Mwelekeo wa Maendeleo Kitaifa


TingTing

TingTing

Member
Joined
Dec 20, 2009
Messages
93
Likes
2
Points
0
TingTing

TingTing

Member
Joined Dec 20, 2009
93 2 0
Tanzania ni nchi moja ambayo imejaaliwa karibu kila kitu ikiwa ni pamoja na amani na maeneo kwa ajili ya upanuzi na maendeleo madogo madogo. Nchi yetu imekuwa ikipanuka kadri siku zinavyozidi kusonga mbele kwa ujio wa vizazi vipya kila kukicha. Tatizo ambalo tunalo ni viongozi wetu wa sasa kutoshindwa kupanga au kuweka mipango endelevu kwa ajili ya kulikomboa taifa ama kuliweka katika sehemu ya biashara ya ushidani au ubora wa kurahisisha maisha na mizunguko kwa wananchi na wakazi wa Tanzania kwa ujumla.

Mara nyingi huwa najiuliza kwa nini tuwe na systems nyingi ambazo hazifanyi kazi kwa namna ambayo inatakiwa? Kwa nini hatuna kupitia kwa viongozi wa sasa mipango endelevu ya kuiweka nchi katika ubora wa ushindani? Kwa nini baadhi ya viongozi wetu wa sasa wanaendekeza ubinafsi kwa maslahi yao wenyewe badala ya kitaifa? Kuna kiongozi ambaye anaweza simama na kusema kuwa aliiboresha nchi yake Tanzania kwa kuleta mipango na mikakati endelevu na kuiweka wazi kwa maslahi ya taifa? Ni maswali ambayo majibu yake yanaweza kuwa rahisi lakini kutokana na uelewa wa wahusika basi yanaonekana ni magumu kuyajibu.

Hii inaoyesha dhahiri kuwa mipango na mikakati haitekelezwi kabisa na wahusika hubakia kuwapumbaza wananchi na maneno yao ya ulaghai. Mfano ni pale ambapo "Zima Moto" inapokuwa mbali na makazi ya wananchi huku mji ukipanuka katika kila wilaya. Sitashangaa nikiambiwa leo kuwa wilaya zote zinategemea zima moto ya maeneo ya Upanga. Hivi kweli kuna mipango au mikakati yoyote ya kuleta huduma karibu na wanachi walipo? Hivi ni kwa nini watanzania tunashindwa kujipanga hadi kila kitu tufanyie na "mzungu"? Hii ni kuonyesha udhaifu katika ujasiri wa kujaribu kurekebisha na kuboresha mambo tofauti tofauti kwa faida ya wananchi. Tunapozungumzia suala la kutengeneza reli na kuleta treni ikimbiayo 120km/h kutoka Dar hadi Rwanda siyo kuwa ni jambo baya ila tu ni kuangalia hali halisi ya uhitaji wa huduma hiyo. Mfano; tinaweza tengeneza barabara "2-ways or 3-ways highway" kila pande kwenda na kurudi toka Tanga hadi mkoa wa Kagera ambapo kuna mpaka wa Rwanda na Tanzania. Badala ya kuijazia kazi Bandari ya Dar, tunatakiwa tuboreshe Bandari ya Tanga ili iweze kuhudumia nchi jirani kama Rwanda n.k. Ni dhahiri kuwa Rwanda lazima itegemee nchi jirani kuweza kuingiza vitu nchini mwao wakati njia ya karibu itakuwa ni Tanzania kupitia Tanga. Rwanda kutegemea Mombasa ni gharama sana kwao na wawekezaji wao kutokana na kupitia nchi mbili kama si tanzania tokea Mombasa basi ni Uganda tokea Mombasa kisha Rwanda. Ujio wa Umoja wa Afrika Mashariki utatuwezesha kuingiza hela kupitia Bandari ya Tanga.

Bandari ya Mtwara pia inatakiwa iboreshwe na kuwekwa katika kiwango ambacho kinaweza kubeba meli kubwa toka nchi mbali mbali. Bandari ya Mtwara iweze kuhudumia nchi jirani kama Msumbiji, Mbeya, Malawi na Zambia wakati Bandari ya Dar ibakie kama ndiyo main center na bandari yenye kuhudumia mikoa ya karibu pia ndani ya Tanzania na nchi jirani ikiwezekana. Umuhimu wa barabara za toka Mtwara hadi Tunduma, Tanga hadi Kagera na Dar hadi Kigoma zitaweza kutatua tatizo la misongamano ya mgari barabarani na pia kwa kiasi kidogo kupunguza foleni barabarani.

Miundombinu inapokuwa imeboreshwa basi wawekezaji uweza kujitokeza na pia gharama za uendeshaji zinaweza kupungua kutokana na uzuri na uimara wa barabara hivyo kuwapunguzia mzigo wawekezaji kwenye suala zima la kugharamia huduma za usafirishaji wa bidhaa zao au mizigo yao. Tanzania bila kuwa na "vision" basi tutaishia kuwa hapo hapo tulipo hadi vizazi vijacho vije vibadili miundo. Serikali haifanyi chochote kwenye suala zima la rushwa na matokeo yake wanaoangamizwa ni wale wala rushwa wadogo wadogo angali wale wakubwa wanatawala tu mitaani bila ya kuwa na wasiwasi. Hivi ni lini ambapo tutafika pale ambapo tutaweza kuwa na imani na viongozi wetu pamoja na huduma kwa ujumla? Ni lini tunaweza kumsaidia mzawa mwenye nia ya kuwekeza kwa kumpunguzia maushuru ambayo hayaendani na nia halisi ya mwekezaji mzawa. Gharama hizi utuacha tukikosa wawekezaji ambao ni raia wa tanzania haswa wale ambao wapo nje ya nchi na wana nia ya kuwekeza nchini mwao lakini wanashindwa kutokana na ukiritimba uliopo.

Binadamu wanasahau kuwa hipo siku itafika na wao watakuwa wananchi wa kawaida kama wananchi wengine na hizo sheria wanazoziweka sasa zitawasulubu tu wakati wao ukifika na sitashangaa wakianza kuwa mstari wa kwanza kuzilaani. Nimefurahishwa na habari kuwa sasa makampuni ya simu yanatakiwa kuingia katika "stock exchange" ambapo watanzania wenye uwezo na nia wanaweza kununua hisa katika makampuni hayo ya simu. Tatizo la hili ni kuwa rushwa ilitapakaa sana na wahusika wanalijua hili lakini walifumbia macho sana maana walijiweka wao kama ndio wanashares katika makampuni hayo badala ya kutenga baahdi ya hisa kwa wananchi wa kawaida hili nao waone matunda ya uwewekezaji wa wageni. Jirani zetu Kenya wao walikuwa na utaratibu wa asilimia 30 ya uongozi lazima iende kwa wazawa na pia lazima itengwe fungu fulani kwa wananchi wa kawaida wenye nia na uwezo.

Kama wengi wanakumbuka ni pale Safaricom na Mumias na "KPLC" walipoamua kuja na public offer "IPO" na tuliona wanafunzi, wakenya na karibu kila raia akiwa tayari kununua hisa kadha wa kadha. Utartibu huuu unatakiwa uendelee na kwa wawekezaji wengine wowote wale ambao ni wageni ikiwa ni pamoja na kuajiri wazawa katika nafasi za chini ambazo zinaweza kufanyika au kufanywa na wazawa. NMB walijaribu kuuza kwa wananchi wenye nia na uwezo kipindi fulani cha nyuma na angalau inaonyesha matumaini na wao ndio angalau walikuwa wa kwanza kujitangaza kufanya hivyo wakati CRDB na NBC wao wanaona walivyo ni sawa tu huku wakiendelea kuwapa huduma mbovu wananchi wake haswa CRDB Bank. Kama ingekuwa ni uwezo wangu basi ningejizatiti katika kuboresha mfumo mzima wa Elimu, Afya, Miundombinu, Nishati, Usalama wa Nchi na Raia, Kilimo, Sheria na Katiba, Kodi na Mapato, Bima ya Afya na Uongozi wenye kuwajibika na kujiwajibisha. Tanzania bila kuwa na kiongozi ama viongozi wenye misimamo kama Moi, Kagame et al hii nchi haiwezi kuboreshwa na hawa wa sasa. Mabadiliko makubwa ndio yatatupeleka tunapoona panafaa. We do not need wazee rather what they call "Young Turks" who are reformists to lead this country. Wazee will take us nowhere believe me, if I am wrong correct me. It is so sad after 40-years yet if it were not for previous "WAKOMBOZI" you as a leader wouldn't be mis-using your position for personal gains, wouldn't be putting on those suits at expense of taxpayers cash and would you be riding in those non-economical 4WD Landcruisers & Prados, Mercs, BMWs and Vogues. :(
 

Forum statistics

Threads 1,250,530
Members 481,403
Posts 29,736,594