Mwenda ni nani?

Mwenda ni nani?

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
13,181
Reaction score
20,471
CHADEMA yamteua Mwenda ubunge Kalenga


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemteua mwanasheria Sinkala Mwenda kugombea ubunge wa Kalenga baada ya kuwashinda wenzake 13.


Katika kinyang’anyiro cha uteuzi huo kada aliyekimbia Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kushindwa kura za maoni mwaka 2010, Zubery Mwachura, aliambulia kura sifuri.


Mwenda alitangazwa kuwa mshindi baada ya uchaguzi uliofanyika juzi kwa zaidi ya saa 10 mjini Iringa.

Uchaguzi huo ulisimamiwa na wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA taifa, Chiku Abwao na Benison Kigaila, ambapo kura 132 zilipitisha jina la mwanasheria huyo huku kura 122 zikimchagua Grace Tendega.
Katika uchaguzi huo, kada wa CHADEMA na muuza magazeti maarufu mjini Iringa, Aidan Pungili, aliambulia kura 2 wakati Daniel Luvanga akipata kura moja.

Wagombea wengine walioonyesha kufanya vema baada ya kujiunga na CHADEMA wakitokea CCM ni Dk. Evaristo Mtitu, aliyepata kura 32 na Ancent Sambala aliyepata kura 22.

Mgombea, Akbar Sanga, alipata kura 21; Rehema Makoga kura nne, Henry Kavina kura tisa, Mussa Mdede kura 48; Mchungaji Samweli Nyakunga kura mbili na Mwalimu Vitus Lawa akipata kura 14.

Kigaila aliwataka viongozi wa CHADEMA Jimbo la Kalenga kukijenga zaidi chama hicho na kwamba, baada ya kampeni kuanza Wana CHADEMA wilaya zote za Mkoa wa Iringa wataingia kazini katika jimbo hilo.



  • Source: Tanzania Daima
 
Kila la kheri kamanda Mwenyezi Mungu awalinde mfanye kpeni za kistarabu
 
ni raia wa zambia eneo la ....... kule slaa alikokwenda akakutana na rais satta last year ngoja uhamiaji wafanye yao ccm tunashinda kama kawa kawa dawa
 
Mtakuja kutukanana ,na mwisho mgimwa atashinda,chadema ya sasa ni ya mazingaombwe,na sii ya wanamikakati,mtaisoma namba mbowe boys.
 
Kamati kuu leo ndio inakutana rasmi kupitisha jina la mgombea ubunge jimbo la kalenga.
 
Kamati kuu leo ndio inakutana rasmi kupitisha jina la mgombea ubunge jimbo la kalenga.[/QUOTE/]

Bila shaka Kamati Kuu haitafanya makosa ya kutompitisha!

Kumbuka CCM inajuta kwa kumpitisha Kigwangwala aliyeshika nafasi ya tatu!
 
Heading haiendani na thread, hata hivyo Lucas Sankala Mwenda ameshinda kwenye uchaguzi wa awali, cc ndiyo itakayoamua either kumpitisha mwenda, ama Grace aliyekuwa mshindi wa pili.
CHADEMA lazima ihakikishe inapitisha jina la mgombea ambaye ni kipenzi cha wanaKalenga.
 
Back
Top Bottom