉7. Nyota ⭐ / ✡

Safari ya nafsi, mwongozo wa nyota angani.

⭐ Nyota yenye pembe 5 = usawa wa nafsi, mwili, roho, akili na hisia.

✡ Nyota ya pembe 6 = muunganiko wa mbingu na dunia.

Nyota 7 = ngazi 7 za uumbaji, sayari 7 za jadi, na hatua 7 za mwanga.

Ndiyo maana manabii na wachawi wa kale walitumia nyota kwa ramani ya maisha.

👉8. Mwezi 🌙

Hisia, siri na subconscious mind.
Mwezi huongoza ndoto, maono na mizunguko ya kiroho.
Pia ni cycle ya uzazi (mwanamke ana mzunguko wa siku 28 kama mwezi).

Mwezi mpya = mwanzo mpya.

Mwezi mpevu (full moon) = ukamilifu na nguvu ya juu ya hisia.

👉9. Jua ☀️

Chanzo cha uhai, fahamu, mwanga na ubunifu.

Jua ndilo linalotoa maisha kwa mimea, wanyama na binadamu.
Pia huashiria uongozi, nguvu ya kiume na ubunifu wa ndani.

👇Ishara zingine za Jua:

🔘 Duara lenye nukta katikati (☉) ... ishara ya kale ya Jua. mfano kwenye uwanja wa mpira ile ni alama ya jua

Mandala za rangi ya manjano/zahabu pia mara nyingi huwakilisha jua.

👉10. Mandala

-Neno Mandala linatoka lugha ya Kisanskrit, likimaanisha “duara takatifu”.

-Ni mchoro wa duara wenye michoro ndani yake, unaowakilisha ramani ya roho na ulimwengu.

-Kila mandala hubeba vibration maalum kwa meditation au kuamsha fahamu.

Msamiati mwingine unaweza kutumia ni “Nguzo ya Duara” au “Alama ya Roho”. mfano nguzo za duara za kulia na kushoto kwenye kibaraza cha mahekalu,makanisa,majumba ya ibada n.k

Mfano 👉mandala yenye maua 8 huashiria usawa wa vipengele 8 vya maisha (mwili, roho, hisia, akili, jamii, kazi, mapumziko, uhusiano).

🔴 NGUVU ZA ISHARA.....

▪️Hulinda

Ishara zinaweza kuwa kama kinga.
Mfano: mtu akivaa msalaba, pete, au hirizi, si mapambo tu bali anaamini kuna nguvu ya kumlinda.
Ni kama kuweka alama ya “usinikaribie” kwa nguvu hasi.

▪️Hufungua akili ya tatu (Third Eye) 👁️
Ukijua ishara na kuzielewa, unafungua jicho la ndani linalokuonyesha zaidi ya kinachoonekana kwa macho.
Unaweza kuelewa ndoto zako, au kuona mtu ana mawazo gani hata kabla hajayasema.

▪️Huunganisha na nguvu za juu ✨
Ishara ni kama antena za redio.
Zinaunganisha roho yako na nyota, sayari au hata nguvu ya Mungu.
Mfano: mtu akitazama jua, au akitumia mandala, anahisi nguvu ya kuunganishwa na ulimwengu mzima.

▪️Lakini pia zinaweza kufunga mtu ⛓️
Ukibaki kwenye tafsiri ya juu juu, unakosea.
Mfano: mtu akidhani msalaba ni chuma tu, au mwezi ni mapambo tu angani, atabaki kwenye mwili bila kugusa roho yake halisi.
Ishara ni kama milango ... unaweza kuingia ndani (roho), au ukabaki mlangoni (kimwili).

HIVYO

👉Ishara ni lugha ya muumba na ulimwengu.
Ni alama za siri ambazo zinabeba ujumbe wa roho.
Ukiunganisha Ishara + Namba, unapata msimbo kamili wa maisha.

👉Mtu anayejua kusoma na kutafsiri ishara:
Anaweza kutambua mambo yatakayotokea kabla hayajatokea.
Anaweza kuona siri ambazo macho ya kawaida hayaoni.
Anaishi maisha ya ndani yenye mwanga na uelewa mkubwa.

👉Kwa kifupi: Ishara = Vifunguo vya roho kuelekea milango ya ukweli.

Umeelewa..❓
IMG-20251002-WA0637(1).jpg
 
Back
Top Bottom