Mwapachu waambie barrick walipe kodi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwapachu waambie barrick walipe kodi

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by mfianchi, Sep 12, 2011.

 1. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,946
  Likes Received: 1,505
  Trophy Points: 280
  Tulisoma hivi majuzi kuwa makampuni ya migodi na simu hailipi kodi inayostahili kutokana na mapato wanayoyapata,kwa lugha nyepesi ni kuwa wanakwepa kulipa kodi,na sheria zetu ziko wazi kuhusu wakwepaji kodi.Pia nilimsikia Mwenyekiti wa Barrick Mheshimiwa sana Juma Mwapachu akisema kampuni yake imetenga mamilioni ya fedha kwa ajili ya mfuko wa jamii zinazozunguka hiyo migodi,mimi naona kwanza angejikemea mwenyewe na watendaji wake kwa kukwepa kulipa kodi kwa kampuni iliyo chini yake na inamharibia taswira yake kama kiongozi makini.Pia nashangaa TRA wameufyata angekuwa muhindi wa pale kariakoo au mimi mlalahoi siku nyingi ningeshafilisiwa,
  Angalizo TRA wasiwe wanaangalia tu vidagaa kwenye ulipaji kodi bali hata mapapa au nyangumi nao washughulikiwe kwa usawa,inashangaza kwa TRA walivyoshupalia pale Break Point kuhusu mashine za malipo hadi mkurugenzi akatoa ufafanuzi lakini kwa mapapa kama makampuni ya simu na migodi hatujasikia tamko lolote.
  Ingekuwa nchi za wenzetu huko majuu haya makampuni yangekuwa historia,kazi kwako Kitilya na aibu kwa TRA
   
Loading...