Mwanza wazidi kuporomoka, wazidiwa na Dodoma, Pwani na Mbeya kwenye mapato

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,586
14,138
Nawasalimu kwa jina la JMT

Katika kile kinachoonekana ni shift of economic powers baina ya Mikoa,Mkoa wa Mwanza na Jiji la Mwanza kiujumla vimezidi kuporomoka kiuchumi na hivyo kuondoa ushawishi na umuhimu wake kiuchumi..

Kwa mujibu wa makusanyo ya kila Halmashauri, Mkoa wa Mwanza umeshika nafasi ya 5 kitaifa ukizidiwa na Dodoma (2),, Pwani(3) na Mbeya(4) huku Dar ikiongoza kama Kawa.

Kwa mwenendo huu wa Kiuchumi ni wazi Mkoa wa Pwani ulioitwa wa waswahili sasa utaheshimika kama mdau mkubwa wa uchumi wa Tanzania..

Nimejiuliza tuu inakuaje mkoa wa Mwanza wenye idadi kubwa ya watu lakini wanashindwa kuonyesha umuhimu wao kwenye uchumi hapa Tanzania?

Wingi wa watu ni fursa lakini kwa Mwanza na Kanda ya Ziwa kiujumla naona ni majanga tupu..Ni muhimu sasa serikali kugawa rasilimali Kwa kuzingatia uchangiaji kwenye Pato la Taifa.

Hongera sana mkoa wa Dodoma,Pwani na Mbeya Kwa kuonyesha uchapakazi kwa vitendo.

Serikali uangalieni Mkoa wa Rukwa kwa jicho la huruma na kusaidiwa , yaani mapato ya Mkoa bil.6 kweli?

Screenshot_20220506-134844.png

Screenshot_20220506-134941.png

Screenshot_20220506-155529.png

Screenshot_20220506-155655.png
 
Mapato ya Halmashauri kama Service Levy...?! na mengineo ndio yanapima GDP...?! mbona hapo kwenye kiambatanisho chako sioni, nione Lengo pamoja na Makusanyo yaani bajeti...
 
Mwanza wamekatishwa tamaa.wanakusanya mapato ya kutosha alafu watu wachache wanaiba kwa kiongeza ma-sifuri sifuri mpaka manne kwenye manunuzi ya serikali.
kifaa chenye thamani ya milioni 30 kinanunuliwa kwa milioni 100.
Nyie ndio maana huwa mnauana Sababu ya umaskini uliokithiri..

Hayo mapato hutumika kwenye Halmashauri husika hayaendi kokote.
 
Mapato ya Halmashauri kama Service Levy...?! na mengineo ndio yanapima GDP...?! mbona hapo kwenye kiambatanisho chako sioni, nione Lengo pamoja na Makusanyo yaani bajeti...
Ni moja ya kiashiria muhimu cha GDP na moja ya kipimo kinachoonyesha uhalisia zaidi wa maisha ya watu na shughuli zao..
 
Ni moja ya kiashiria muhimu cha GDP na moja ya kipimo kinachoonyesha uhalisia zaidi wa maisha ya watu na shughuli zao..
Naona kuna kiambatanisho hapo juu umeweka kwenye upande wa majiji Mwanza CC ni ya pili baada ya Dar es salaam, sasa sijajua kwanini unasema ni ya tano...?! halafu kama sijakosea Mwanza CC si ndio Nyamagana...?!
 
Tatizo JF imevamiwa na misukule VILAZA halafu wanachojua Ni kutanguliza pua tu kubishana, Chuki, wivu, UTAPELI na UKABILA na ROHO MBAYA za UBINAFSI.

Mapato ya Halmashauri hukusanywa kila Robo mwaka, na Mara nyingi vyanzo vya mapato ya Halmashauri hufahamika.

Mfano, Leseni hulipwa kila baada ya mwaka mmoja, na nyingine miezi 6.

Sàa Kama robo ya kwanza ya mwaka tayari Mwanza walishafanya kazi kikamilifu ya kukusanya mapato ulitaka warudi tena kukusanya kwa watu wale wale walio lipa?

Tatizo la lileta mada Lina CHUKI kaliiii na Mwanza mpaka linakesha likiokoteza kilakoa na Mwanza. Ukienda kwenye uzinwa Njombe vs Kahama unalikuta, ukienda Arusha vs Mwanza unalikuta, ukienda Dodoma vs Mwanza unalikuta.

Kama kweli unataka kuona kuina uhalisia wa mapato, angalia:

  • percentage ya target na siyo figure za mapato ya awamu.
  • angalia pia total amount iliyokusanywa kwa mwaka wa fedha, na siyo mapato ya robo mwaka.

Kama Kuna msukuma alikupiga pampu na hakukulipa, weka beef na yeye na siyo mikoa yote wanayokaa wasukuma.
Mbona povu jingi Sana mkuu,sio mimi nimeleta Takwimu ni Tamisemi ,more ni mjumbe tuu Sasa unataka kumuua mjumbe? Mjumbe hauwawi 😂😂.

Chuki za nini mkuu,utakula actual figures au percentage?

Mwanza imeshapigwa bao ,jipangeni kuzalisha zaidi sio kuchukia 😆😆
 
Angalia hichi kipande kwenye Halmashauri za Majiji...View attachment 2214870
Sasa baba wewe umekisia kukusanya bil.15 ukakusanya bil.12 ni wazi percentagewise uko vizuri ila mwenzio mfano Arusha amekisia kukusanya bil.23 akakusanya bil.18 ,ni kweli percentage wise yuko chini ila vipi kwenye mapato halisi nani anayo mengi?

Watu hawali percentage bali pesa halisi,ndio maana hata makisio yenu ni kidogo kwa sababu nyie ni maskini hamna pesa..

Mwisho hoja ni mikoa sio majiji ,kwa hiyo weka gragh za Mikoa kama mada ilivyo.
 
Tatizo hili nalo ni jambo la kisiasa sana hapa nchini. Hizi namba zinaandikwa kwa utashi wa mtu fulani ili kuwafurahisha watu fulani ila kiuhalisia hali ya kiuchumi iko tofauti kabisa, hali ya maisha ya watu katika eneo iko tofauti kabisa na makusanyo yanayooneshwa kwenye takwimu.

Jambo la msingi kila mmoja apambanie ugali wake na wanae kama anao. Mambo ya makususanyo uziachie halmashauri, wakusanya ushuru wenyewe na mkurugenzi maana wao ndio wanufaika wakubwa wa ushuru huo. Ni jambo la kawaida kukuta EFD mashine yenye zaidi ya mwaka mmoja haijafanya kazi katika kiziuzi cha wakusanya ushuru hali makusanyo yanafanywa kila siku na kuishia mikononi mwa watu wachache kitu ambacho kinakuja kuathiri makusanyo ya jumla ndani ya halmashauri.

Halmashauri za wajanja huenda ndio zinazoning'inia huko mkiani au katikati. Huku wanaojifanya wana mbio sana ndio wako mstari wa mbele kabisa!
 
sahihi kabisa umasikini ukitamalaki alafu kuna wengine wachache wanafaidi rasilimali za taifa lazima watu watachinjana siku za usoni.
Nyie ndio maana huwa mnauana Sababu ya umaskini uliokithiri..

Hayo mapato hutumika kwenye Halmashauri husika hayaendi kokote.
kwaio kama mapato yanaenda popote ndo muibe?.acheni wizi wa fedha za umma.
 
Back
Top Bottom