Mwanzilishi mwenza wa Intel Gordon Moore Afariki

thesym

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
3,797
4,688
Gordon Moore amefariki ijumaa 24.03.2023 akiwa na miaka 94.

Moore alianzisha intel mwaka 1968 akiwa na mwenzake Robert Noyce.

Kabla Moore aliwahi kufanya KAZI kwenye kampuni ya Shockley semiconductor kampuni ya mvumbuzi wa transistor na baadae wakamsaliti kisha kuanzisha kampuni ya Fairchild semiconductor wakiwa watu nane.

Na baadae wengine wakajitoa na kuanzisha kampuni kama Advanced Micro Devices (AMD) na integrated electronic (intel).

Miaka hiyo silicon valley ilitawaliwa na semiconductor. Intel ni kampuni ya Kwanza kuunda general purpose microprocessor.

Moore alikuwa ni PhD holder wa chemistry.
 
Kampuni nyingi Marekani zimeundwa na washikaji kwa ubia, Tanzania twapenda solo sana ndo maana biashara nyingi zinakwama.
Pia wabongo tuna kasumba ya kutaka onekana kila mtu mjuaji

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Wenzetu sijui wanawezaje !
Serikali ya USA huwa inasapoti Sana hizi kampuni, mwanzoni chip zilikuwa zinatumika kwenye siraha hasa missile kabla ya soko la PC kukua na huku idara ya Defence Advanced Research Projects ikiwa inatoa funds za R&D na baadae tena serikali inakuwa mteja.

Na wakati huo serikali inayalinda pale ushindani toka nje unapokaribia kuyapoteza hayo makampuni.

Intel ilikuwa nusu ipotee kutokana na ushinda WA kampuni za semiconductor toka Japan kama Toshiba maana biashara Yao kubwa ilikuwa ni DRAM, baadae serikali ya USA ilianza kulazimisha Japan kupunguza uuzaji WA chips USA na kuongeza bei na mambo mengine, na pia CEO kipindi hiko aliamua kujikita kwenye uundaji WA processor na kupiga Chini memory chips na boom ya PC ikawa anaongezeka.
 
Back
Top Bottom