Mwekezaji aling'akia Bunge

kiatu

Member
Dec 4, 2007
6
1
Kwa wale ambao mmeisoma hii habari katika gazeti la Majira napenda kuwapa ukweli wa hii Hoteli.

Ni kuwa kuwa kuna mgodi wa dhahabu unaondeshwa ki-siri na mmiliki wa hii hotel. Itakuwa kuna mkono wa mkubwa ndani ya serikali. Sijui hata kama hii hotel huwa inafanya kazi za hotel maana ada zake za chumba kwa siku ni kubwa mno, na vyumba vyake huwa vimejaa. Kwa mfano ukienda sasa hivi kuulizia chumba unaweza ambiwa vimeisha jaa hadi mwezi wa 12.

Kuhusu huo mmgodi: Njia ya kuingia ndani ya huu mgodi iko katika jengo moja ndani ya hii hotel. Kwa nje inaonekana kama nyumba/jengo lakini ndani ni machimbo.
Mimi ninaishi na kufanya kazi maeneo ya Serengeti, yote yalioandikwa ni ya kweli. Hakuna kupinga. Nawashukuru wabunge walioliona hili labda wana JF tukilivalia njuga ukweli unaweza patikana. Tutazidi kupashana habari njisi nitakavyozipata.
Nimewahi kutana na mfanyakazi mmoja aliyefukuzwa katika Hoteli hii, alikuwa upande wa ulinzi. Siku moja aliiingia ndani kwa ubishi kutaka kujua kinachoendelea na alifanikiwa kuiba picha moja ya mtu flani. Nitawaelezea siku moja nikikusanya data zote kuhusu hiyo picha.
Basi baada ya kukutwa humo ndani, siku hiyo ndio ilikuwa nwisho wake wa kufanya kazi katika Hotel hii.
Napenda kuwakilisha
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom