Mwarabu kumilikishwa Loliondo

Mwarabu kumilikishwa Loliondo

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,946
Reaction score
38,657
Wadau,
Nakumbuka wengi wetu bado tunamkumbuka mwandishi wa habari za kiuchunguzi Marehemu Stan Katabalo aliyeibua mchakato wa kimya kimya wa Ikulu kumuuzia Mtawala wa UAE ardhi yetu yenye rasilimali ya Loliondo. Kifo chake kilikuwa cha kutatanisha, na ikichukuliwa enzi zile ambapo uhuru wa vyombo vya habari ulikuwa ndani ya kikombe hivyo hakukuwa na wa kuibana serikali kuhusiana na utata mwingi uliogubika habari ile na kifo chake.

Leo tunashuhudia mwendelezo wa serikali kushinikiza kuwaondoa wananchi wa Loliondo ili kupanua kitalu cha uwindaji kwa mwarabu ambaye kipande alichopewa kimeshamalizika wanyama na anataka ZAIDI. Kinachotia mashaka ni namna ambavyo mwekezaji huyo alivyoweza kujijengea himaya yake ambapo hata mtu anapokaribia ama kuingia eneo lile anakutana na ujumbe KARIBU KATIKA FALME YA NCHI ZA KIARABU ambapo kwa ujumbe huo ni dhahiri kipande ile ni milki ya mfalme wa uarabuni.

Katiba imekiukwa na wanaotakiwa kuijibu hii ni IKULU kwa sababu ndiyo tuliowapa mamlaka ya kuilinda Katiba chini ya Rais. Nanukuu hapa chini kipengele kilichokiukwa, soma kwenye bold
28. Ulinzi wa taifa Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6 (1) Kila raia ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha uhuru, mamlaka, ardhi na umoja wa taifa.
(2) Bunge laweza kutunga Sheria zinazofaa kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kutumikia katika majeshi na katika ulinzi wa taifa.
(3) Mtu yeyote hatakuwa na haki ya kutia sahihi kwenye mkataba wa kukubali kushindwa vita na kulitoa taifa kwa mshindi, wala kuridhia au kutambua kitendo cha uvamizi au mgawanyiko wa Jamhuri ya Muungano au wa sehemu yoyote ya ardhi ya eneo la taifa na, bila ya kuathiri Katiba hii na sheria zilizowekwa, hakuna mtu atakayekuwa na haki ya kuwazuia raia wa Jamhuri ya Muungano kupigana vita dhidi ya adui yeyote anayeshambulia nchi.
(4) Uhaini kama unavyofafanuliwa na sheria utakuwa ni kosa la juu kabisa dhidi ya Jamhuri ya Muungano.

Tuhuma hizi zimekuwa zinakiukwa kwa makusudi kutolewa ufafanuzi na wahusika (Ikulu).

Nchi imemegwa na kupewa asiyestahili. Nini kifanyike?
 
IPO SIKU KILA KITU KITAWEKWA WAZI, na sasa ndo yameanza kuwekwa wazi, huo mkataba wa loliondo na falme za kiarabu ni dhahiri tunaibiwa ndani ya nchi yetu. Haya yalifanyika wakati wa utawala wa mwinyi nadhani lakini wakati wa mkapa yakaendeleswa na hata sasa JK anayaendeleza, JK weka mambo funguka, pengine tunafaidi kwa uwepo wao au nyie wakubwa peke yenu ndio mnao faidi?
 
Napita tu maana nna ghadhabu na Jk na magamba nisije nkala ban kama juzi nliposababishiwa na Ndugai na Serugamba.
 
Msingi wa utumwa umejengeka kwenye akili ya mtumwa mwenyewe.
Bila kubomoa misingi ya utumwa katika fikra za wananchi na viongozi wa kiafrika, Uhuru wetu hautakamilika.
Kinachoendelea sasa hivi ni kujirudisha utumwani kwa kuchagua wenyewe!
Kuna ulazima wa kujenga fikra za kuchukia kutawaliwa na hata tunapokumbuka historia tuendeleze juhudi za ukombozi na siyo kuwachekea na kuwamilikisha ardhi yetu watesi wa mababu zetu.
Uhuru kwa waafrika ulikuwa na utaendelea kuwa na maana ya ukombozi wa mtu mweusi, na sera za msingi zinatakiwa kuhakikisha misingi ya uchumi wa Afrika ikiwemo Tanzania unamilikiwa na Waafrika wenyewe.
Yeyote yule anayejaribu kurudisha nyuma misingi ya uhuru na ukombozi wa waafrika, ndiye adui namba moja hata kama ni ndugu wa damu.
 
28. Ulinzi wa taifa Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6....hakuna mtu atakayekuwa na haki ya kuwazuia raia wa Jamhuri ya Muungano kupigana vita dhidi ya adui yeyote anayeshambulia nchi.
Nimejiuliza sana maana ya hiki kipengele nakosa jibu.Jeshi la polisi wamewekwa tayari kupambana na raia wanaodhamiria kumwondoa mvamizi.Nijuavyo ni kwamba mvamizi anaweza kuja kwa mbinu nyingi ikiwemo ya mikataba ya ulaghai lakini azma yake ni kuikalia nchi ama kipande cha nchi kwa manufaa anayoyajua yeye.Tufike mahala tuwashinikize wabunge kuchukua hatua ya kuhoji madudu kama haya bila kusubiri raia waamue...
 
NI kweli mwarabu alimilikishwa Loliondo na kutokana na juhudi za wabunge kama kina Philp Marmo na mwandishi Stan Katabaro walizuia akaendelea kuwinda kimya kimya huku akifanya kila kitu kama Dubai. Leo Serikali hasa IKULU inammilikisha Mwarabu eneo la Loliondo. Wanafanya hesabu ili kutumia vipengele vya sheria ya ardhi ya kuhaulisha ardhi ya vijiji na kuwa ya hifadhi. Wanadai ni kwa madhumuni ya hifadhi huku mwarabu inasemekana amewinda takriban wanyama 50,000 hadi sasa, amejenga chanzo kikuu cha maji ameweka mtambo wake wa mawasiliano. Halafu leo IKULU inataka kuwaondoa Wamasai. Kwa sababu Serikali haitambui tena sheria isipokua zile za kujinufaisha, TUWAUNGE MKONO wamasai wa Loliondo. WOTE KWA UMOJA WETU TUSIKUBALI
 
mmarekani anaitwa mmarekani
mcanada anaitwa mcanada
muUAE anaitwa mwarabu
warabu mbona wanatoka nchi nyingi tu, moja wapo ni Tanzania, sasa hao wote ndio wamiliki? Acheni ubaguzi bana
 
mnataka wazungu na wadenmark pekee ndio waje wawekeze??? pili hii habari ni ya kizushi tu
 
mnataka wazungu na wadenmark pekee ndio waje wawekeze??? pili hii habari ni ya kizushi tu
Tatizo lako ni kuyaangalia mambo kisiasa bila hata kutafakari.

Hebu fafanua uzushi wa habari hii
 
NI kweli mwarabu alimilikishwa Loliondo na kutokana na juhudi za wabunge kama kina Philp Marmo na mwandishi Stan Katabaro walizuia akaendelea kuwinda kimya kimya huku akifanya kila kitu kama Dubai. Leo Serikali hasa IKULU inammilikisha Mwarabu eneo la Loliondo. Wanafanya hesabu ili kutumia vipengele vya sheria ya ardhi ya kuhaulisha ardhi ya vijiji na kuwa ya hifadhi. Wanadai ni kwa madhumuni ya hifadhi huku mwarabu inasemekana amewinda takriban wanyama 50,000 hadi sasa, amejenga chanzo kikuu cha maji ameweka mtambo wake wa mawasiliano. Halafu leo IKULU inataka kuwaondoa Wamasai. Kwa sababu Serikali haitambui tena sheria isipokua zile za kujinufaisha, TUWAUNGE MKONO wamasai wa Loliondo. WOTE KWA UMOJA WETU TUSIKUBALI
Mkuu hata katiba imeonesha njia endapo kuna wahuni watadhani wanaweza kuuza nchi bila kuhojiwa ...hakuna mtu atakayekuwa na haki ya kuwazuia raia wa Jamhuri ya Muungano kupigana vita dhidi ya adui yeyote anayeshambulia nchi....

Hakuna wa kuwazuia watanzania wakiamua kulinda nchi yao. Naunga mkono juhudi za WAMASAAI kutoondolewa kwenye ardhi yao ambayo ni yetu sote
 
Wanakesha huku jf wakipambana na chadema uku wanauza nchi yetu.,hayo ndo maendeleo hata wale walioishi maeneo hayo toka mkoloni leo wanaambiwa sio kwao ni kwa lijamaa liwekezaji la 2013,kama hizi ndo sera za magamba tutegemee mengi tutahamia hadi baharini..
 
OBD imeamua sasa kudai haki yao ambayo wamekuwa wakiilipia kwa miaka mingi.
Pamoja na kujaribu kuwarubuni viongozi wa maeneo wanayoyataka kuyaongezea kwenye himaya yao lakini wameshindwa. Mbinu kubwa wanayoitumia sasa ni kuwaweka watawala wenye maamuzi kwenye mfuko wao na tumeyaona matokeo yake.

Ni wajibu sasa kuilinda nchi kwa namna yeyote ile. Haiwezekani tukawa kama vipofu na kuacha urithi wetu halali ukimalizwa mbele yetu. Katiba iheshimiwe
 
Wadau,
Nakumbuka wengi wetu bado tunamkumbuka mwandishi wa habari za kiuchunguzi Marehemu Stan Katabalo aliyeibua mchakato wa kimya kimya wa Ikulu kumuuzia Mtawala wa UAE ardhi yetu yenye rasilimali ya Loliondo. Kifo chake kilikuwa cha kutatanisha, na ikichukuliwa enzi zile ambapo uhuru wa vyombo vya habari ulikuwa ndani ya kikombe hivyo hakukuwa na wa kuibana serikali kuhusiana na utata mwingi uliogubika habari ile na kifo chake.

Leo tunashuhudia mwendelezo wa serikali kushinikiza kuwaondoa wananchi wa Loliondo ili kupanua kitalu cha uwindaji kwa mwarabu ambaye kipande alichopewa kimeshamalizika wanyama na anataka ZAIDI. Kinachotia mashaka ni namna ambavyo mwekezaji huyo alivyoweza kujijengea himaya yake ambapo hata mtu anapokaribia ama kuingia eneo lile anakutana na ujumbe KARIBU KATIKA FALME YA NCHI ZA KIARABU ambapo kwa ujumbe huo ni dhahiri kipande ile ni milki ya mfalme wa uarabuni.

Katiba imekiukwa na wanaotakiwa kuijibu hii ni IKULU kwa sababu ndiyo tuliowapa mamlaka ya kuilinda Katiba chini ya Rais. Nanukuu hapa chini kipengele kilichokiukwa, soma kwenye bold

Tuhuma hizi zimekuwa zinakiukwa kwa makusudi kutolewa ufafanuzi na wahusika (Ikulu).

Nchi imemegwa na kupewa asiyestahili. Nini kifanyike?

Una uhakika na hapo kwa red? au unataka kupotosha umma wa watanzania!

Nyie semeni wazi tu kwamba mnachotaka ni malisho na maji kwa ajili ya ng'ombe wenu (wanyamapori siyo priority kwenu), haya mengine ni uzushi mtupu!!
 
Tatizo lako ni kuyaangalia mambo kisiasa bila hata kutafakari.

Hebu fafanua uzushi wa habari hii

Mkuu, usiwe unaumiza kichwa chako kwa watu wa aina hii ( bungeni, majebere , and ze makopolo and co ) .......uelewa wameuza lumumba kwa vipande vya rupia.
 
Last edited by a moderator:
Una uhakika na hapo kwa red? au unataka kupotosha umma wa watanzania!

Nyie semeni wazi tu kwamba mnachotaka ni malisho na maji kwa ajili ya ng'ombe wenu (wanyamapori siyo priority kwenu), haya mengine ni uzushi mtupu!!
Nina uhakika mkuu. Uthibitisho wake ni haya tunayoyashuhudia leo.
Tatizo lako na wenzako huko juu ni kujaribu kutumia hadaa ya kutumia wanyama pori ili mkamilishe mpango wenu wa uovu.

Wanyama walikuwepo hata kabla ya mjerumani kuja, na Wamaasai waliishi na wanyama hao huku wakifuga bila matatizo yeyote. Lakini tangu mlipokubali kuishi kwenye mifuko ya majambazi ya nje ndo mmejivua hata uraia.
 
Mkuu nimefurahi ulivyosema hapo kwa red, kumbe unajua kiini cha tatizo la Loliondo. Ndo maana nimesema hayo mengine ni bla bla tu. Central point ni kwamba wanataka malisho na maji kwa ajili ya mifugo yao. Kwahiyo serikali inavyosenga hilo eneo inamaana hawatakuwa na access na hivyo vitu, full stop!!!

Mkuu wanayosema politicians na activists ni porojo tupu, point kubwa ni hiyo niliyoisema believe me or not!
 
Una uhakika na hapo kwa red? au unataka kupotosha umma wa watanzania!

Nyie semeni wazi tu kwamba mnachotaka ni malisho na maji kwa ajili ya ng'ombe wenu (wanyamapori siyo priority kwenu), haya mengine ni uzushi mtupu!!

Hata ikiwa uongo watu watahisi kweli, tatizo mnaharibu sana kuliko kujenga ndugu zangu.
 
Back
Top Bottom