Mwanza waongoza kwa ukuaji mkubwa wa mchango wake katika pato la Taifa (GDP) 2016

Wenzetu mfano USA kila Jimbo linapambana na hali yake , hii inasaidia kila mkoa ungebuni vyanzo vya kupata mapato.
Nahisi watawala wengi wa kiafrika hurundika karibu pato lote la taifa sehemu ambapo wazungu/wafadhiri wanapofikiaga pindi wanapotembelea nchi husika ili kutaka kuwaaminisha kama ile misaada wanayotoa inatumika vizuri.

Mfano hivi yule mtawala alikuwa na lengo gani la kupinga kuwa watu wa Mwanza walikuwa wanashindwa kununua samaki badala yake wakawa wanakula mapanki. Tena si bora kipindi kile tulikuwa tunaweza kupata hayo mapanki, siku hizi nirahisi zaidi kupata kilo ya nyama kuliko hilo panki, leo hii panki ni dhahabu.

Nilisikia kiongozi mmoja wa Amerika siku alipotembelea Tanganyika kule Dar ombaomba wote walisafishwa mjini sasa nini lilikuwa lengo.
 
Nafikiri hatutasikia tena ule ubishani ni mji gani unafuata badala ya Dar, na ule mpambano wa Arusha vs Mwanza umeisha rasmi mpaka takwimu hizi zibadilike.
Wanaoupambanisha Mwanza na Arusha, kuna kitu huwa wanakisahau kimoja kuwa kuna mji huwa unakuzwa na nguvu ya strategic position yake lakini mwingine unakuwa kutokana na strategic policies. Hapo unajua who is who.
Ndiyo maana, kwa Mwanza Serikali ikiongeza tu nguvu kidogo, Mkoa na jiji vitapaa sana kiuchumi maradufu.
Hata hivyo, niliwahi kuweka humu bandiko lisemalo "Mwanza jiji pekee nchini lenye uwezo wa kuleta ushindani kwa jiji la Dar" Hilo bandiko is there to stay wazee.
 
Hiyo ndiyo hoja yangu. Binafsi ni mfuatiliaji mzuri wa masuala ya kiuchumi kwa miaka kadhaa!!! Kwenye hii mada naona wana-Mwanza wapo so excited wakati sioni kipya! Wapo so excited kwa sababu wanachanganya hizi taarifa za kiuchumi! Kwavle mwaka jana iliripotiwa Mwanza ni among the poorest regions, hii taarifa inawapa ahueni. Wanachosahau au wasichofahamu ni kwamba, hata pale zilipotoka taarifa za kwamba Mwanza ni among the poorest regions, bado Mwanza ilikuwa ni among the top contributors wa GDP!

Hata mwaka 2015, Mwanza ilikuwa ni second after Dar es salaam!

Sijawahi kusikia Mwanza inakuwa nje ya top 5 kwenye uchangiaji wa pato la taifa, na in fact, mara kwa mara inakuwa ni ya pili after Dar es salaam.

Sasa kama ni kitu cha kawaida, ni kwanini watu wapo so excited?! In fact, wanachanganya takwimu!!

The problem ni kwamba, ingawaje mara kwa mara Mwanza ni top contributor wa GDP bado kwenye taarifa za umaskini inakuwa among maskini kwa sababu hizo ulizotaja hapo juu! Wengine wanachanganya Mkoa wa Mwanza na Mji wa Mwanza! Wakati shughuli nyingi za kiuchumi zipo mjini Mwanza, Generally speaking, zaidi ya 75% ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza wanaishi vijijini na shughuli zao kubwa ni kilimo. Tangu zao la pamba likose soko, hawa wananchi wamekuwa hawana zao maalumu la biashara!

Shughuli zinazochangia kwa kiasi kikubwa GDP kwa Mwanza ni shughuli za wachache. Tofauti na Kilimanjaro kwa mfano. Kilimanjaro mara kwa mara sio top contributors wa GDP.... Hata hivyo sio among the poorest kwa sababu shughuli nyingi za Kilimanjaro ni za wananchi wenyewe; hususani biashara.

Endapo Manispaa ya Mwanza ingekuwa ni mkoa unaojitegemea kama ulivyo Dar es salaam; am sure isingekuwepo kwenye orodha ya mikoa maskini. Lakini mara kwa mara inakuwepo kutokana na idadi kubwa ya wananchi wanaoishi vijijini!
Wewe unasema kweli kabisa ndiyo maana Mimi taarifa ya mwaka jana nilikuwa siishangai kabisa, isipokuwa watumiaji wa mitandaoni ndio waliitumia vibaya kwa kuudharau mji wa Mwanza kuwa, unajitapa kushindana na Arusha wakati ni masikini kiasi hicho.
Hivyo narudia kusema wazi kuwa, licha ya Mkoa wa Mwanza, on per capita basis kuwa masikini kulinganisha na baadhi ya mikoa yenye kipato kikubwa, bado jiji la Mwanza ni tajiri sana na huwezi kulilinganisha ovyo ovyo na vimiji vyenye wakazi wapatao 500,000 wakati lenyewe linakaribia milioni moja.
Kila nchi vimiji vya saizi ya kati vinatendi kuwa na on per capita gdp kubwa kulinganisha na miji mikubwa. Mfano mzuri ni jinsi jiji la Frankfurt lenye wakazi 700,000 pekee linavyoipiga miji yote mikubwa na tajiri sana Ujerumani ya Berlin, Hamburg na Munich licha ya kuwa na wakazi zaidi ya milioni 3.5; 1.7 na 1.3.
 
Wenzetu mfano USA kila Jimbo linapambana na hali yake , hii inasaidia kila mkoa ungebuni vyanzo vya kupata mapato.
Huo ndo mfumo wao, ila kwetu tuko na mfumo tofauti na una malengo mema sana. Hata ktk levo ya familia tu, ni nani awezaye kumwacha mwana familia wake afe kisa tu kwake ni masikini hana kipato? Kwakuwa Iringa na Moro wana umeme, Ufike Mwanza kibiashara wakiuziwa na toka mikoa hiyo? Mtwara wana gesi, waimiliki wao tu? Familia haiko hivyo.
 
NDIVYO INGEKUWA VIZURI.KUNA NCHI ZA ULAYA ZINAENDESHA NCHI KWA KUVUA TU SASA JIULIZE TANGA,MTWARA ,LINDI JE SEKTA YA UVUVI INA MCHANGO GANI :eek::eek::eek::eek::eek::eek::eek:
 
Wewe ni mbishi sana, wengi hatukatai mfumo huu uliopo wa serikali kukusanyanyia hadhina mapato yote alafu inaanza kusambaza tena sehemu zote kwa kuanaglia mahitaji.

Tunachopinga ni serikali kukusanya kutoka kila eneo lakini ikaelekeza karibu nusu ya makusanyo hayo Dar pekee.

Dar tayari ulikuwepo uwanja mpya wa michezo lakini ule uwanja wa Taifa wa zamani umejengwa upya.

Dar tayari kulikuwa na terminal 2 za uwanja wa ndege lakini imejengwa tena terminal 3.

Dar kulikuwa na haspitali zote muhimu katika nchi hii lakini imejengwa nyingine pale Mloganzila.

Wameongeza maghorofa mapya pale Mlimani wakati hayo majengo yangwweza jengwa mikoa mingine kama mwanzo wa chuo kikuu kipya,

Barabara nyingi kule zinajengwa na wizara wakati huku zinachiwa halmashauri na nilishangaa mpaka taa za barabarani zinalipiwa bill ya umeme na wizara,

Miladi karibu yote ya ujenzi wa nyumba za taasisi za serikali hufanyika kule.

Yaani wao ndio wanasababisha watu wakimbilie kule kurundikana kwenye kamji kadogo alafu inapotokea tatizo la foreni za magari wananza kuchukua mafungu ambayo yangekuja jenga uwanja wa ndege huku wanayatumia kule.

Usizani watu wanapenda kuacha makwao na kukumbila kule ni basi tu fulsa hazipelekwi makwao.

Yaani msaada mkubwa naouona kwa sisi tunaoitwa wa mikoani ni kulipiwa mishahara ya watumishi wa umma tena wengi wakiwa ni hawa wa TAMISEMI.
 
Sawa, mi ktk hilo sina ubishi hata kidogo, ninachokikataa ni yale tu mawazo mgando kwamba, kwakuwa Moro kuna vyanzo vya umeme vyingi, basi pato la umeme huo liinufaishe Moro tu na si kunufaisha taifa lote. Hapo tu.
 
Wewe ni mbishi sana, wengi hatukatai mfumo huu uliopo wa serikali kukusanyanyia hadhina mapato yote alafu inaanza kusambaza tena sehemu zote kwa kuanaglia mahitaji.

Tunachopinga ni serikali kukusanya kutoka kila eneo lakini ikaelekeza karibu nusu ya makusanyo hayo Dar pekee.

Dar tayari ulikuwepo uwanja mpya wa michezo lakini ule uwanja wa Taifa wa zamani umejengwa upya.

Dar tayari kulikuwa na terminal 2 za uwanja wa ndege lakini imejengwa tena terminal 3.

Dar kulikuwa na haspitali zote muhimu katika nchi hii lakini imejengwa nyingine pale Mloganzila.

Wameongeza maghorofa mapya pale Mlimani wakati hayo majengo yangwweza jengwa mikoa mingine kama mwanzo wa chuo kikuu kipya,

Barabara nyingi kule zinajengwa na wizara wakati huku zinachiwa halmashauri na nilishangaa mpaka taa za barabarani zinalipiwa bill ya umeme na wizara,

Miladi karibu yote ya ujenzi wa nyumba za taasisi za serikali hufanyika kule.

Yaani wao ndio wanasababisha watu wakimbilie kule kurundikana kwenye kamji kadogo alafu inapotokea tatizo la foreni za magari wananza kuchukua mafungu ambayo yangekuja jenga uwanja wa ndege huku wanayatumia kule.

Usizani watu wanapenda kuacha makwao na kukumbila kule ni basi tu fulsa hazipelekwi makwao.

Yaani msaada mkubwa naouona kwa sisi tunaoitwa wa mikoani ni kulipiwa mishahara ya watumishi wa umma tena wengi wakiwa ni hawa wa TAMISEMI.
Hapa sasa ndo umeongea kitaifa, hilo mimi sitakupinga kabisa. Nilichokuwa nakipinga ni kusema kwamba mapato ya Mwanza yawekezwe Mwanza, na kujinasibisha na Umwanza wake. Huu ndio uasisi wa ukanda na ukabila, kwa pamoja tuupinge.
 
Hiyo ndiyo hoja yangu. Binafsi ni mfuatiliaji mzuri wa masuala ya kiuchumi kwa miaka kadhaa!!! Kwenye hii mada naona wana-Mwanza wapo so excited wakati sioni kipya! Wapo so excited kwa sababu wanachanganya hizi taarifa za kiuchumi! Kwavle mwaka jana iliripotiwa Mwanza ni among the poorest regions, hii taarifa inawapa ahueni. Wanachosahau au wasichofahamu ni kwamba, hata pale zilipotoka taarifa za kwamba Mwanza ni among the poorest regions, bado Mwanza ilikuwa ni among the top contributors wa GDP!

Hata mwaka 2015, Mwanza ilikuwa ni second after Dar es salaam!

Sijawahi kusikia Mwanza inakuwa nje ya top 5 kwenye uchangiaji wa pato la taifa, na in fact, mara kwa mara inakuwa ni ya pili after Dar es salaam.

Sasa kama ni kitu cha kawaida, ni kwanini watu wapo so excited?! In fact, wanachanganya takwimu!!

The problem ni kwamba, ingawaje mara kwa mara Mwanza ni top contributor wa GDP bado kwenye taarifa za umaskini inakuwa among maskini kwa sababu hizo ulizotaja hapo juu! Wengine wanachanganya Mkoa wa Mwanza na Mji wa Mwanza! Wakati shughuli nyingi za kiuchumi zipo mjini Mwanza, Generally speaking, zaidi ya 75% ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza wanaishi vijijini na shughuli zao kubwa ni kilimo. Tangu zao la pamba likose soko, hawa wananchi wamekuwa hawana zao maalumu la biashara!

Shughuli zinazochangia kwa kiasi kikubwa GDP kwa Mwanza ni shughuli za wachache. Tofauti na Kilimanjaro kwa mfano. Kilimanjaro mara kwa mara sio top contributors wa GDP.... Hata hivyo sio among the poorest kwa sababu shughuli nyingi za Kilimanjaro ni za wananchi wenyewe; hususani biashara.

Endapo Manispaa ya Mwanza ingekuwa ni mkoa unaojitegemea kama ulivyo Dar es salaam; am sure isingekuwepo kwenye orodha ya mikoa maskini. Lakini mara kwa mara inakuwepo kutokana na idadi kubwa ya wananchi wanaoishi vijijini!
Rekebisha usemi wako mwanza siyo manspaa bali mwanza ni jiji. Aidha kilimanjaro cyo wote ni wafanyabiashara. Wananchi wengi wa kilimanjaro wanafanyia biashara zao kwenye mikoa mingine
 
Ni kwavile tu home kwako, ila kimaisha, Mbeya ni bora hata si ya kulinganishwa na Mwanza. Sijasema kwa ukubwa wa miji, huko mi sipo. Nimeishi Mbeya na kuijua vyema Mwanza. Mwanza ni mji hatarishi, hauna uhai zaidi ya ziwa tu na lenyewe halijatumika vyema ingawa uwezekano upo mbeleni.
Wewe fafanua. Kimaisha kivipi ? Mbeya twalishwa red meet kila siku. Wakati mwanza unachagua ule unachokitaka. Samaki wabichi , red meet of all kinds ndizi aina zote kutoka bukoba na kanda maalum, dagaa wabichi na wakavu, kuku wa kienyeji n. K. Kwa vyovyote vile anayeishi mwanza anaenjoy zaidi ya yule wa mbeya , vinginevyo ni ushabiki usiokuwa na kichwa wala miguu.
 
Ndio mji wa pili kwa ukubwa ktk kanda yote ya ziwa. Mikoa kama saba hivi ipo ktk kanda hii. Ni miongoni mwa Miji kumi mikubwa nchini, hivyo Kahama si ya kubedhwa. Sema tu msingi wa uchumi wake si wa maana sana.
Wewe Kwa mara ya mwisho umefika kahama lini ? Tuulize sisi ambao ni kila Leo tuko kahama, kwa sasa kahama haiendi mbio sana kama miaka mitano nyuma. Na ifikapo mwaka 2020 mgodi wa buzwagi ukifungwa utakuwa mji wa kawaida sana. Wafanyabiashara wakubwa sasa wanahamisha biashara zao kahama kwa sababu mzunguko wa pesa ni mdogo kwa sasa.
 
Wenzetu mfano USA kila Jimbo linapambana na hali yake , hii inasaidia kila mkoa ungebuni vyanzo vya kupata mapato.
USA mbali,Kenya tu hapo ,yangu mfumo wa ugatuzi,kaunti zimeendelea sana maana zinashindana.Ujue ukifika Kenya utaona tofauti kubwa sana ya maendeleo yao na sie wabongo
 
Kahama huko ni migodi tu iliwachanganya watu baada ya kufungwa wafanyabiashara wore watasepa,ilifika mahala ati watu wakasema kahama iko mbele ya MBEYA,mmh nikabidi kuwa mpole lakini hebu tuombe uzima itakapofika 2020 kula MTU atapata picha ya wapi ni sehemu nzuri kuwekeza biashara ikadumu kwa mda mrefu..kuna miji ya kati iko ignored lakini siku za usoni ita offer economic potential sana mfano Tunduma,Makambako,Ifakara,Songea,Tunduru,Mpanda,Kilwa masoko,Karatu,Igunga,Babati,Mafinga,Njombe,Itigi na Mbamba Bay
Katika maeneo yote uliyotaja ni Tunduma tu ndiyo ninaweza kuikubali. Kwingine huko ni kujilisha upepo tu.
 
Kahama iizidi Mbeya? Sifa za kijinga sana, Kwahiyo Kahama inaipiku Morogoro? Haiwezekani, ila ni mji wa pili kwa ukubwa kanda ya ziwa na ipo ktk kumi bora nchini. Mbeya ina ustawi wa kudumu sawa na Wakinga na utajiri wao wa mbao, ni rasilimali yao ya kudumu.
Mbeya nilikuwepo june mwaka huu ni mahali pa kawaida sana. kwa mzunguko wa pesa mbeya mtasubiri sana.
 
A
Wewe fafanua. Kimaisha kivipi ? Mbeya twalishwa red meet kila siku. Wakati mwanza unachagua ule unachokitaka. Samaki wabichi , red meet of all kinds ndizi aina zote kutoka bukoba na kanda maalum, dagaa wabichi na wakavu, kuku wa kienyeji n. K. Kwa vyovyote vile anayeishi mwanza anaenjoy zaidi ya yule wa mbeya , vinginevyo ni ushabiki usiokuwa na kichwa wala miguu.
Acha uongo,tangu lini mjini kukakosekana chakula,? Kuna dagaa na samaki wa Nyasa,Tanganyika,Rukwa na hao kutoka Victoria,na kila aina ya mazao ya kilimo na matunda sio kama kanda hiyo ambayo mvua zinabahatisha except Kagera labda na Tarime
 
Katika maeneo yote uliyotaja ni Tunduma tu ndiyo ninaweza kuikubali. Kwingine huko ni kujilisha upepo tu.
Pengine ww unatazama hali ya LEO kuliko kesho,sidhani kwamba eti by 2025 Tunduma itakuwa mbele kuishinda Ifakara au Mpanda ,ni ishu ya mda tu coz barabara ndo zinajengwa maeneo hayo kwa sasa ili ku unlock potentials
 
Kahama ile hata sio manispaa nieleze kivipi maana naona ni kama mtukula tu au useme inakua kwa kasi ila haijauzidi tabora na bk
Kiukweli kahama ni kati ya miji kumi mikubwa Tzn,kutoitwa manispaa ni michakato tu ya kisiasa ila vgezo vyote inavyo..Ila jambo la msingi kuelewa ni kwamba sustainability yake in terms of future growth ni ndogo coz hakuna supportive factors nyingi zaidi ya migodi
 
Wewe Kwa mara ya mwisho umefika kahama lini ? Tuulize sisi ambao ni kila Leo tuko kahama, kwa sasa kahama haiendi mbio sana kama miaka mitano nyuma. Na ifikapo mwaka 2020 mgodi wa buzwagi ukifungwa utakuwa mji wa kawaida sana. Wafanyabiashara wakubwa sasa wanahamisha biashara zao kahama kwa sababu mzunguko wa pesa ni mdogo kwa sasa.
Eti ni kweli kahama inaizidi bukoba na tabora kwa sasa ? Mimi simuelewi ananiletea takwimu za miji kumi tz wakati hivyo uwekwa na watu kwenye google .wakati kanda ya ziwa mji wenye uhusiano,na unaogelewa zaidi hapa mwanza ni bukoba ndo maana tunahitaji meli mfano mwanza inaitegemea bukoba kwa ndizi, sukari,kahawa biashara na mtukula.na pia bk inaitegemea mwanza kwa vingi pia hivyo baada ya mwanza bk ndo inafuata kanda ya ziwa kahama bado kwa bk na tabora bado ni miji mikubwa ikizingatiwa ni manispaa bado na kahama ni mji tu unaochangamka
 
A

Acha uongo,tangu lini mjini kukakosekana chakula,? Kuna dagaa na samaki wa Nyasa,Tanganyika,Rukwa na hao kutoka Victoria,na kila aina ya mazao ya kilimo na matunda sio kama kanda hiyo ambayo mvua zinabahatisha except Kagera labda na Tarime
Huwezi kupata dagaa wabichi pale mbeya hata hao samaki wa kyela kuwapata ni shida. Kawadangaye wasiofika mbeya. kama unazungumzia viazi mviringo na unga wa mahindi hapo sawa. Na mwanadamu haishi kwa kula wanga tu bali hata kwa kila kitoweo kitokacho majini
 
Back
Top Bottom