Kahise
JF-Expert Member
- Jul 25, 2008
- 379
- 435
Wadau wa Elimu, kwanza naomba ku declare interest kuwa mimi nilisomea ualimu ngazi ya stashahada.
Wakati nasoma shuleni, hasa somo la Historia nilifundishwa na kuaminishwa kwamba elimu ya kikoloni ilikuwa mbaya. Kwamba wakoloni waliwasomesha watanzania wale ambao walitaka kuwatumia kuimarisha utawala wao, kwamba ilitolewa kwa ubaguzi, kwamba ilikuwa haina nia njema, n.k.
Leo nikitafakari elimu hiyo niliyoipata, nashindwa kuelewa kwanini nilifundishwa mambo yale.
Je, baada ya Tanzania kupata kujitawala elimu yetu yenyewe imekuwa na malengo madhubuti ya kuwakomboa Watanzania au mambo yameendelea kuwa HOVYO?
ANGALIA: Wakati wa elimu ya mkoloni, Kila aliyeingia shule alijua kusoma na kuandika.
Wakati huu, lengo la kujua kusoma na kuandika lipo, lakini wasiojua kusoma na kuandika wanaendelea kupanda madarasa.
Elimu ya mkoloni ilipangwa kwa malengo mahususi kwamba kila level inayofikiwa iwe imemwandaa mtoto kupata Ujuzi (skill) fulani. Hivyo, kujua kusoma, kuandika na kuhesabu kulipangiwa miaka 4 tu, yaani Darasa la Kwanza mpaka la nne.
Baàda ya pale wanafunzi wanaenda Middle School kwa miaka minne tena ambapo walimaliza wakiwa na fani tofauti tofauti. Kijana aliyemaliza middle school wakati ule aliweza kuishi ndani ya jamii kwa kujiajiri. Kisha kijana aliweza kuendelea na masomo yake ya sekondari nayo ilikuwa na malengo mahususi kwa kila level.
Leo tijiangalie, kujua kusoma, kuandika na kuhesabu, kunachukua miaka 7 na wanaoweza kuujua ujuzi huo ni wachache kwa kuwa tunapata vijana wengi wanaomaliza shule bila kujua kusoma na kuandika.
Je, wadau ni kweli elimu yetu ina tija yoyote kwa watoto wetu?