MWAROBAINI WA BOMOA BOMOA HUU HAPA

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,543
22,050
Kutokana na bomoa bomoa inayoendelea kuwakumba wananchi mbalimbali hivi sasa, wengine wakiachwa patupu hawana pa kwenda, na wengine kufariki dunia kwa presha na misongo ya mawazo iliyopitiliza,mfano, ktk bomoa bomoa ya juzi imemkumba mkazi mmoja ambaye ana mke na watoto waliokuwa wanajiaandaa kufungua Shule, mkazi huyo pia alikuwa na mgonjwa ndani ambaye ni mama mkwe wake mwenye stroke, mkazi Huyo Huyo ana miezi 5 tu tangu nyumba yake iungue akiwa safarini, je unadhani mtu kama Huyo alikuwa katika hali gani alipoona nyumba yake ikibomolewa bila malipo? Je alijua kuwa kajenga kwa makosa? Je alifuata taratibu za ujenzi? Jibu..kutokujua sheria siyo kinga ya kosa,ni lazima nyumba yake ingebomolewa, JE UNA MPANGO GANI NA WEWE KUHUSU UJENZI ? UNAJUA TARATIBU?
Leo nitazungumzia sheria na matumizi ya hifadhi ya barabara, Sheria ya barabara namba 13 ya mwaka 2007 kifungu cha 29 kimeainisha eneo la hifadhi za barabara kuu, za mikoa mpaka zile za mitaa hivyo; upana ulioainishwa kwa ajili ya matumizi ya barabara hutumika kwa ajili hiyo tu na si vinginevyo. Mamalaka za barabara zinaweza kutoa kibali kwa maandishi cha kutumia hifadhi ya barabara husika kwa muda na masharti maalum kadiri itakavyoonekana inafaa. Muda utakapoisha mwombaji atalazimika kuomba kibali upya kwa mamlaka ya barabara ambapo atajibiwa kulingana na mipango ya maendeleo ya barabara husika. Itakapotokea kuwa eneo la hifadhi ya barabara linatakiwa kwa ajili ya matumizi ya barabara, basi mwombaji(mwenye kibali) ataondoa mali yake na kuliweka eneo katika hali nzuri kwa gharama zake mwenyewe.
Upana wa hifadhi ya barabara Upana wa hifadhi ya barabara kuu za mikoa ilikuwa mita 45, yaani mita 22.5 kila upande kutoka katikati ya barabara kabla ya mabadiliko ya kisheria kufanyika mwaka 2007. Hapa chini nimeeleza upana wa barabara kwa mujibu wa sheria ya zamani katika mabano na mbele yake ni sheria mpya ya mwaka 2007 inayotumika hadi Hivi sasa.
AINA ZA BARABARA NA UPANA
a). (SHERIA YA ZAMANI-Barabara kuu na za mikoa kwa barabara ya njia moja 22.5 kila upande kutoka katikati ya barabara) SHERIA MPYA YA 2007 ni 30m kila upande kutoka katikati ya barabara
b).(ZAMANI- Barabara kuu na za mikoa kwa barabara ya njia Mbili 22.5 kila upande kutoka katikati ya kisiwa cha barabara(Median)) SHERIA MPYA 2007 ni 30m kila upande kutoka katikati ya kisiwa cha barabara(Median)
C). (ZAMANI- Barabara za wilaya 15m kila upended kutoka katikati ya barabara (SHERIA MPYA 2007-Ni 20m kila upande kutoka katikati ya barabara.
d). (ZAMANI-Barabara ndogo 10m kila upande Kutoka ktkt ya barabara ) SHERIA MPYA 2007 ni 15m kila upande kutoka katikati ya barabara.
e). (ZAMANI-Barabara za vijiji 10m kila upande kutoka katikati ya barabara) SHERIA MPYA 2007 ni 12.5m kila upande kutoka katikati ya barabara
Mambo ya kujadili
a) Je wananchi wanafahamu mgawanyo na matumizi ya ardhi kwa mujibu wa sheria za ardhi, 1999 na sheria ya barabara, 2007?
b) Je, unafahamu ulipojenga kuwa sio sahihi? Au unasubiri kubomolewa? Matumizi ya ardhiyametengwa kwa matumizi mbalimbali, kuna maeneo ya viwanda, makazi,barabara,maeneo ya wazi n.k wewe upo barabarani utatolewa, upo kiwandani utatolewa, upo katika open space…
c) Mara nyingi ikitokea bomoabomoa, wananchi huuliza: Hivi, mbona tuliruhusiwa na maafisa ardhi wenyewe kujenga hapa,na wakati mwinginevibali,leseni, au hati tumepewa nao na pia; mamlaka zingine za serikali, kama za umeme na maji, nazo zilitupatia huduma?
d) Je , uliwaona na kutaka ushauri wa kitaalam kutoka kwa wataalam ili wakushauri kabla ya kununua kiwanja na kujenga ?
e) Na wewe unaejiandaa kununua eneo ,unajua hizo taratibu za kufuata?
 
Back
Top Bottom