Mwekezaji atiwa mbaroni kwa ujangili

Mwekezaji atiwa mbaroni kwa ujangili

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,687
Meneja wa Hoteli ya Kitalii ya Tree Top, iliyoko ktk Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, wilayani Moduli ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kukutwa na ngozi za chui nyumbani kwake, akiwa katika harakati za kuisafirisha kinyemela kwenda nje ya nchi.
Inasemekana kuwa ameachiwa kwa dhamana baada ya kudhaminiwa na mfanyakazi mmoja wa Hotel za Sopa Lodges inayomiliki msururu wa hoteli kwenye mbuga za wanyama katika Mikoa ya Arusha na Mara.
Chanzo cha habari hii ni gazeti la Mwananchi la jumatatu, Desemba 24, 2012.
 
Vinana vipo vingi kumbe,! WEKA MBALI NA TEMBO
 
Huyo si mwekezaji bali mchukuaji. Na majambazi wa namna hii wapo wengi kwenye mbuga zetu wakikingiwa vifua na vinana na visekwa vinavyojulikana kujiingizia utajiri kwa kubaka mbuga zetu. Hadi leo hakuna anayejua idadi ya watalii wanaoingia nchini kutokana na kuzuka tabia ya watu wa viwanja vya ndege kukusanya Euro 50 na kutowapa risiti watalii hivyo kuingia na kuondoka kinyemela. Huyu alipaswa kuchomwa moto. Hiyo ngozi angekamatwa nayo kapuku huenda angeuawa kama jangili siku hiyo hiyo. Kama serikali imebariki ujangili tena kwa wezi wanaoitwa wawekezaji kwanini wananchi nao wasifanye ujangili ili kujikimu?
 
Mwekezaji wa utaliii kakamatwa, Kagasheki hapendi jamani.
 
Back
Top Bottom