Mweka hazina - Halmashauri ya wilaya Mbarali aondolewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mweka hazina - Halmashauri ya wilaya Mbarali aondolewa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by wwww, Jun 29, 2012.

 1. wwww

  wwww JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 350
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 60
  Wanajf kama kawaida yangu nilikuwa kwetu Ubaruku kununua mchele nikapata habari kuwa Kamati ya fedha ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali imemuondoa Mweka Hazina wa Wilaya katika nafasi yake.

  Ilinibidi niondoke Ubaruku kuja Rujewa km 4 kutoka Ubaruku ndipo nikapewa full story kama ifuatavyo;
  Mweka Hazina aliyeondolewa anaitwa FERDINAD K. MANYELE na aliyekaimishwa nafasi hiyo huku ikisubiriwa kupatiwa Mweka Hazina mwingine anaitwa WILFRED MBEWA.

  Kwa mujibu ya mtoa habari kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Mweka hazina huyu ameondolewa na kikao cha Kamati ya Fedha kilichokaa leo kuanzia majira ya saa 5 asubuhi na kumalizika saa 8 mchana kwa azimio kuwa Mweka Hazina ndg. Ferdinand Manyele aondolewe kwenye nafasi yake kwa kushindwa kabisa kuimudu nafasi yake na kuisababishia Halmashauri madeni makubwa ambayo hayalipiki.

  Mtoa habari anaendelea kusema; Mweka Hazina huyu alihamia Halmashauri hii akitokea Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ambako pia aliwahi simamishwa kazi kwa takribani miaka 6 kwa ajili ya kufuja fedha za Halmashauri hiyo, lakini wakubwa wakahongwa kesi ikaisha na kurudishwa kazini, ndipo alipohamishiwa Mbarali.

  Anaendelea kusema, kama ulisikia kwenye gazeti la Tanzania Daima kama wiki mbili zilizopita kuwa huyu bwana aliwekwa ndani na TAKUKURU katika kituo cha Polisi Mbarali kwa tuhuma za kufuja fedha za maedeleo ya Wananchi kama vile fedha kutoka Idara ya Afya Tshs. 101,000,000/= zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali Mpya ya Wilaya, Fedha za Elimu Tshs. 127,000,000/= zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na sasa kuna tuhuma nyingine kuwa yeye pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ndg. Aswege Kaminyoge wametafuna Fedha za WORLD BANK TSHS. 300,000,000/= zilizoletwa kwa ajili ya ujenzi wa tanki la Maji na usambazaji wa mabomba kwa ajili ya wananchi wa Ubaruku.

  Mtoa taarifa anasema ndiyo maana Kamati ya Fedha inayoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ndg. KENNETH NDINGO (CCM) ambayo ina wajumbe wengi ambao ni MADIWANI kutoka CCM wakaamua kuwa wazalendo na kuamua kwa pamoja na MADIWANI wa Upinzani kumuondoa huyu Mweka Hazina.

  RAI YANGU.

  Halmashauri zingine ziige mfano huu kwa kuwawajibisha watendaji wote wanaofuja fedha za Serikali na Serikali isiwakingie kifua watu hawa kwa kuwahamishia sehemu nyingine bali wawashushe vyeo vyao na kuwapeleka kwenye vyombo vya sheria kama wanatuhuma.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. L

  LOVI MEMBE JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2013
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,121
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  huyu manyele ana tuhuma nyingine za kuendesha halmashauri kama biashara ya mbao za baba yake. Alikuwa akikacha vika vikao na kwenda kukusanya maduhuli toka kwa mawakala kinyume cha taratibu za fedha za serkali. Ni malaya mkubwa sana huyu hapa rujewa alishatembea na wanawake wasiopungua 20 ukiacha wake zake 3 mmoja karibia augue ugonjwa wa moyo. Hatari sana amemjengea nyumba aliyekuwa ps wa ded .huyu ps aliondolewa nafasi kutokana na kuvujisha taarifa . Pia alikuwa akimpendelea kwa kumpa pesa za posho za safari ambazo hata hivyo hajawahi kusafiri. Yaani manyele kama king mswati ii vile na prado lake aalilonunua withini six months after arrival at mbarali dc. Marvelous boy haka ni insinuatum humanus sui generis. Kwa ujumla ni lazima ashughulikiwe sawasawa nasikia anajivuni kakake ambaye ni profe. Manyele mkurugenzi wa tbs
   
Loading...