Mwema na habari za ki interijensia.


C

Calist

Senior Member
Joined
Dec 17, 2010
Messages
130
Likes
0
Points
0
C

Calist

Senior Member
Joined Dec 17, 2010
130 0 0
Mara nyingi tumekuwa tukiwasikia polisi wakizuia mambo kadha wa kadha yasifanyike kwa sababu za kiinterijensia, hawa ni wataalam waliobobea katika kutafuta taarifa muhimu ambazo kwa mtu wa kawaida sio rahisi kuzipata. Taifa limetumia kodi zinazokusanywa kutoka kwa walala hoi kuwaandaa wataalam hawa.

Sintofahamu inakuja pale tunaposikia viongozi wa kisiasa na kidola wakiomba kupewa majina ya vigogo walioficha vijisent kwenye nchi za wenzetu waliotangulia, hivi kweli hawa interijesiaz wameshindwa kupata majina hayo hadi wasubiri kutajiwa na raia wa kawaida ? Au kazi yao ni kutafuta kutafuta tu habari za wanaojindaa kufanya fujo kwenye mikutano ya cdm ? Acheni utani bana mnawajua walioficha vijisent shughulika nao vinginevyo ni wakati muafaka wa kuhoji uwepo wenu kama una manufaa kwa taifa hili.
 

Forum statistics

Threads 1,236,893
Members 475,327
Posts 29,271,301